Huku wananchi wa kawaida wanaoishi maeneo ya Moshono hadi kilipo chuo kikuu cha Nelson Mandela mkoani Arusha, wakitaabika kwa vumbi jingi na barabara mbovu, imekuwa ni kawaida kwa Uongozi wa Mkoa na TANROAD mkoani hapa kufanya marekebisho ya barabara hiyo pale tuu wanaposikia kuna ugeni wa mmoja wa viongozi wakubwa anaetegemewa kutumia barabara hiyo. Kwa Mara ya mwisho barabara hii ilipitishwa grader na kumwagwa vifusi mwaka Jana 2012, Rais alipokwenda kufungua rasmi Chuo cha Nelson Mandela.
Baada ya muda mfupi barabara hiyo imekuwa na mashimo mengi na vumbi jingi sanaaa na kuwa kero kubwa kwa wananchi wanaoishi pembezoni na hata wafanyakazi wa Chuo hiki kipya, hilo halikuonekana kama tatizo kwa viongozi wa Mkoa wa Arusha.
Baada ya Kusikikia Waziri Mkuu Pinda, atafanya ziara katika chuo hicho kesho tar 31/01/13, kuanzia jana na leo barabara hyo imeanza kusawazishwa na hata kunyunyuziwa maji kuondo vumbi.
Watu wanajiuliza, JEE UONGOZI WA MKOA UPO KWA AJILI YA KUWAFURAHISHA JK NA PINDA AU KUWATUMIKIA WANANCHI WA MKOA HUU??? KAMA TATIZO NI PESA, HIZI ZA KUREKEBISHA KIPINDI CHA UGENI WAO KINATOKA WAPI? NI FUNGU LA RAIS NA WAZIRI MKUU AU? KWA NINI HALI ISIACHWE KAMA ILIVYO ILI NAO WAJIONEE MATATIZO YA WANANCHI???