Unajua unamiliki nini kati ya asset au liability?

Unajua unamiliki nini kati ya asset au liability?

bomouwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Posts
1,149
Reaction score
800
Habari za asubuhi hii wajameni!

Nimekua nikichunguza mambo ya vijana hususani wa mijini na hasa wale ambao wanahisi maisha kwao ni kua na gari zuri,nyumba nzuri,na masimu makubwa makubwa na mambo mengine kadha wa kadha.

Lakini nadhani kuna mambo ya msingi sana ambayo vijana tunahitaji kuyafikiria kabla ya kufanya hasa ukizingatia maisha ni mipango na sio mitazamo kama vile watu wanajua.

Labda nije katika mada husika kama vile inavyosema hapo juu kwamba unajijua unamiliki nini kati ya asset au liability?

Kwa wale ambao hapa tumeachana kidogo nirahisishe kwa kusema hivi, yaani uksma ASSET maana yake isiyo rasmi ni kitu kinachokuingizia na LIABILITY ni kitu kinanachokutoa katika mfuko wako. Nadhan hapa sasa tumeelewana walau kidogo yaani.

Kumekua na lindi la vijana wengi sana ambao wamekua wakipambana ili wajikwamue kimaisha na kuhakikisha wanakua na maisha bora kama chama chao kinavonadi sera zake."maisha bora kwa kila mtanzania".labda tujaribu kuhoji mfano huu.

BWANA X:huyu amejenga nyumba yenye garama ya fedha za kitanzania 78milioni na ameamua kuipangangisha kila mwezi akipata laki350,000 kutoka kwa mpangaji wake lakini wakati huohuo bwana x anaishi katika nyumba ya kupanga anayolipa kiasi cha shilingi za kitanzania 80,000 kwa mwezi.

BWANA Y:
huyu amejenga nyumba yenye thamani ya shilingi za kitanzania 57milioni na ndipo anapoishi kwa sasa ingawa anailipia nyumba hiyo maji,umeme,kodi ya jengo,kodi ya ardhi n.k.

Sasa tuje katika uhalisia wa kimtazamo kama vile jinsi binadamu tulivowazuri kunanga wenzetu kuliko kusifia,angalia hao bwana x na y jinsi ambavyo wote ni wamiliki wa nyumba zao tena halali kabisa lakini angalia ni kwa jinsi gani hawa mabwana wamezidiana uelewa wa kumiliki asset na kumiliki liabilty!

Bwana x anafaidika kwakua garama za malipo ya maji,umeme hazipo katika matumizi yake ya mwezi na hivyo kumfanya aongeze pato kwa kua anaasave kiasi hicho ukilinganisha na bwana y.

Sasa vijana wengi hua nawaangalia kwa jinsi walivo na maisha ya kiliab ility kwakua wanakua wanavitu visivokua na tija katika maisha yao kuliko kuwekeza kwenye vitu ambavyo vinamsingi kwao.

Kijana anaingiza mshahara wa laki4 labda lakini cha kushangaza anamiliki simu au tab ya kuanzia laki5,ieleweke si mbaya kumiliki tatizo katika principles za uchumi mtu huyu ni limbukeni maana anamatumizi yaliozidi kipato chake.

Unakuta kijana kapanga nyumba nzima lakini kipato chake ni kidogo kulinganisha na kodi ya laki250 kwa mwezi ila kwa kuwa anahitaji washkaji wamuone anajua na ana mipango basi maskini ya Mungu anajiumiza na kwa kuongeza kamkopo ka kununua IST au VITZ au PASSO basi ilimradi mshahara uingie hata laki150 imsogeze kwa mwezi.

Nawasihi vijana jifunzeni kubadilika na ujue kusema "MIMI NI MIMI NA NINAWEZA" kwa kua kila jambo linawakati wake hivyo ni muhimu sana vijana mkaweka nguvu katika kuwekeza kwenye assets kuliko liaabilities ambazo mnahisi ni muhimu kumbe ndizo zinazowarudisha nyuma katika maendeleo yako.

Kataa pepo la mikopo isiyokua na tija kimaendeleo ila chukua mkopo wenye kuleta tija ya kuongeza kipato chako cha kila siku na uendelee kuongeza malengo yako kwa kuona faida ya uwekezaji wako kadri siku zinavoendelea kwenda mbele.

Gari,simu,nyumba vinaweza kuwa assets na visiwe liability tena kwako.ANZA SASA.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU BARIKI VIJANA WA TANZANIA

 
Mimi nina liabilities kibao, Assets zero am still finding one
 
Dah somo zuri sana mkuu be blessed mada hii imenikumbusha walimu wangu wakati nasoma shahada ya kwanza Dr. Ulomi na Dr Urasa.
 
hivi hesabu hii watu walikuwa hawaijuwi poleni sana sana! binafsi nyumba yangu hunipatia laki 5*12=6mil,nimerent nyumba tabata nalipa 90 elfu *12=1,080,000 na 7itaki mambo ya personal transport itanigharimu mafuta// am busy on toping assets
 
hivi hesabu hii watu walikuwa hawaijuwi poleni sana sana! binafsi nyumba yangu hunipatia laki 5*12=6mil,nimerent nyumba tabata nalipa 90 elfu *12=1,080,000 na 7itaki mambo ya personal transport itanigharimu mafuta// am busy on toping assets

Nmeipenda hii Style yako ya Maisha kwani, hapo Watoto watasoma kwa Burudani bila Bugudha,wahsindwe tu wao.

Vijana wengi tunaona ni dili kutembea na Masimu makubwa ya 1M na kuendelea huku tukijisahau kutengeneza Assets kwa ajili ya maisha yetu ya Baadae.

Mfano: Hii leo hapa Bongo ukibahatika kumiliki Mijengo ako Miwili hadi Mitatu inayoweza kukuingizia Wastani wa Tsh 1M, basi ww utakuwa ushajikwamua katika lile kundi la watu Maskini.

Vijana tuliowengi huwa tunafikiria kuwa tukiishapata Pesa nyingi kwa Mkupuo ndio tutajenga. Kwa mawazo haya tutaishia kupanga tu kwenye nyumba za watu.

Tuamke na tumbane. Bado hatujachelewa.
 
Ningemjua Tajiri mmoja tu aliekufa na akazikwa na nyumba,gari,mashamba,ningetumia 90%ya muda wangu kuvitafuta.
 
Ningemjua Tajiri mmoja tu aliekufa na akazikwa na nyumba,gari,mashamba,ningetumia 90%ya muda wangu kuvitafuta.

Kauli za kimaskini hizo.hata mitume wa mwenyezi mungu walikuwa wanatafuta rizki na kufanya biashara.na wala hujaambiwa utumie muda wako wote kutafuta pesa na mali.na hakuna dini inayotukuza umaskini.hivi wote mkiwa maskini hizo zaka zitatolewa na nani
 
Good lesson kwa mtu aliye tayari kujifunza big up kaka maana haya ndio mambo ya msingi kuliko kukaa mkisifia watu kwenye mitandao.
 
Ningemjua Tajiri mmoja tu aliekufa na akazikwa na nyumba,gari,mashamba,ningetumia 90%ya muda wangu kuvitafuta.

kwani kuna masikini anayezikwa na kigoda, kibatari na kandambili?

Huu ni ubinafsi sasa, yani unataka uzikwe na mali zako mkeo na wanao waanze upya!

Acha hizo bana.
 
Back
Top Bottom