vampire_hunter007
JF-Expert Member
- Jul 25, 2015
- 1,034
- 2,599
Habari wakuu, mimi ni mgeni humu naomba kutoa ya moyoni
Bunge ni sehemu muhimu sana ya kuhakikisha maslahi wa wananchi yanalindwa na wawakilishi wao waliowachagua. Lakini kinyume chake mara nyingi wabunge wa ccm wamekuwa wakilalamikiwa kupitisha na kuunga mkono hoja hata kama ni kandamizi kwa wananchi as long as hoja hiyo imetolewa na chama chao. Yaani kwa ufupi wamekuwa wakilalamikiwa kutanguliza maslahi ya chama kabla ya maslahi ya wananchi waliowachagua. Hili ni tatizo kubwa sana na ni miongoni mwa sababu kubwa sana zinazochangia umasikini wa watanzania.
Viongozi waliopo serikalini ni walewale wanaotokea katika jamii zetu. Yaani ni majirani zetu, kaka zetu, rafiki zetu, dada zetu, nk. Ni watu wanaotokana na sisi. Hivyo tabia za viongozi hawa kwa kiasi kikubwa huwakilisha tabia za wananchi wao. Na ndio maana kulalamika huku nimekuita unafiki. Ni sawa na wewe kujiangalia kwenye kioo kisha ulalamike kuwa ile taswira yako kwenye kioo ina pua kubwa na masikio marefu. Nitatoa mifano.
Sisi wananchi ambao tulitarajiwa kuwa mstari wa mbele kuwaweka sawa viongozi wetu, kuwakosoa wanapokosea, kuhoji panapotutia shaka na kuelekeza tunapoona kuna manufaa, sisi ndio tumekuwa tukitanguliza mapenzi yetu kwa hawa wanasiasa na kuweka maslahi ya taifa nyuma. Yaani kigezo cha kukubali taarifa na kuikataa imekuwa ni mapenzi yako kwa wanasiasa Fulani. Ikija taarifa mbaya kuhusu unayempenda utaipinga hata kama ina ushahidi na ikija taarifa mbaya dhidi ya usiyempenda utaishabikia na kuisambaza hata kama haina ushahidi.
Mifano.
Kuna siku zitto kabwe alipost document inayoonesha freeman mbowe ana pesa katika account nje ya nchi na si pesa ndogo. Na document ilikuwa ikitoa maelekezo kwa watu Fulani kulipwa. Zitto alipost na kuhoji uhalali wa kile kilichoendelea katika document ile. Katika hali ya kustaajabisha vijana wanaounga mkono chadema walimuattack zitto na kutetea document ile bila ya hoja zozote za msingi bali kwa mapenzi yao tu. Hawakuhoji wala kutaka kujua uhalali wa kuhifadhi fedha zile nyingi katika benki za nje. Wao walichokiona pale ni kuwa zitto “msaliti” anamfuata fuata mbowe na kuwa ametumwa na ccm. Hebu kuwa mkweli wa nafsi yako na jiulize kama ile document ingekuwa na saini ya Ridhiwani Kikwete kama reaction ya vijana hawa ingekuwa the same. HAPANA…. Unadhani ni kwa nini?
Siku chache nyuma gazeti moja lilipost picha ya mtu akimfuta viatu Ridhiwani kikwete na kusema mtu Yule ni Paul Makonda. Picha ile haioneshi sura ya mtu huyo. Lakini moja kwa moja vijana wenye mapenzi na chadema wakaiamini na kuanza kutoa maneno ya kashfa dhidi ya makonda na ridhiwani bila kutaka uthibitisho kuwa Yule ni makonda au laa. Wao hili haliwahusu as long as anayetuhumiwa ni mtu wasiyempenda.
Kabla sijaondoka kwa makonda, ni mara ngapi tumeona makonda akifanya jambo zuri la kupongezwa lakini reaction ya wenye mapenzi na chadema ni matusi na kuwa anapenda sifa na kuwa anajiandalia mazingira ya kugombea ubunge uchaguzi ujao. Kwa hiyo kwa mtazamo wao hakupaswa kufanya aliyoyafanya.
Ndo unakuta kijana akihoji kwa kejeli elimu ya nape nnauye. Na kuandika reply au thread ndeeeefu kumponda kwa elimu yake. Lakini ukihoji kuhusu elimu ya kubenea kijana huyu huyu anakuja kukutuhumu unamuonea wivu na kuwa elimu sio jambo la msingi katika uongozi, na kuwa wenye elimu ndio mafisadi wakubwa kwa hiyo bora yeye asiye na elimu.
Na ndio haohao waliokuwa wakimtukana na kumkejeli Edward lowassa kuwa fisadi kwa sababu tuhuma zinatolewa na chama wanachokipenda, tuhuma zilipohamia chama wasichokipenda ikawa jibu ni kama fisadi mbona hamumpeleki mahakamani. Na kutumia hoja ya ufisadi mpaka mahakamani kwa nguvu huku at the same time wakiwatuhumu kina Andrew change, Tibaijuka,etc kuwa ni mafisadi bila ya kwenda mahakamani. Pia wakimlaumu Magufuli kumrudisha Prof Muhongo kwa sababu ni fisadi/kasababisha ufisadi bila kujali wao wamempa nafasi ya kugombea uraisi mtu mwenye tuhuma hizohizo.
Kwa upande wa pili sasa, baada ya magufuli kuingia madarakani (kihalali au kwa dhulma) akafanya aliyoyafanya na kusifiwa na dunia nzima. Watu wakajenga mapenzi. Sasa hivi utakapohoji jambo lolote kuhusu magufuli utaambiwa unatafuta tu makosa na kuwa unasubiri akosee tu upate la kusema. Hivyo basi hatakiwi kuhojiwa kwa lolote aliamualo na alitendalo. Wale wenye mapenzi naye watamtetea na kumlinda hata kama hawana hoja za msingi. Ukipitia thread nyingi humu JF utaliona hilo.
The same goes kwa mawaziri wake, pia hawatakiwi kuhojiwa. Ukihoji wewe una husda na wivu na unasubiri wakosee t undo ukosoe na humuungi mkono raisi kipenzi magufuli.
Huu ndio unafiki wa watanzania. Kibaya zaidi hawa wenye unafiki huu ndio wanaojiita Great Thinkers. Tusichojua ni kuwa hao viongozi wa serikalini ndio haohao akina sisi. Unafiki huu ndio wanaoingia nao huko serikalini na kutanguliza mapenzi ya chama kabla ya hoja za msingi na maslahi ya taifa. Hawa wanaojiita Great Thinkers ndio ambao unaweza ukaja na hoja za msingi za kuwakosoa naye akaja na jibu fupi tu kuwa wewe ni ACT hivyo humwelezi lolote, Au peleka pumba zako Lumumba, au Ukawa mmeishiwa hoja kaeni kimya tinga tinga litumbue majipu. Ukija na hoja za msingi kukosoa jambo kuhusu magufuli, Great Thinker atakuja na jibu jepesi tu kuwa wewe pia ni jipu so subiri utumbuliwe.
Huu ni unafiki na tusipobadilika hakuna mabadiliko yoyote yatakayopatikana kwa viongozi tunaowachagua.
Huu ndio unafiki wa watanzania, Great Thinkers