Unafiki wa Wabunge Huu hapa

Unafiki wa Wabunge Huu hapa

mgeni wenu

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2012
Posts
3,664
Reaction score
1,731
Wana JF kama mnakumbuka baada ya uchaguzi wa Igunga kuna kada wa CHADEMA aliuwawa na mwili wake kuokotwa baadaye ukiwa umeoza na hata kutotambulika kwa Urahisi,Baadaye Uchaguzi wa Arumeru Aliuwawa Msafiri Mbwambo(Mwenyekiti wa Chadema USA RIVER)kwa kukatwa Shingo kwa msumeno wa engine ya Mnyororo(chain Saw)tena wauaji wakisaidiwa na viongozi wa CCM ambao walikamatwa na kutoroka mikononi mwa Polisi(kwa Msaada wa Viongozi wa CCM na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani)

Sikuona Bunge kusimama na kuunda tume,pia walikufa Waandamanaji(Chadema)kwa kuuwawa na Polisi Arusha Bunge lilikuwa kimya na hakuna aliyeinuka kusema,pia waliuwawa watu Kwa Bomu Olasiti(Arusha)kwa mipango michafu ya wana CCM hakuna aliyesema,Wabunge wa Chadema wakiwa wakipigwa na Kunyanyaswa na Polisi,hakuna aliyetakiwa kuwajibika,.

Kwenye Mkutano wa Chadema Soweto(arusha)walikufa Wana Chadema na watoto wadogo kwa kupigwa Risasi na polisi hiyo hawakuona Ila Majangiri ambao wana Mahusiano na wabunge wa CCM walipoguswa na mifugo ya Wakubwa kuguswa imebidi Baraza livunjwe na Wapo wanaotaka Pinda pia atimuliwe,

HUU NI UNAFIKI WA BUNGE...
 
uzi huu umefanana na maelezo ya jamaa mmoja aliyekuwa kwenye kipindi cha marumbano ya hoja itv wiki hii sijui ndio yeye!! Anyway unalolisema ni sawa kwani mtandao wa majangili ndio uliosababisha mawaziri wajiuzuru.
 
Mkubwa damu hulipwa kwa damu na machozi hulipwa kwa machozi....
Tungoje si mbali yataeleweka tu
 
Mawazo ya kweli mara nyingi hufanana,siyo mimi mkuu ni mawazo tu
uzi huu umefanana na maelezo ya jamaa mmoja aliyekuwa kwenye kipindi cha marumbano ya hoja itv wiki hii sijui ndio yeye!! Anyway unalolisema ni sawa kwani mtandao wa majangili ndio uliosababisha mawaziri wajiuzuru.
 
Wana JF kama mnakumbuka baada ya uchaguzi wa Igunga kuna kada wa CHADEMA aliuwawa na mwili wake kuokotwa baadaye ukiwa umeoza na hata kutotambulika kwa Urahisi,Baadaye Uchaguzi wa Arumeru Aliuwawa Msafiri Mbwambo(Mwenyekiti wa Chadema USA RIVER)kwa kukatwa Shingo kwa msumeno wa engine ya Mnyororo(chain Saw)tena wauaji wakisaidiwa na viongozi wa CCM ambao walikamatwa na kutoroka mikononi mwa Polisi(kwa Msaada wa Viongozi wa CCM na aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani)

Sikuona Bunge kusimama na kuunda tume,pia walikufa Waandamanaji(Chadema)kwa kuuwawa na Polisi Arusha Bunge lilikuwa kimya na hakuna aliyeinuka kusema,pia waliuwawa watu Kwa Bomu Olasiti(Arusha)kwa mipango michafu ya wana CCM hakuna aliyesema,Wabunge wa Chadema wakiwa wakipigwa na Kunyanyaswa na Polisi,hakuna aliyetakiwa kuwajibika,.

Kwenye Mkutano wa Chadema Soweto(arusha)walikufa Wana Chadema na watoto wadogo kwa kupigwa Risasi na polisi hiyo hawakuona Ila Majangiri ambao wana Mahusiano na wabunge wa CCM walipoguswa na mifugo ya Wakubwa kuguswa imebidi Baraza livunjwe na Wapo wanaotaka Pinda pia atimuliwe,

HUU NI UNAFIKI WA BUNGE...

Nadhani siyo tatizo lako bali na tatizo la ufahamu wako au madarasa uliyohitimu, Una uhakika gani kwamba pale Olasiti waliokufa ni wanachadema? Tujuze kwa vielezo mfano Namba za Kadi zao za uanachama na zilitolewa wapi na tarehe ngapi, pia tuthibitishie ka ni kweli kuwa kila kwenye mkutano wa CDM wote wanaokwenda pale mi wanachadema! Acha unafiki.
 
Basi kama walokufa ni wana CCM we taja kadi zao na number(arusha CCM kabaki Magesa Mulongo na wewe

Sna hakika kama ni kweli wewe ulikwenda shule na shule ikakustaarabisha, Thibitisha kwa vielelezo ni kadi namba ngapi zilizopatikana kuthibitisha kuwa waliouawa pale Olasiti na kwingineko ni Wanachadema? au ni hisia zako zinazotokana na mazoea ya wanasiasa uchwara wa kutaka kujitafutia umaarufu hata kwa damu ya wtu? , mfano auwawe Mwangosi CDMmgeuze sera au mada, mawaziri wajiudhuru mgeuze mada, Pinda atoe kauli ya wakorofi kupigwa tayari ni mada, Mbona ya Mwigamba hamuigeuzi mada? ,Mbona ya aliyekwenda Dibai na hawala yake kustarehe kwa gharama za fedha ya walala hoi hamuijadiri kama mada? Acha ukuda.
 
