Watanzania ni watu wenye kasumba ya ajabu sana. Wengi wao ni watu wanaopenda kutendewa kitu wasichopenda kumtendea mwingine! Nitatoa mifano miwili nikijaribu kubainisha unafiki wa watanzania walio wengi!
Aicha Radhia alipoteuliwa kuwa Miss Tanzania, swala hili lilieta mushkeli mkubwa sana na manung'uniko nchini, kisa tu Aicha alikuwa ni mtanzania mwenye asili ya India. Watanzania walihakikishwa wanambagua Aicha na kutompa ushirikiano wa kutosha katika kipindi chake cha umalikia wa taji la miss Tanzania... Hata wakati anashinda kuna watu walimwaga machozi uwanjani wasikubaliane na the fact kuwa 'mhindi' amekuwa miss Tanzania.
Watanzania hao hao waliombagua Aicha Radhia, ndio wanaolia kuwa wanabaguliwa kwenye mataifa ya watu kam Marekani, Ulaya na India, huku wao pia wakiwa wanafanya hayo hayo.
Huu ni unafiki wa hali ya juu sana!