Qunax
Senior Member
- Oct 16, 2016
- 100
- 127
Watu maarufu, viongozi wa dini wanaohusianisha madai ya raia juu ya shutuma za mkuu wa mkoa wa dar es salaam kuhusu vyeti vya taaluma na ukwamishaji katika kampen yake ya kupambana na madawa ya kulevya ni wanafiki, wanafiki kwa sababu gani ikumbukwe kuna watanzania zaidi ya 15,000 ambao serikali ilitangaza walifoji vyeti na wamefukuzwa makazini na kama damu yao tayari imeshamwagika wale inaonekana kama sio watu ni simbilisi, leo hii raia wanacomplain juu ya huyu mtu mmoja baadhi ya watu wenye heshima kubwa katika taifa hili wanadiriki kusema raia wanamkwamisha mheshimiwa kwenye mapambano ya madawa huo ni unafiki wa hali ya juu yaan inaonekana dhahiri wanajitahidi kufunika kombe mwanaharamu apite, mbona hali halisi inajieleza hakuna asietaka mapambano ya madawa ya kulevya ukiacha walengwa, na kelele zinazopigwa na raia sio za kukwamisha kampeni hyo bali ni kuhusu vyeti vya taaluma vya muheshimiwa kama kuna ambao walipigwa chini kwa sababu ya vyeti yeye asipigwe chini kama nani maana nchi ni ya Watanzania wote na hakuna aliye juu ya sheria.kama sheria ni msumeno acha ikate kote kote.....alishutumiwa mheshimiwa mwigulu baada tu ya siku mbili akaweka sawa na watanzania wakaelewa, watanzania ni watu wenye utashi sio mawe tungewekwa wazi kuhusu hivyo vyeti vyake tungeelewa tu na mapambano yangeendelea tatizo liko wapi?
Wale wasanii na viongozi wa dini mnaondelea kuwashutumu watanzania wanaohoji kuhusu vyeti eti ndio wanaokwamishwa jitihada za mheshimiwa mnakosea sana......Mbona kuna Mawaziri kama vile Mwinyi tangu aingie madarakani miaka yote hii sijawahi kusikia mtanzania yeyote akitia neno lolote juu yake na anaifanya kazi yake vizuri kabisa kama ingekuwa ni chuki kama inavyoenezwa sumu basi angeandamwa na yeye.....Mimi naomba msiwaquorte vibaya Watanzania mkumbuke mnaongoza kundi kubwa la vijana wa karne ya 21 so msifanye mambo kama yale yaliyofanywa na viongozi wa miaka ya 60.