Unafiki wa watanzania kutoifahamu "tanganyika"

Unafiki wa watanzania kutoifahamu "tanganyika"

MADINI CHUMA

Member
Joined
Dec 25, 2013
Posts
29
Reaction score
9
Wadau, nasikitika sana ninapomskia mtu tena msomi na kiongozi wa nchi hii anaposema haitambui TANGANYIKA. Mfano ni Mh. Nchemba katika mikutano yako mara nyingi husema haitambui TANGANYIKA pia jana nimemsikia kiongozi mmoja wa CCM akisema haitambui, sasa nina maswali machache naomba mnisaidie (1): Kama kweli TANGANYIKA haitambuliki tarehe 9 December huwatunaadhimisha nini? (2): Kama TANGANYIKA haitambuliki TANZANIA ilitokana wapi? (3): Kama TANGANYIKA haitambuliki mwenge wa uhuru ulitoka wapi? (4): Kama TANGANYIKA haitambuliki NYERERE alikuwa rais wa kwanza wa wapi? (5): Kama kweli TANGANYIKA haitambuliki chama cha wanasheria wa Tanganyika kilisajiriwa wapi? (6): Kama kweli TANGANYIKA haitambuliki ZANZIBAR wanalalamika wamemezwa na nani? (7) Kama kweli TANGANYIKA haitambuliki Mwl. Nyerere na Karume waliunganisha ZANZIBAR na nchi gani kuipata TANZANIA? (8): Kama kweli TANGANYIKA haipo TANU kilikuwa chama cha nchi gani? Mengine mtanisaidia nyinyi wanajamvi maana hawa watu wananichanganya sana. NAWASILISHA.
 
Back
Top Bottom