Huyo nae eti anatetea ccm... ni miongoni mwa raia mizigo anywhere... cdm yaweza kukutua hyo mizgo yako... pumbav
 
Kiukweli wabunge hasa wa CCM ni wanafiki sana,matukio yote yaliyofanywa na majangiri ndiyo yameundiwa tume kuchunguza wamepata hasara kiasi gani.Baada ya kugunduwa kwamba yaliguswa maslahi ya mkuu ndiyo maana mawaziri wakalazika kupigwa chini.Lakini kama hii biashara ya ujangiri ingekuwa ya walalahoi,nakwambiya mpaka wafanyakazi wanaohudumia ofisi wangepandishwa vyeo.
 
Nadhani siyo tatizo lako bali na tatizo la ufahamu wako au madarasa uliyohitimu, Una uhakika gani kwamba pale Olasiti waliokufa ni wanachadema? Tujuze kwa vielezo mfano Namba za Kadi zao za uanachama na zilitolewa wapi na tarehe ngapi, pia tuthibitishie ka ni kweli kuwa kila kwenye mkutano wa CDM wote wanaokwenda pale mi wanachadema! Acha unafiki.

...mwenzio katoa facts iwe ni CDM au CCM its not a point...kama wewe unazo facts kuhus aina ingine za watu na ID zao ziweke ukipenda......the fact of the matter au jambo la msingi kuelewa hapa ni kuwa watu walikufa kwenye matukio yale......na waliohusika hatujasikia wameshitakiwa.....ili haki ipatikane.....
 
Nadhani siyo tatizo lako bali na tatizo la ufahamu wako au madarasa uliyohitimu, Una uhakika gani kwamba pale Olasiti waliokufa ni wanachadema? Tujuze kwa vielezo mfano Namba za Kadi zao za uanachama na zilitolewa wapi na tarehe ngapi, pia tuthibitishie ka ni kweli kuwa kila kwenye mkutano wa CDM wote wanaokwenda pale mi wanachadema! Acha unafiki.

Ngoja nikujengee hoja we mbwira ili ukawafundishe na wenzako.. na hii ni falsafa ndogo tu..

kuna tofauti kati ya mwanachadema na mwanachama wa chadema, pia mwanaccm na mwanachama wa ccm.. mwananchi na mzalendo..

mwanachadema inajumuisha mwanachama wa chadema mwenye kadi na mkereketwa wa chadema asiye na kadi, mradi anaiunga mkono chadema.. the same to ccm..
Mwananchi ni mkazi yeyote wa nchi husika, hata kama amekuja visitation kwa miezi sita, wakati mzalendo ni mkazi wa kudumu wa nchi husika..

Sasa rudia kusoma thread ndio ulete maswali yako from ur holed-brain!!
 
Samahani kama nitakuwa nimekosea kwenye tafsiri ya mwananchi na mzalendo. Mwananchi ni raia wa nchi, aijalishi kama ana uraia wa kuzaliwa au kuandikishwa. Mzalendo ni raia mzawa mwenye asili ya nchi husika. maneno kama haya yanapoulizwa, yanakuwa yamebeba ujumbe mzito "uko wapi uzalendo wako"?
 
Hapo mbona sioni tatizo kwake yeye kusema waliuwawa wanachadema...? Tujikite kwenye hoja ambayo ni mauaji ya wananchi kwenye mkutano wa chadema....na siyo tuanze kujadili makosa madogo madogo amabayo kila mtu anaweza kuyafanya...!!
 
Basi kama walokufa ni wana CCM we taja kadi zao na number(arusha CCM kabaki Magesa Mulongo na wewe

Mkuu mgeni wenu una hoja nzuri kwenye bandiko lako na ni hoja fikirishi sana ila sasa unapokosea ni kuhusisha mauji ama visa hivyo na vyama. Nadhani tungesema tu kwamba Watanzania waliuawa ama waliathirika kama ambavyo imekuwa kwenye hili sakata ka Tokomeza. Katika sakata la Tokomeza rejea imekuwa ni kwa Watanzania na wala si CHADEMA ama CCM.

Hoja yako ni fikirishi hasa linapokuja suala la kuguswa kwa majangili. Mimi naamini kwamba ukishirikisha jeshi katika operation yoyote lazima kuwe na shida kwa kuwa kama kawaida Jeshi la Ulinzi huwa halina mhalifu bali lenyewe linajua adui. Japo walifanya mengine ambayo si ya kibinadamu lakini majangili inabidi yasakwe yatokomezwe. Kwa sasa nadhani yanachekelea na kuendelea kuua tembo na kujipatia nyara zingine kemu kemu yakiwemo meno ya viboko na ngiri.

Last edited by a moderator:
Huyu mleta uzi ajitahid kutengeneza heading inayoendana na content, angeandika'unafik wa wabunge wa ccm'
hata hvyo huyu mwenyewe n mnafiki mkubwa sana,anaacha kusema ukweli hvi hajui kwamba hakuna viongozi kama wa CHADEMA. Ukweli ni kwamba matukio mengi ya kutisha yameratibiwa na viongoz wa makao makuu CDM.
 
Nimekusoma

Back
Top Bottom