Unaikumbuka Barcelona ya Frank Rijkaard?

Ile mechi barca ndio aliopigwa nne. Gaucho japo alifunga bao zuri ila kipigo kipo pale pale. Sasa messi hakufunga goli ila aliitoa chelsea na kwenda final kuchukua kombe.

Exactly Mkuu!!! Yeah barca alipigwa 4. Na King messi ndie aliitoa chelsea na kuipeleka tim yake final and then ikabeba ndoo.
 
All
alibebwa..akasababisha drogba kutaka kumdunda refa..akafungiwa..baadae xavi alikuri kushika ndani ya 18..ila mungu mkubwa 2012 barce wakatolewa peupe huku wakionekana kukosa mbinu

Sasa kama xavi alikiri kushika ndani ya 18 hayo ni makosa ya refa sio kubebwa. Ukweli ni kwamba makosa yanatokea sana hasa kwenye mashindo ya uefa kila msimu lazima timu angalau moja itolewe kwa uzembe wa refa. Msimu uliopita bayern katolewa kwa magoli ya offside na red card hawakulalamika wala kumpiga refa. Kabla ya hapo atletico alikosa ubingwa kwa goli la offside la ramos. Tatizo la chelsea bado wana mentality ya team ndogo refa akikosea wanasema anabeba. Huwezi kusikia timu kubwa kama barca, real, bayern wakisema refa anabeba. Hata guardiola alisema ni aibu kuona timu kubwa zinalalamikia refa
 
Sasa kama xavi alikiri kushika ndani ya 18 hayo ni makosa ya refa sio kubebwa. Ukweli ni kwamba makosa yanatokea sana hasa kwenye mashindo ya uefa kila msimu lazima timu angalau moja itolewe kwa uzembe wa refa. Msimu uliopita bayern katolewa kwa magoli ya offside na red card hawakulalamika wala kumpiga refa. Kabla ya hapo atletico alikosa ubingwa kwa goli la offside la ramos. Tatizo la chelsea bado wana mentality ya team ndogo refa akikosea wanasema anabeba. Huwezi kusikia timu kubwa kama barca, real, bayern wakisema refa anabeba. Hata guardiola alisema ni aibu kuona timu kubwa zinalalamikia refa
ile mechi ya Chelsea na barce haikuwa makosa ya kibinaadam..rais wa uefs platini kabla ya mechi alisema asingependa fainali ijirudie..yaani fainali ya man u na Chelsea..kisha tukaona maamuzi ya kijinga uwanjani..Barcelona wakishika Mara tatu ndani ya 18 na hakuna penati
 
Aloo umenikumbusha machungu mkuu, hii mechi ilinifanya niichukie sana michuano ya uefa champs league, yaani baada ya mechi kuisha sikuamini kabisa na ilichukua muda kuamini. Fara sana yule mu Hungary aliyochezesha hii mechi namuombeaga kifo mpaka leo!

Nikikumbuka milima tuliyopitaga mpaka tunafika fainali ule ubingwa ulistahili kuwa wetu, nakumbuka tulimtoa real Madrid tena ile galaticoz iliyokuwa na watu kama Ronoldo, Michael Owen,Robinho,Raul,Beckham na sio hii ya akina benzema. Tukamtoa na juventus liyekuwa mtawala wa ligi ya italy! Nusu fainali tukanusurika kwa Villarreal aliyokuwa tishio kule Spain... Yaani acha tu.

Mimi mpaka mpira unaanza nilikuwa sina wasi wasi kabisa nilijua Barcelona ni ronadinho pekee tu, na kweli Ebue na koro toure walimdhibiti sana ronadinho. Mambo yalikuja kuvurugika baada ya ile red card ya magumashi aloyopewa Lehmann. Ndio Barcelona wakaanza kucheza mpira wao, lakini pamoja na hivyo bado tuliwapiga goli na kuwakosa zingine nyingi tu.

Kuna huyu jamaa wa kuitwa Henrick Larsson huyu ndie aliyekuja kutuharibia sherehe kabisa sijui aliingia na dawa, yaani aliyoingia tu second touch akatoa assist kwa eto'o. Halafu Wenger nae alivyokuwa mwehu walivyochomoa akamtoa Fredrick Leunjberg akamwacha Alexender helb aliyokuwa anasumbuliwa tu na iniesta, tumepigwa goli la pili ana mtoa fabregas ana mleta flamin, nadhani alichanganyikiwa zaidi hata ya mashabaki.

Aisee ile mechi iliniuma sana lakini pia henry nae alitunyima ushindi sababu alipata clear chances kama tatu hivi yuko yeye na valdes halafu zote aliishia kumpa tu.

Anyway Niko Emirates hapa tunamkandamiza Spurs!
Pole sana!
 
Barcelona ya KING MESSI/GUARDIOLA ndio bora kuwahi kutokea.

In short King Messi ndie Barcelona na Barcelona bila ya Messi ingelikuwa ya kawaida sanaa. Messi ndie ameleta mabadiliko ktk timu,tik taka na kuipatisha mataji yasiyohesabika.

Messi Mungu akupe maisha marefu.
Mkuu Barcelona ya "Romario na Hristo Stoiczkow" ilikua mziki mwingine.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom