Mfiaukweli
JF-Expert Member
- Aug 30, 2018
- 5,636
- 8,774
Mara ya kwanza na pekee hadi leo Taifa Stars kucheza fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (kipindi hicho yakijulikana kama Kombue la Mataifa Huru ya Afrika) ilikuwa ni mwaka 1980. Kipindi hicho kulikuwa na mashindano makubwa matatu ya soka nchini:
1. Ligi kuu
Ilichezwa kwa mtindo huu:
Kutafuta Bingwa wa Wilaya (timu za kata kwenye wilaya husika zilicheza kupata bingwa wa wilaya; baada ya bingwa kupatikana wachezaji walioonyesha kiwangonbora kutoka timu zilizoshindwa walikuwa huru kujumuishwa kwenye timu bingwa).
Kutafuta Bingwa wa Mkoa (klabu bingwa za wilaya kwenye mkoa husika zilichuana kupata bingwa wa mkoa. Bingwa wa mkoa pia alikuwa na hiari ya kuimarisha kikosi chake kutoka kwenye timu zilizoshindwa kwenye msimu husika)
Kutafuta Bingwa wa Kanda. (Mikoa kadhaa iliunda kanda moja, na mabingwa wa mikoa husika walicheza kutafuta bingwa wa kanda).
Kutafuta Bingwa wa Taifa (mabingwa wa kanda walicheza kwenye kituo kimoja kwa mfumo wa ligi na aliepata points nyingi ndie aliekuwa klabu bingwa wa Tanzania.
Kombe la Taifa
Kila mkoa uliunda timu (kutokana na wachezaji wazawa wa mkoa husika; mtindo wa mtoano ulitumika na kocha wa timu ya Taifa aliyatumia mashindano haya kuteua wachezaji wa Taifa Stars)
UMISETA
Mashindano ya shule za sekondari (kuanzia wilaya, mkoa, kanda hadi Taifa). Kombaini ya UMISETA Taifa ilicheza na kombaini ya shule za sekondari za Zambia. Ndipo kina Kalusha Bwalya walipojulikana.
Mfumo huu ulikuwa rahisi kuuendesha na timu hazikuwa na ulazima wa kuuza mechi kwa kuwa gharama za uendeshaji hazikuwa kubwa.
TFF rudisheni mfumo huo. Ushahidi ni kuwa tangu tuachane na mfumo huo Taifa Stars imekuwa kichwa cha mwendawazimu. Brazil haina mfumo wa home and away pia. Tusiwaige Waingereza na vinchi vingine vya Ulaya ambavyo:
(a) eneo ni dogo kwa hiyo timu kusafiri upande mmoja kwenda mwingine hauchukui muda mrefu hata kuathiri performance ya wachezaji
(b) miundo mbinu yao na sponsorships ni more advanced.
I rest my case.