Unaishauri nini chadema kuelekea safari ya ukombozi, 2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unaishauri nini chadema kuelekea safari ya ukombozi, 2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Patriote, Apr 2, 2012.

 1. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #1
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kwanza kabisa napenda kuchukua nafasi hii kuipongeza sana timu nzima ya makamanda wa chadema na wananchi wa Arumeru kwa kuwapa raha watanzania kwa kufanya maamuzi yaliyo sahihi. Wana Arumeru mmetutendea haki watanzania wenzenu.

  Pili nawapongeza wananchi wa Kiwira-mbeya, Lizaboni Songea/Ruvuma, Mwanza na wale wa Tanga kwa kufanya maamuzi sahihi ya kuimwaga CCM.

  Aidha, naomba nichukue nafasi hii kukaribisha ushauri, maoni pamoja na constructive critisisms kwa chama na uongozi wa chama chetu ili tujipange vizuri katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu 2015. Ikumbukwe kuwa harakati za ushindi wa uchaguzi ujao zinapaswa kuwa zimeshaanza mana chama bado hakijafika maeneo mengi ya vijijini na kunachangamoto nyingi zinazokikabili chama chetu. Ni chama chetu ndicho kilichobeba matumaini ya watanzania waliowe wengi. Hivyo tunapaswa kushirikiana ili kukidhi matarajio ya watanzania na hivyo kushinda katika vita hii ya ukombozi.

  Ushauri wangu mimi, naomba kwenye website ya chama, ziwekwe contacts za viongozi wa chama waliopo katika ngazi za mikoa, wilaya na hata kata ili tuweze kuwasiliana nao moja kwa moja na kuwapa mbinu mkakati, maoni au ushauri. Nakaribisha maini yenu wanajamvi.
   
 2. m

  majogajo JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  zaidi mm ntamshukuru lwakatare katk kuorganize ulinzi na usalama.
   
 3. Mu-sir

  Mu-sir JF-Expert Member

  #3
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 3,633
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  mimi nashauri kwanza viongozi wa cdm wenye accounts zao humu wawe wanashiriki mijadala coz hii forum ndiyo inayoongoza hapa tanzania kwa hoja na mitazamo makini halafu wajipange zaidi kuelekea 2015 wasimamishe watu makini kugombea urais yasiwe yale ya kuweka mgombea mwenza ambaye hana elimu ya kutosha japo katiba inruhusu lakini siyo compatible na kizazi cha sasa kwa mtazamo wangu ni hayo tu.
   
 4. m

  mahangu Senior Member

  #4
  Apr 2, 2012
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 145
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Nashukuru sana kwa hatua uliyoichukua ya kukaribisha maoni na ushuri.

  Kwanza nami niungane na wewe kuchukua fursa hii kuwapongeza wananchi wenzetu wa Arumeru kwa kufanya maamuzi sahihi na kuitikia wito wa watanzania walio wengi wa kutaka mabadiliko, kwakweli wana Arumeru hatuna cha kuwapa zaidi ya " AHSANTENI SANA" , pili kuipongeza timu nzima ya kampeni iliyofanikisha ushindi huu na mwisho mshindi mwenyewe kwa kushinda kwa kishindo kama wana ccm wasemavyo.

  Niingie kwenye ushauri/maoni
  1. Kama ulivyosema CDM haijaenea sana maeneo ya vijijini ambako CCM hbado inangome nzito, kwa uapnde wa mijini kwakweli CDM inaelekea kuziteka kwa 95%. Nashuari uongozi uweke mkakati kwanza wa kuhakikisha wanawatumia viongozi wa mikoa, wilaya na kata ili kuweza kufanya itikadi na uenezi maeneo ya vijijini. Najua sehemu nyingi hakuna viongozi, sasa kwa kipindi hiki cha miaka mitatu iliyosalia, wahakikishe wanateua hata watu wa kushika uongozi kwa muda ili mradi tu wachague watu makini.

  2. CDM ielekeze nguvu zake nyanda za juu kusini mashariki- hayo ni maeneo ya mikoa na Lindi, Mtwara na Ruvuma. Mikoa hii kwakweli hasa Lindi na Mtwara, wananchi wanakiu sana na mabadiliko lakini hawajapata watu wa kuwahamasisha. Kwahiyo naomba nguvu pia ielekezwe huko.

