Unajua malengo ya maisha yako hapa Duniani?

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,910
6,706
Ulimwengu wote huu ni kitu kimoja tuu...na unatenda Kwa kutegemeana kama vidole vya mkono au viungo vya mwili vinavyo tegemeana na hii ni Kwa viumbe vyote hai na vile visivyo viumbe hai.....Tazama okseni kutoka katika Miti, ni muhimu kwetu binadamu na viumbe wengine...mbolea kutoka kwetu ni chakula Kwa mimea...Tazama maji yalivyo muhimu kwetu viumbe , mimea inavyo tupatia chakula nk.....

Tambua Kila kiumbe kina Jukumu maalumu katika kutegemeana huku.. Tazama muhindi kazi yake ni kutoa mahindi tuu na Wala muhindi hauzai maembe, Wala mnazi hauzai njegere.. Ina maana hilo ndio jukumu lake na unatii kufanya hilo jukumu bila shida kabisaa...

Njoo kwetu Binadamu vile vile , hakuna binadamu alie zaliwa bila kuwa na LENGO KUU katika kutegemeana huku Kwa sisi Kwa sisi wanadamu!!! Wengine huja kama wasaidizi wa Kiroho, Wengine Matabibu, Wengine Kutulinda, nk...na huo ndio mpango wa Roho yako ulo upanga kabla hata haujavaa mwili...na ni wewe mwenyewe uliichagua mpango huo hata kabla haujava Mwili huo wa nyama!!!....

Jiulize hapo ulipo!! JE?? Unajua Lengo la Roho yako kuvaa mwili??? Ulikuja kutimiza nini katika mzunguko huu wa kutegemeana??? ....

Ulimwengu ni mkalimilifu , hauna upungufu hata kidogo...asicho nacho huyu anacho mwingine Ili Kwa umoja wetu tutimize Yale yalio katika Mwili na tuyafurahie maumbile!!!

Shida ilianza pale Tabibu anakua Mlinzi, na Mkufunzi anakua Daktari, Mtu wa msaada Kiroho hataki kabisa kazi hio anafanya biashara....kinacho tokea ni kufanya kazi Ili upate kipato tuu..na Wala sio lengo lililo kuleta hapa duniani...

Embu jiulize kazi hio unayo ifanya unafanya Kwa kua inakulea na inakipato kizuri au yalianza kwanza Mapenzi Kwa suala Hilo harafu baadae ndio shughuli hio ikaanza kukupa kipato??? Nini kilianza, ni sauti Yako ya ndani au kwakua ulikosa Cha kufanya kujikimu ki maisha???
Na je unaifanya Kwa Furaha TENA BILA KUISUKUMA kazi hio Kwa aina yeyote Ile au Kila siku unaipambania kazi Yako Kwa jasho na damu??? Au Hulali usiku Wala mchana Ili tuu kazi hio idumu???...Nafsi Yako inafurahia unacho kifanya ??? Au ikifika muda wa kwenda kazini unajikuta huna Raha kabisa unatamani mwisho wa wiki ufike Ili upumzike ...Nini unacho kipenda kutoka katika hicho unacho fanya, ni kipato au kazi yenyewe???... Nazani maswali hayo yatakufungua kidogo kutazama ufanyacho na kuanza kupata picha halisi angalau kidogo...

Tambua kama shughuli yako imejaa mikosi isio eleweka , unatumia nguvu nyingi sana katika kuitumikia lakini unazalisha kidogo, haikidhi mahitaji Yako na wanao kutegemea, Kuto kudumu, haikupi Furaha Wala liziko ya nafsi, unakua mtu wa kuipambania kazi, Muda mwingine unafanya lakini ndani mwako Wala hakukupi amani...nk tambua unakua upo katika shughuli ambayo sio Lengo la wewe kuwa hapa!!! Gari moshi (treni) inapita juu ya Reli...haipiti bara bara ya Lami Wala vumbi

Hapa ndipo lilipokuja suala la Maisha ni kupambana, maisha ni kuhangaika !!! Kwanini uhangaike katika kile kilicho kuleta hapa duniani??? Hapana huo ni uongo ..Kwanini upambane?? ..Muhindi haupambani kutoa mahindi unatoa tuu...samaki hapambani KUOGELEA. ..

Asilimia ya watu waliofanya makubwa na kuacha alama duniani walipo ondoka ni wale waliofanya shughuli zao kutokana na kutimiza Lengo lao la kuja hapa Duniani....

Anza kujisikia mwenyewe na kuisikia sauti inayo toka ndani mwako hasa unapokuwa umetulia na hauna linalo kusukuma kama majukumu nk...Nini unapenda kukifanya ambacho ni Jibu au msaada Kwa wengine? ?? huna lolote ambalo jamii tunaweza nufaika nalo??? Hapo ndipo yalipo mafanikio yako au je hakuna suala ambalo mala nyingine hua linajirudia ambalo hata ikipita miaka kadhaa lakini linajirudia tena, huwa unatakiwa kulifanya lakini unaogopa au unaona kama huna pa kuanzia au unaliona halifai lakini suala Hilo hua halipotei ambalo unahisi ukifanikiwa kulifanya itakupa liziko kubwa sana la nafsi yako..Tambua ndani mwako kunajua Kila kitu, na endapo utakusikia vizuri huko ndani mwako utapata jibu...

Watu wengine hujikuta tuu Kwa Neema wanafanya kile walicho takiwa kuja kukifanya hapa duniani ila wengine Hutokea mpaka maisha yawalazimishe kabisa labda kupitia kufilisika kabisaaa na kukosa msaada au wengine kupitia Magonjwa na waumwe mpaka wakose chakufanya kabisaa ndio kidogo kidogo waanze kuisikia sauti itokayo ndani mwao...ndio maana Kuna watu wengi sana baada mahangaiko makubwa ndio anakuja kuwa shujaaa...
 
Yaani wee jamaa Mungu akusaidie sana uvuke mipaka yote ya vikwazo..hii kitu muhimu sana ila wabongo lala Mmmm!!
 
Back
Top Bottom