Hivi huo Ualimu wenye dhiki mnaoongelea ni Ualimu upi huo?
Maana mimi kuna brother yangu ni Mwalimu yuko Tabora ana mkwanja kunizidi mimi niliyeajiriwa sekta nyingine serikalini. Pamoja na kwamba ana takehome ndogo ya 900,000/= ila ana mizinga ya nyuki kama 130, analima tumbaku hekari nyingi, na ana Shamba la miti ya mbao hekari 20. Mwaka juzi kavuna miti kadhaa kala milioni 70 simple tuu. Sasa ni Ualimu upi wa dhiki mnaouongelea nyie?