Unafiki wa Serikali

Tanzania 1

Senior Member
Oct 4, 2007
197
25
Serikali wanayadai haya hapa chini huku tovuti zao ziko ovyo kabisa; ni sawa na hakuna!!

Serikali yataka wananchi kuchangamkia teknolojia ya habari na mawasiliano

2008-05-14 16:01:40
Na Joseph Mwendapole, Jijini


Serikali imesema mikakati ya makusudi inahitajika kuwaandaa wananchi wanaoishi mijini na vijijini kutumia fursa za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, TEKNOHAMA.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ulinzi, Dk. Hussein Mwinyi, wakati akizindua wiki ya maonyesho yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini, TCRA.

Dk. Mwinyi amesema TEKNOHAMA imekuwa nyenzo muhimu inayotumika kwa kiwango kikubwa katika mifumo ya uchumi wa dunia.

Amesema katika karne hii ya 21 inayotambulika kama karne ya Sayansi na Teknolojia, nchi zilizoendelea zimeimarisha mifumo ya TEKNOHAMA na wanategemea sana mtandao wa intaneti.

Ameongeza kuwa kutokana na hali hiyo Tanzania haiwezi kubaki nyuma na kuwa kama kisiwa, badala yake inapaswa kuimarisha matumizi hayo katika shughuli za maendeleo.

``Ili kutumia kikamilifu fursa za TEKNOHAMA katika maendeleo ni lazima tuweke mikakati ya makusudi ya kuwaandaa wananchi wetu wanaoishi mijini na vijijini kwa kila mwananchi awe tajiri au maskini, mlemavu au asiye na ulemavu waandaliwe kuitumia``, akasema.

Akaongeza kuwa wakuu wa nchi zote duniani katika kikao chao cha jamii habari kupitia mpango kazi wa Geneva walizitaka nchi wanachama kutafuta ufumbuzi juu ya mahitaji maalum ya walemavu.

Akasema wakuu hao walitakiwa kuweka mikakati ya kitaifa na kuhimiza utengenezaji wa vifaa vya TEKNOHAMA na huduma Muafaka kwa mahitaji ya walemavu.

Akasema sambamba na hilo wito ulitolewa kwa tafiti za maendeleo kuwezesha upatikanaji wa TEKNOHAMA kwa wote ikiwemo watu wenye ulemavu.

SOURCE: Alasiri
 
Back
Top Bottom