Unajuaje gari imechezewa umbali wake uliotembea (tempered with milleage)?

Mhandisi Mzalendo

JF-Expert Member
Aug 23, 2010
6,017
9,738
Habari wakuu,

Je kwa sisi/wao wanaonunua haya magari nee a.k.a second hand from outside africa. Je, unajuaje mtu kacheza na milleage/km za gari? Mfano km ilizotembea gari ni 120,000 km ila mtu anakuuzia 45,000 km. Je, hapa utatambuaje?

Uzoefu:
Nishawahi kununua gari ya 76,000 km/milleage kumbe ni 120,000 hapa bongo.

Tupeane ujuzi.
 
Ni ngumu kutambua kwasababu njia iliyopo ambayo watu huitumia ni kwa kuangalia uchavu wa gari katika sehemu mbali mbali mfano kwenye steering wheel na pedal zote.
 
Kwa faida ya wale wanaonanunua hapa nchini kwa wasambaa, wapare, wagogo linganisha Umri wa gari kulinganisha na mwaka wa usajili nchini kulinganisha idadi ya wamiliki kulinganisha na km ilizotembea zinazosoma kwenye dash board. Kama hazileti uhalisia km zimechezewa.

Mfano: Gari ya 2000, imeingia nchini 2011(Miaka kumi baada ya kutengenezwa) unauziwa leo 2021, ina km 107,000/=. Hapo ni kwamba kila mwaka ilitembea km avarage 5000 tu tangu kutengenezwa sasa akili kichwani kwako.

Kwenye idadi ya wamiliki kama previous kwenye kadi ni 0, lakini anayekuuzia si mwenye jina la kadi hiyo gari historia yake ya umiliki ina walakini, huwezi jua imepita mikono mingapi bila kubadilishwa kadi
 
Back
Top Bottom