Unafiki kwenye Siasa Unalipa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Unafiki unalipa, Hamad Rashid kawa Waziri Zanzibar, jamaaa yangu Humphrey Polepole anazidi kusaga lami tu mara ITV mara Chanel 10 mara Startv,

Lakini Luten Kanali Likvol Shekvov mkufunzi wa tabia na hisia za kibinadamu katika chuo cha majasusi cha Russian Federal Security Service anabainisha kuwa hulka za kibinadamu huathiriwa na unafiki, lakini unafiki usio na bughudha "unaolipa zaidi" ni ule ufanywao na wazee.

Kwa kijana utakabiliwa na changamoto kubwa katika safari yako ya maisha.

Na: Yericko Nyerere
 
Na Yericko Nyerere

Hivi na wale 46 wa mitandaoni vipi? Au sababu ni vijana?
 
Amefanya na anafanya kazi sana kijana Wa watu, naamini Magu anamuona na anajua kaz zake, pia mwenyekiti Wa chama anajua jinsi jamaa anavyokitetea chama, naamin hawatamwangusha
 
Unafiki ni dhambi kubwa sana kwa Mungu.

Naamini pia adhabu ya unafiki wa Hamad Rashid wa kujifanya kipofu na kuuita uchaguzi wa marejeo wa jecha na CCM yake kuwa ulikuwa uchaguzi huru na haki, hakika adhabu ya unafiki huo uliopitiliza, hautasubiri hukumu ya akhera, bali adhabu yake ataanza kuionja hapa hapa duniani.
 
Yaa unalipa lakini mwisho wake hauwi vizuri. Nitakupa mfano kidogo, Maalim alimfanyia yule mzee unafiki na kusababisha mzee kuvuliwa nyadhifa zote akidhani atateukiwa kuwa Rais, mwisho hakuwa Rais. Chadema waliwahi kusema hawawezi kushirikiana na cuf kwa kuwa cuf ni CCM B baada ya mwafaka, baadaye wakaazima mgombea mweza wapate urais, mwisho hawakupata. Chadema waliwahi kuzunguka nchi nzima wakidai Mh.Lowassa ni fisadi na Mbowe akasema jamaa ni dhaifu sana, mwisho wakafanya unafiki wa kumsafisha nchi nzima kuwa ni safi na kumwazima agombee urais akifikiri watapata, mwisho walikosa Rais. Mifano iko mingi, Nakubaliana unafiki unalipa kwa kitambo tu, mwisho unakuwa sio.
 
Huyo kijana Polepole naye ni mnafiki wa kupitiliza, kwa namna anavyojitahidi kuitetetea CCM kwa nguvu zake zote hata pale anapojua fika kuwa CCM wamefanya uovu wa dhahiri, naye adhabu yake haitamsubiri mbinguni kwa Mungu. Bali naye ataanza kuonja adhabu yake hapahapa duniani.

Inashangaza pia kwa vyombo vya habari vingi vya luninga kumpatia airtime ya kupitiliza kada huyo kijana wa CCM, ambaye ni mnafiki wa kupitiliza, ili akitetetee kwa nguvu zake zote chama chake cha CCM.

Ila huyo Polepole kiboko yake ni Mchungaji Msigwa, kwa kuwa hivi majuzi kwenye kipindi cha mada moto cha channel 10, aliweka mpira kwapani na hakutokea kwenye kipindi hicho kwa kuhofia 'makombora' ya Mchungaji Msigwa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom