Unafiki wa Waraabu (UAE) dhidi ya Qatar

Unafiki wa Waraabu (UAE) dhidi ya Qatar

elmagnifico

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Posts
8,260
Reaction score
9,764
Mpango wa kushambulia mfumo wa kifedha wa Qatar ulioandaliwa na wanachama Umoja wa falme za kiarabu (Emirates) umebainika katika folda ya akaunti ya barua pepe ya balozi wa UAE Marekani, Bwana Yousef al-Otaiba.

Tovuti ya uchunguzi ya Marekani ijulikanayo kama The Intercept, ilipata folda hilo lenye mpango huo na kuamua kuweka wazi njama hizo, ambazo zinahusisha shambulio la mfumo wa kifedha wa Qatar.

UAE pia inalenga kuongeza deni la Qatar Kulingana na ripoti hiyo.

Kwa mujibu wa tovuti hiyo ya The Intercept, Benki ya Havilland iliyoko Luxemburg-inayomilikiwa na familia ya mtalaamu wa masuala ya kifedha ajulikanaye kama David Rowland, ndiyo ilihusika katika kuandaa mpango huo wa UAE.

Lengo la mpango huo ni kuhakikisha kwamba uchumi wa Qatar unaanguka, kupunguza thamani za hati funaate na kuongeza gharama zake za mikopo, hatimaye kushusha thamani ya sarafu ya Qatar hali itakayosababisha Qatar kutumia fedha nyingi za kigeni zilizoko kwenye hifadhi yake.

Kampeni ya PR

Mpango huu unaonyesha kuwa wakati uchumi wa Qatar utakapoanza kudhoofika, UAE pia itaanzisha kampeni ya PR ili kufanya shirikisho la soka FIFA kuwa na mashaka na uwezo wa Qatar kuhusu kuandaa kombe la dunia 2020, hivyo Qatar inyanganywe jukumun hilo.

Lengo la mpango huu ni kuzidi kuchochea mgogoro ambao tayari ushaakuwa mkubwa baina ya Qatar na nchi shiriki za UAE.

source Aljazeera News

Hawa Saudia ambaye ndiye kiongozi wa hili Saga wanawaonea kijicho Qatar hakuna lolote
 
Waarabu wanatumika vibaya na mataifa ya magharibi. Saudi Arabia kajilimbikizia silaha toka kwa mataifa ya magharibi kwa gharama ya mabilioni na sasa anatumika kukinzana na kuidhoofisha Iran. Hao U.A.E nao wanatumika kuidhoofisha Qatar na hasa baada ya Al-Jazeera kugeuka kuwa mwiba mchungu kwa kuharibu propaganda za vyombo vya magharibi.
 
Nahisi hata marekani hana sera maalumu juu ya hili kama ulisikia kauli ya Rex Tillerson aliituhumu UAE kwa wanachomfanyia Qatar wakati Trump akapongana naye kwa kuwa upande wa Saudia
 
Waarabu wanatumika vibaya na mataifa ya magharibi. Saudi Arabia kajilimbikizia silaha toka kwa mataifa ya magharibi kwa gharama ya mabilioni na sasa anatumika kukinzana na kuidhoofisha Iran. Hao U.A.E nao wanatumika kuidhoofisha Qatar na hasa baada ya Al-Jazeera kugeuka kuwa mwiba mchungu kwa kuharibu propaganda za vyombo vya magharibi.
Wacha watumike tuu hawana akili
 
Saudis na Egyptians wana Hofu sana na Qatar kuwa Taifa kubwa katikati yao
Utawala wa Qatar kiasili chimbuko lake ni Saudia hivyo wanajuana sana
 
Na kampeni ya kuondoa uandaaji wa kombe la dunia Qatar wamekwisha ianzisha twitter
 
Saudis na Egyptians wana Hofu sana na Qatar kuwa Taifa kubwa katikati yao
Utawala wa Qatar kiasili chimbuko lake ni Saudia hivyo wanajuana sana
Saudia anataka awe the main master that controls middle East
 
Kwa kukubali kwake kuwa Kimada wa kudumu wa Marekani hawezi kupata hadhi hiyo
Ataangukia pua muda si mrefu na hii power struggle within ukajumulisha na vita ya Yemen bado chokochoko Iran, bei ya mafuta haiko stable
 
Wasaudi wanazidi kujichimbia kaburi na tatizo ni la crowned Prince anaenda kuharibu mfumo mzima
 
Hivi kweli sie waafrika tunaweza kuwasema waarabu kwamba wanatumika na Wazungu na ni wajinga?
 
T
Wasaudi wanazidi kujichimbia kaburi na tatizo ni la crowned Prince anaenda kuharibu mfumo mzima

Tena Huyu Mfalme Salmaan wa sasa ndo akili yake Kama Tunda ya Ubuyu
Kuvuruga Mfumo wa Miaka yote ya Ufalme

Kwa kawaida Ukiwa Mfalme Saudia Jukumu lako ni kuteua Mrithi atakaemrithi Mrithi wako sio Wewe kuteua Mrithi wako sasa Yeye kaingia kamfuta Mrithi wake ambae aliteuliwa na King Abdullah akamteua Mtoto wake pia kateua Mrithi wa atakaemrithi Mwanae na kwa sasa ndani ya Makasri ya Mfalme moto unawaka chini kwa chini Hakuna Tena maelewano
 
Kuchanganya Dini na Unafiki hakutawaacha salama..,
 
Back
Top Bottom