MWANASIASA HURU
Senior Member
- Oct 4, 2012
- 180
- 240
Habari zenu wadau.
Binadamu sisi tuna mambo ya ajabu sana, kuna vitu huwa vinanishangaza na mojawapo ni hili la mtu kufariki na watu kulia kwa uchungu.
Mtu anapofariki ndugu, jamaa na watu wa karibu hulia kwa machungu, jibu la moja kwa moja ni kwamba wanamlilia marehemu kwa kuondoka kwake. yaani hawakupenda aondoke muda huo au siku hiyo au kabisa asiondoke.
Lakini je, vipi pale mnapolia kwa machungu, mara ghafla marehemu anapiga chafya halafu anaamka na kuanza kuwatazama, kisha ananyanyuka na kuwafuata ndugu walio karibu wakilia kwa machungu. Ni wangapi wataanza kufurahi upya kwa kuwa waliyekua wanamlilia sasa yu hai tena?
Kwangu mimi nina wasi wasi kuwa kila mtu atatafuta kona yake ya kupita na kama ni ndani basi wengine watatamani kuta zibomoke.
ilhali wangepaswa kufurahi na kuanza maisha upya na ndugu yao aliyefufuka.
wewe binafsi ungefanyeaje?