Unaijua skanka (Skunk)?

Unaijua skanka (Skunk)?

Endasak Masqaroda

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2013
Posts
1,565
Reaction score
3,664
Nafikiri umeshasikia neno skanka hapa na pale. Nafahamu unaijua kuwa ni bangi na wengine wanadhani skanka ni aina ya madawa ya kulevya tofauti na bangi. Skanka au Skunk ni bangi, lakini kwanini iliitwa Skunk?

DISCLAIMER: Mada hii inaletwa kwa lengo la kutoa elimu tu na utambuzi. Napinga matumizi ya dawa za kulevya za aina zote na siko hapa kusupport aina yoyote ya usafirishaji wa dawa za kulevya kama ilivyo katazwa na sheria za nchi zote duniani zinazokataza matumizi ya dawa za kulevya.

Sasa tuendelee......

Neno Skunk lilitokana na aina ya bangi iitwayo Skunk #1, ambayo ilitengenezwa miaka ya 1970 kwa kuchanganya aina tofauti za bangi ili kupata mmea wenye nguvu zaidi (au skunk), ni aina ya bangi inayojulikana kwa kuwa na nguvu (high potency) kuliko bangi ya kawaida. Jina linatokana na harufu yake kali inayofanana na mnyama anayeitwa Skunk. Upo?

Sifa kuu za Skanka:

1. Nguvu kubwa ya THC (tetrahydrocannabinol).

THC ndiyo kemikali inayosababisha kilevi kwenye bangi. Skanka mara nyingi ina kiwango cha juu cha THC kuliko bangi ya kawaida.
2. Harufu kali sana

Ina harufu nzito inayoweza kusikika mbali kidogo kutoka ilipo.

3. Hulimwa kwa njia maalum.

Mara nyingi skanka hulimwa indoor kwa kutumia taa maalum na mbolea ili kuongeza ubora na nguvu.

Athari za skanka.

Skanka hulevya zaidi kuliko bangi ya kawaida. Inaweza kusababisha:
a. Kizunguzungu
b. Wasiwasi au panic kwa baadhi ya watu
c. Mapigo ya moyo kuongezeka

Kwa kifupi:
Skanka si mmea tofauti kabisa, bali ni bangi iliyoboreshwa (hybrid) yenye nguvu zaidi na harufu kali.

Je, aina zingine za bangi ni zipi?

Kuna aina kuu mbili za bangi. SATIVA na INDICA. Sativa ni ile mmea wake unakuwa mrefu wenye majani membamba.....iko sana huku nchi za tropiki. Hii sifa yake ni kumfanya mtu awe na energy na creative zaidi. Ikakuvuruga akili unajiona unaweza sana😃😄
Indica kwa upande wake ni mimea mifupi yenye majani mapana. Hii inamfanya mtumiaji anasizz-mtu anakuwa mpole na/au huleta usingizi. Skanka sasa ni hybrid ya hizo mbegu hapo.

Hapa Tanzania tuna aina gani inayopatikana zaidi?
Tanzania inapatikana zaidi landrace sativa, indica ni nadra sana. Skanka huletwa zaidi kutoka nje hasa South Africa.

Kwanini skanka inapendwa sana Africa Mashariki?
Je, ni yepi madhara ya kimwili na afya ya akili kwa mtumiaji wa skanka?
Ntarudi.

Sources:
Overgrow.com.....one of the best landrace sativa from Tanzania.

420 magazine.....a landrace strain from Northern Tanzania.

Verilife: African Landrace Strains-Durban Poison & more sativas.

Pichani ni mnyama Skunk
 

Attachments

  • 2679.jpg
    2679.jpg
    38.1 KB · Views: 4
Back
Top Bottom