  3. Cdm iache kuridhika mapema na kujibweteka kama CCM, wanasubiri uchaguzi mdogo ndo nguvu kubwa inaelekezwa, staili hiyo kwa maoni yangu sio endelevu na ina kigarimu chama fedha nyingi kutokana na kutakiwa kutumia pia nguvu nying. Waende vijijini kueneza habari njema, watoke maofisini mwao waende huko, bahati nzuri wabunge tunao wakutosha. ikiwezekana kila Mbunge apangiwe mkoa mmoja, awezeshwe then akatangaze siasa huko kama watu wa makao makuu ni wachache.

  4. Chama kiendelee kufanya mikutano mingi iwezekanavyo ya kisiasa ( sio maandamano), nasema sio maandamano kwa maana ya kuwa maandamano yaitishwe pale tu ambapo kuna jambo mahususi sana, si kila jambo lazima maandamano hapana. kifanye mikutano ya kisiasa ili kuwahamasisha watu kujiunga na chama na hata kujua wajibu wao wa kujiandikisha kupinga kura na kutouza shahada za kupingia kura. Kwa ufupi kufanya elimu ya uraia kwa wananchi. Mfano, DSM toka uchaguzi mkuu upite, CDM hawawahi hata kuitisha mkutano mkubwa hata siku moja na hilo linalalamikiwa na watu wengi japo waliomba sana, sasa hatuelewi chama ni kutojipanga au nini. wangefanya mkutano mkubwa jangwani au kidongo chekundu kwa ajili tu hata kuwashukuru wananchi kwa kuwaamini na kuwapa kura.

  5. Kufanya fund raising kila mkoa ili kupata fedha za kueneza siasa ndani ya mkoa husika. nasisitiza fedha zinazopatikana kila mkoa zitumike katika mkoa husika, kama kwenda makao makuu basi iende kiasi kidogo sana ( 5%). Tuliona kule Arusha jinsi fedha zilivyopatikana na namna watu walivyokuwa na uchu wa kuchanga zaidi.

  6. Chama kiendeshe mikutano katika majimbo yake yote, lengo likiwa ni kuwashukuru wananchi kwa kuwapa imani. Jambo hili CDM wanajisahau sana, uchaguzi ukipita hawarudi kufanya mikutano ya shukrani hata zile sehemu ambazo walishindwa sio mbaya wakarudi na kuwaambia wananchi jamani ahsanteni kwa kura kidogo mlizotupatia lakini uchaguzi ujao tunaomba mtupe nafasi. Tazama kama Igunga kwa mfano, chama hakijawahi kurudi kwenda kushukuru, fikiria toka kutokuwa na mgombe mpaka kura elf 23 kama sijakosea. Jamani viongozi, hili ni pungufu kwenu, rudini mkafanye mikutano ya Ahsante.

  7. Kujihadhari na propaganda chafu za CCM pamoja na Hujuma- Kukua kwa chama kuna changamoto nyingi sana, ni dhahiri CCM watakuwa wanakiwinda sana CDM na huenda wakatumia hata njia chafu kukivuruga ikiwemo kuwatumia/kuwanunua watu ndani ya chama ili wapandikize migogoro. Jambo hili ni la kuwa nalo makini sana tena sana, wapo wanachama/viongozi/wabunge wanaoweza kununuliwa wakaingiza migogoro ndanai ya chama na wakati mwingine kutoa kauli zisizo na mashiko na hivyo kuwafanya viongozi wetu muda mwingi kukaa kushughulikia migogoro. mfano tumeona kule Mbeya Mjini kuna mgogoro, ni wazi unapandikizwa na wapinzani wa CDM. Viongozi kuweni makini sana katika hili.

  Haya ni machache, ninayo mengi lakini naona kwasasa nitoe haya, niwaachie wenzangu nao wachangie ila la website kuwa up to date ni muhimu sana, na kutuwekea mawasiliano ya viongozi wote ngazi ya Taifa hadi Tawi ni muhimu sana ( simu, email etc)

  Ahnte sana
   
 5. N

  NYAMKANG'ILI JF-Expert Member

  #5
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 223
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  NASHAURI: (1) CDM wajitahidi kufanya siasa za issues, wanafanya hilo ila ningependa wafanye zaidi; (2) wahimize kwa udi na uvumba watu wajiandikishe kupiga kura, hasa vijana; (3) wapinge kwa nguvu zote utaratibu wa sasa wa wananchi kukataliwa kujiandikisha kupiga kura, kwa maana ya kuboresha daftari la wapiga kura. Ningependa watu wajiandikishe kupiga kura hata siku ya uchaguzi wenyewe, unajiandikisha hapo2 na kisha kupiga kura, kwani kuna tatizo gani; (4) CDM waanzishe TV channel ya mijadala kwani tangu uchaguzi 2010 naona kama CDM wako blacked out (definately na watawala) na TV zao hapa kwetu, huwaoni kwenye mijadala kama ilivyokuwa huko nyuma; na (5) watumie vizuri mchakato wa kutengeneza upya Katiba ili kubadili mfumo wa utawala wa nchi yetu kwa manufaa ya wote, badala ya ilivyo sasa.
   
 6. M

  Mussa Haruni Member

  #6
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  viongozi,wanachama,wapenzi,wafuasi.......kila mmoja afanye jukumu lake...wote wasibaki wanafikiria kushinda uchaguzi uliopo mbeleni...so wenye kupanga mikakati waendelee...wenye kupuni ni jinsi gani changamoto na ugumu wa maisha vitakabliwa nao waendelee......la msingi kila mmoja afanye sehemu yake kikamilifu
   
 7. m

  mkisah2 Member

  #7
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  1) Elimu ya Urai..haki na wajibu wa mwananchi( unajua kuna watu wanadhani shida ni haki yao)
  2)Operation Sangara
  3)kama issue ni pesa waanzishe fund raising watu tutachanga hata mia mia kwa Mpesa kwaajili ya kueneza habari za ukombozi vijijini
   
 8. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Acheni mawazo finyu nyie, Upinzani umejitambulisha wenyewe na unakuwa kwa mbinu na jitihadi zao wenyewe. Mistakes za Serikali ya JK ndio chachu ya speed ya kukuwa na kufanya vyema upinzani!
   
 9. u

  uwemba1 JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 755
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 60
  Tusisubiri mpk uchaguzi ndipo tunaenda kuwaangukia wananchi tujenge chama vijijini ili 2015 iwe kama kumsukuma mlevi uzuri watu ni waelewa bora uwaambie ukweli tu.
   
 10. Patriote

  Patriote JF-Expert Member

  #10
  Apr 2, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 1,718
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mimi nashauri chadema kiunde kamati/mabaraza ya wataalam mbalimbali ili wasaidie kukishauri chama katika kuweka mambo vizuri kutoka Bungeni hadi kwenye mambo ya jamii. Mabaraza haya yatafanya tafiti mbalimbali zitakazo kisaidia chama kuendesha shughuli zake. Kwa mfano, kazi ya mabaraza haya inaweza kuwa kufanya socio-economic assessment ya jimbo fulani ambalo chama kinategemea kumsimamisha mbunge katika uchaguzi ujao. Hii itawezesha chama kuwa na information za ndani kabisa tena kutoka kwenye horse mouth. Hivyo itakuwa rahisi sana kutumia information hizo katika kampeni husika.

  Mabaraza haya pia yatasaidia kuunganisha wanachama na kuandaa viongozi wajao mana inatakiwa tuwe na long term plans na sio kuwa na plans zinazoishia kwenye kupata madiwani na wabunge. Chadema kiassume kuwa 2015 kinakabidhiwa nchi, hivyo kinapaswa kuwa na viongozi waliotayari kukipokea ccm katika nyanja zote kuanzia wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wengineo ambao hadi sasa wanaiwakilisha CCM. Tusipo jiandaa vyema, itafika 2015 tukiwa bado hatujaiva kwa mabadiliko. Mungu ibariki Chadema, Mungu ibariki Tanzania
   
 11. e

  environmental JF-Expert Member

  #11
  Apr 2, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,054
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Sasa tuingie vijijini kwa kasi ya ajabu[operation sangara].na tuanze sasa.unajua ccm ameumia.anatibu kidonda kwa kuweka dawa ambayo kidonda sasa kimekuwa kansa .hahahahahhaaaaaaaaaaaaaa,pole mafisadi.mwisho ndio huu ,haturudi nyuma kabisa .
   
Loading...