Unaifahamu hiyo familia?

Ronn M

JF-Expert Member
May 2, 2012
1,279
683
Nimalizapo weekend labda niseme hivi! Unaifahamu familia uliyooa/olewa au unayotaraji? Mara nyingi tumesahau jambo 1. Kila familia ina roho (asomae na afahamu) na tabia zake! Wengne wauaji,malaya,walevi,waongo,wagomvi,wachawi,washirikina,magaidi nk, nk! Kabla hujafikiri kuoa/kuolewa, ifahamu. Itakusaidia!
 
Lengo la wewe kuelewa ni 1. Dont be suprised for what you will find it there. 2. And may be the knowledge may help you in deciding wisely
 
Good point, ingawa ni vigumu kwa maisha ya sasa hivi ya kukutana mbali na kwenu/kwao!
 
yes ni vizuri kuifaham ila kiukwel huu uchumba wa kwenye mitandao ya kijamii ni ngumu kuijua familiy
 
Nimalizapo weekend labda niseme hivi! Unaifahamu familia uliyooa/olewa au unayotaraji? Mara nyingi tumesahau jambo 1. Kila familia ina roho (asomae na afahamu) na tabia zake! Wengne wauaji,malaya,walevi,waongo,wagomvi,wachawi,washirikina,magaidi nk, nk! Kabla hujafikiri kuoa/kuolewa, ifahamu. Itakusaidia!

Kwa sehemu kuna ukweli, lakini si kila aliye kwenye hiyo familia anaweza kubeba tabia za hiyo familia. Nimezifahamu baadhi ya familia kadhaa ambazo ni walevi kupindukia lakini unakuta kuna mmoja angalau anatokea kuwa tofauti na wengine! Zipo pia familia zenye kupenda ugomvi au uhuni lakini unakuta kuna masalia machache yasiyo na hizo tabia.

Ila all in all, naungana na wewe kwa 100% kuwa ni vzr kuhafamu familia ambayo unakwenda kuungana nayo!
 
nakumbuka kaka yangu wa kwanza kuzaliwa wakatim anatarajia kuoa, baada ya kumweleza baba, baba alifanya udadisi kujua alipotoka huyo mwanamnke, baada ya kujua atokapo huyo mwanamke, kisha akamwambia kaka asubiri atamjibu.Alisafiri kwa siri hadi huko kijijini na kufanya ushu-shushu wake na baada ya kurudi akamwambia kaka aende kule kijijini akamuone mzee fulani yeye ndiye atakayekuwa baba yake wa kumsaidia kuposa na kumfungisha ndoa.
Kumbe alishaongea na huyo mzee na kukubaliana naye amsdaidie kusimamia ndoa ya kaka yetu kwa kuwa huko kaka alipotarajia kuoa ni mbali na alipo na yeye alikuwa ni mtumishi asingeweza kusafiri kwenda huko.

Na utaratibu huo aliufanya hata kwetu sisi kufanya ushu-shushu kabla ya kutoa go ahead ya kuoa.

Ni jambo zuri sana kuijua familia unayooa au kuolewa, wazee walikuwa na maana zao kutukataza kuto-oa koo fulani.
 
Well said RM, kuna familia zingine balaa, ukipata story zao unaweza kughaili kuoa/kuolewa.
 
Nimalizapo weekend labda niseme hivi! Unaifahamu familia uliyooa/olewa au unayotaraji? Mara nyingi tumesahau jambo 1. Kila familia ina roho (asomae na afahamu) na tabia zake! Wengne wauaji,malaya,walevi,waongo,wagomvi,wachawi,washirikina,magaidi nk, nk! Kabla hujafikiri kuoa/kuolewa, ifahamu. Itakusaidia!

Its too late for some of us! Ila ushauri utasaidia kwa wadogo zetu.
 
Kwa sehemu kuna ukweli, lakini si kila aliye kwenye hiyo familia anaweza kubeba tabia za hiyo familia. Nimezifahamu baadhi ya familia kadhaa ambazo ni walevi kupindukia lakini unakuta kuna mmoja angalau anatokea kuwa tofauti na wengine! Zipo pia familia zenye kupenda ugomvi au uhuni lakini unakuta kuna masalia machache yasiyo na hizo tabia.

Ila all in all, naungana na wewe kwa 100% kuwa ni vzr kuhafamu familia ambayo unakwenda kuungana nayo!

Tuzungumziapo mambo mengi hua tunapenda kuweka asilimia nyingi, siku zote kuna wachache hujitokeza na kua tofauti na jamii yao inayowazunguka ila ukweli upo pale pale SIKU ZOTE jamii hufanana ndio maana koo,kabila,nchi, kuna vtu vingi hufanana miongoni mwao.

na hili sisi tunaoenda kuoa/kuolewa tulizingatie na kuliko kwenda kuondoa nuksi.
 
Wala siyo too late, hiki ni kizazi kingine kabisa, hii hoja ni Irrelevant kwa sasa kwani kuoa sasa hivi ni jambo la mkataba wa watu wawili tu. mke siyo wa Familia na mume si wa Familia.

