Turbulence
Senior Member
- Apr 24, 2012
- 153
- 30
Kilimo Kwanza asante kwa taarifa muhimu. Ni kweli kilimo cha greenhouse kinalipa sana, kwa sababu tija ni kubwa mno! Lakini ni vizuri pia watu waelewe kwamba greenhouse haziwezi kufanya kazi Dar na maeneo mengine ya Pwani kutokana na joto kali na humidity. Greenhouse inakubali kwenye maeneo ya Altitude kuanzia 900m, lakini pia joto lisiwe juu ya 27. Kuna namna ambayo unaweza kufanya greenhouse ifanye kazi Dar, lakini ni high tech, kwa sasa hatuwezi. Watu wengi wa Dar walihamasishwa kununua greenhouse, na wakafanya hivyo. Matokeo yake walipata hasara kubwa, kwa sababu hawakuvuna hata robo ya robo waliyotarajia. Nawafahamu zaidi ya watu 140 waliofunga greenhouse, na sasa wamepata hasara kubwa, wanalia!!. Kitaalam, haishauriwi hata kidogo kufunga greenhouse Dar na Pwani. Ni costfful na painful experience.