Zamani kuna waliokuwa wanapenda kujipendekeza kuoa Familia faulani zenye uwezo wa kiuchumi lakini siku hizi hata kama utajipelekesha huko matatizo ya kiuchumi yakiwakumba ni yenu wenyewe.
 
Umenena mkuu, nashukuru kwa hili linafanyika sana kwenye familia yangu, mengine labda itokee bahati mbaya.
 
Kwa sehemu kuna ukweli, lakini si kila aliye kwenye hiyo familia anaweza kubeba tabia za hiyo familia. Nimezifahamu baadhi ya familia kadhaa ambazo ni walevi kupindukia lakini unakuta kuna mmoja angalau anatokea kuwa tofauti na wengine! Zipo pia familia zenye kupenda ugomvi au uhuni lakini unakuta kuna masalia machache yasiyo na hizo tabia.

Ila all in all, naungana na wewe kwa 100% kuwa ni vzr kuhafamu familia ambayo unakwenda kuungana nayo!

Tuzungumziapo mambo mengi hua tunapenda kuweka asilimia nyingi, siku zote kuna wachache hujitokeza na kua tofauti na jamii yao inayowazunguka ila ukweli upo pale pale SIKU ZOTE jamii hufanana ndio maana koo,kabila,nchi, kuna vtu vingi hufanana miongoni mwao.

na hili sisi tunaoenda kuoa/kuolewa tulizingatie na kuliko kwenda kuondoa nuksi.

Nakubaliana na wewe mkuu!
 
Kwa sehemu kuna ukweli, lakini si kila aliye kwenye hiyo familia anaweza kubeba tabia za hiyo familia. Nimezifahamu baadhi ya familia kadhaa ambazo ni walevi kupindukia lakini unakuta kuna mmoja angalau anatokea kuwa tofauti na wengine! Zipo pia familia zenye kupenda ugomvi au uhuni lakini unakuta kuna masalia machache yasiyo na hizo tabia.

Ila all in all, naungana na wewe kwa 100% kuwa ni vzr kuhafamu familia ambayo unakwenda kuungana nayo!

Na point yangu ni kuwa kama ukifahamu itakusaidia kuamua kwa hekima na usahihi
 
nakumbuka kaka yangu wa kwanza kuzaliwa wakatim anatarajia kuoa, baada ya kumweleza baba, baba alifanya udadisi kujua alipotoka huyo mwanamnke, baada ya kujua atokapo huyo mwanamke, kisha akamwambia kaka asubiri atamjibu.Alisafiri kwa siri hadi huko kijijini na kufanya ushu-shushu wake na baada ya kurudi akamwambia kaka aende kule kijijini akamuone mzee fulani yeye ndiye atakayekuwa baba yake wa kumsaidia kuposa na kumfungisha ndoa.
Kumbe alishaongea na huyo mzee na kukubaliana naye amsdaidie kusimamia ndoa ya kaka yetu kwa kuwa huko kaka alipotarajia kuoa ni mbali na alipo na yeye alikuwa ni mtumishi asingeweza kusafiri kwenda huko.

Na utaratibu huo aliufanya hata kwetu sisi kufanya ushu-shushu kabla ya kutoa go ahead ya kuoa.

Ni jambo zuri sana kuijua familia unayooa au kuolewa, wazee walikuwa na maana zao kutukataza kuto-oa koo fulani.

Mzee Mtambuzi, ths z true story. My brother, from my sister's mother, wanted to marry from a certain family. Wakati huo alikuwa very successful. Alikuwa anasupply mchele maeneo mengi dar. Alikuwa na maduka ya jumla. Wazee wakamkataza sana lakini akang'ang'ania. Alikuwa na certificate in teaching bt akawa anasema hawezi kufundisha. Since ameoa mambo yakawa hovyo. Akadrop day by day. Ninavyoandika sasa yeye ni mwl wa primary kipawa
 
Hapa unamaana kama mtu ni mlevi na aoe/aolewe kwa walevi
kama ni wachawi/washirikina waoane
Kama wauaji waoane
kama majambazi waoane
kama malaya na waoane

Hakika na kuambia utachunguza sana na kama hujapiga goti kumuomba MUNGU akupe mme/mke mwema kamwe hutopata!
Ushauri: Omba kwa MUNGU akupe mwenza bora kwa akili na macho yako hutompata kamwe.....

Unaweza ukaoa/olewa kwenye familia ya aina yeyote lakini kama Ulimwomba MUNGU na akakupa wa kutoka huko ni anamakusudi yake na yeye ndiye atamtengeneza aendane na wewe
 
cku iz m2 akilizika na tabia na yule amtakae bc imekuwa tosha sababu ndo anaeenda kaa nae, hajali haw wengine wakoje, ila n vzur kujua angalau kiunagaubaga 2 kuhs familia ucka
 
Its too late for some of us! Ila ushauri utasaidia kwa wadogo zetu.

Its never too late. You still have an option to check in depth nature of your family. There some things you can still change while you are in. Remember the emphasis is to raise a good life and good family!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom