Nape: Usalama wa Taifa hausaidii nchi, wamekalia kusikiliza simu za watu

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,779
18,746
Video



Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye ameibuka na kuituhumu Idara ya Usalama wa Taifa nchini haifanyi kazi zake ipasavyo inavyohitajika na badala yake wamekalia kusikiliza simu za watu wanavyoongea pamoja na kufanya mambo ambayo hayalindi uchumi wa Tanzania.

Nape ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa akichangia bungeni taarifa ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama katika mkutano wa 10 kikao cha nane cha Bunge mjini Dodoma na kuishauri kamati hiyo ipeleke mapendekezo ili waweze kupitia upya sheria ya Usalama wa Taifa na kuiwezesha mikono yao iende mbali na wakumbuke jukumu lao la kuhakikisha wanalinda uchumi nchi katika kipindi hiki, ambacho demokrasia ya siasa inahama na kuelekea kwenye demokrasia ya uchumi ambapo muda mwingi wanapaswa kuutumia huko na sio pengine.

Kutoka na hayo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Kapteni George Mkuchika amemjibu Nape na wabunge wengine kwamba kazi ya Idara ya Usalama wa Taifa sio kutafuta watu waliopotea au kuumizwa kama wanavyodai na laiti wangelifahamu wanachokifanya wangekaa kimya.

"Kazi ya usalama wa Taifa nchi yeyote ni kutafuta habari na kuishauri serikali. Kwa kifupi tu mimi nasema hoja mlizozitoa kuhusu idara kwamba haishauri serikali mambo ya uchumi na mambo mengine hamna ushahidi", amesema Kapteni Mkuchika.

Aidha, Kapteni Mkuchika amesema katika nchi zote duniani Idara ya Usalama wa Taifa wanapaswa waishauri serikali yake kimya kimya na sio kila mtu afahamu kwamba wamefanya jambo gani.

"Huwezi kusikia nchi yoyote kuwa kuna msemaji wa Idara ya Usalama wa Taifa kwamba kasema hivi wala vile hakuna kitu kama hicho. Kwa hiyo unaposema serikali hawakuishauri unao ushahidi juu ya hilo?", amehoji Kapteni Mkuchika.

Pamoja na hayo, Kapteni Mkuchika ameendelea kwa kusema "Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1996, kazi zilizopitishwa kwa mujibu wa Bunge kuna shughuli nne za idara kwamba ni kukusanya na kutafuta habari pamoja na kuzifanyia tathmini na wanapoyafanya hayo hawayafanyi katika mkutano wa hadhara, kushirikiana na vyombo vya idara nyingine vinashughulika na usalama wa nchi, kuwashauri Mawaziri ili waishauri serikali na mambo yote ya kuhujumu uchumi na mengine wanayafanya kimya kimya".

Kwa upande mwingine, shughuli za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Taifa zimehairishwa jana jioni (Ijumaa) mpaka Aprili 03 mwaka 2018.

Chanzo: EATV

-------------
Yericko Nyerere anasema,

CHANGAMOTO NA MAPOKEO YA TISS:

Leo nataka nishereheshe hoja ya Mh Nape Nnauye Bungeni ikiungwa mkono na wabunge Mh Msigwa na Mh Zitto Kabwe ya kupendekeza mabadiliko ya mfumo wa usalama wa Taifa nchini Tanzania. Hoja hii ni muhimu sana sana kiliko inavyofikiriwa, na nihimize wabunge waitilie mkazo bila kuathiriwa na itikadi za kisiasa. Nimesikiliza hata majibu ya hoja ya Mh Waziri Mkuchika akitetea kwamba TISS haihitaji marekebisho kwakuwa inafanya kazi kwa ufanisi.

Nijaribu kumkumbusha Waziri Mkuchika, mabadiliko ya idara au mashirika ya kiusalama duniani sio jambo geni ama jambo la siri, Tarehe 20 January 1996 Mzee Mkapa alitia saini sheria iliyounda upya chombo hiki cha ujasusi kutoka kuitwa Tawi Maalumu ndani ya Jeshi la Polisi, (SB) na kuzaliwa TISS, Mzee Mkapa alitumia Buge hilihili la Jamhuri kufanya mabadiliko haikuwa siri, hakuna mbunge asiyejua kazi na majukumu ya TISS kwakuwa yapo kisheria kwa sheria iliyotungwa na Bunge, Kifungu cha sheria ya Usalama wa Taifa (Duties and Power of TISS) kifungu cha 14-(1),(2),(3) (a) na (b), kinafafanua wazi kazi za MSINGI za TISS. Lakini haiishii hapo tu, kifungu cha 15-(1),(2),(3) (a),(b),(c) na kifungu (4).

Sasa leo Mkuchika akiwapinga wabunge kwa hoja kuwa hawajui kazi za kisheria za TISS inashangaza na huku ndio kuingiza siasa kwenye chombo hiki, kwa Mataifa yaliyoendelea Waziri alitakiwa kutulia na kujibu kwa hoja mujarabu za kimantiki au kupokea hoja za wabunge na kuzipeleka katika vyombo vya michakato kuliko kujibu tu tena kienyeji tu kwa hoja nyeti kama hii.Katika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi nimeleza kwa kirefu kwanini mabadiliko ya TISS ni muhimu, fuatana nami hapa chini toka kitabuni:

Idara ya TISS ambayo ndio uhai wa taifa la Tanzania imefanya mengi ya kutukuka na yasiyomithirika hata kwa chembe ya haradali. Wadadisi wa masuala ya kijasusi watakubali kuwa TISS ndicho chombo pekee nchini Tanzania kilichofanya kazi yake kwaufanisi mkubwa na kulifikisha taifa lilipo sasa, Pamoja na kusimama imara kwa taasisi hii, yapo mambo ya msingi yanayotakiwa kuwekwa sawa ili taasisi hii iendane na mageuzi ya dunia ya leo ya Sayansi na Teknolojia na uchumi wa kijasusi, mahuisho katika chombo hiki muhimu ni lazima yaguse nyanja zote muhimu kuanzia uhusiano,watendaji,teknolojia na sheria. Mathalani Sheria ya Usalama wa Taifa ya mwaka 1996 iliyounda upya chombo hiki ina upungufu kwa sasa kulingana na mageuzi dunia ya kifikra na kiteknolojia, Sheria hii inaififisha taasisi hii huku ikiruhusu siasa kujipenyeza ndani ya chombo hiki adhimu na muhimu kwa uhai wa taifa letu, sheria inasema, "kazi yake kubwa ni kukusanya na kuchambua taarifa (intelligence gathering and analysis) na kuzipeleka/kushauri wahusika kuchukua hatua."

Kwa maneno hayo, TISS imenyimwa nguvu ya moja kwa moja, kama zilivyo taasisi za wenzetu huko ughaibuni tulikozoea kuakisi kila kitu. Mara nyingi utekelezwaji wa aina kama hii ya sheria hufaa kwenye mataifa ya kijamaa na kiimla, lakini kwenye mataifa ya kidemokrasia na yenye mfumo wa vyama vingi ni hatari sana kuwapo kwa sheria hii. Upitishaji wa sheria hiyo lilikuwa shambulizi moja kubwa dhidi ya mamlaka ya Usalama wa Taifa lililohitimishwa kwa kutekwa Idara hiyo ya Usalama wa Taifa. Wanasiasa na mafisadi walifanikiwa, na tangu hapo kuyumba na kudorora kwa taifa kila nyanja ndipo kulipoingia Tanzania. Hii inatoa fursa kwa viongozi wa kitaifa (wakisiasa) kuingiza wazo lao lolote walipendalo, liwe jema kwa taifa ama jema kwao binafsi. Lakini hatari zaidi inakuja pale watawala wanapoingiza itikati zao za kisiasa katika kutekeleza wa ushauri wanaopewa na chombo hiki, Bunge la Tanzania linayofursa ya kuihuisha sheria hiyo ili taasisi ya Usalama wa Taifa Tanzania iwe huru na iwe na meno, yaani (ibaini na kuzuia yenyewe), Hata hivyo uhuishwaji wa sheria hii ufanywe kwa umakini ili kutofungua mwanya wa idara hii kuwa na nguvu ya kumuondoa kiongozi/rais pia uende sambamba na kuifanya imlazimishe kiongozi anayeshindwa kuchukua hatua kwa ushauri wa taarifa sahihi za usalama au anayechukua hatua zisizotakiwa wakati ana taarifa na ushauri sahihi wa taasisi hii awajibike. Ili hii iwe na maana chombo hiki kinatakiwa kiimarishwe lakini pia kitenganishwe na siasa za vyama.

Kwa taifa ambalo ni imara,Usalama wa Taifa ni taasisi inayotakiwa kufanya kazi kwa weledi kuliko idara yoyote ile.Weledi wake hautakiwi kutiliwa shaka yoyote kwa viwango vya kitaifa,kikanda (regional) au kimataifa kwa maana pana zaidi. TISS inatakiwa kutengeneza mfumo ambao ni rahisi katika kufanya ubadilishanaji wa taarifa za kijasusi (informations sharing) wakati huo huo ikijaribu kuimarisha vitengo vilivyopo ili kutimiza malengo ya idara na taasisi kwa ujumla kama ilivyo mifumo ya mataifa makubwa kama mkakati wa ulinzi na usalama wa Marekani, Uingereza, Pakistan, Israel, Afrika Kusini, China, India na Canada.

Ingawa mikakati mingi ya mataifa yaliyoendelea imekuwa ikibadilika kwenye maslahi yao ya kiuchumi na ushindani wa nguvu na mamlaka kimataifa lakini kwa taifa lililofikisha umri wa miaka 50 ni lazima liwe na mtazamo imara na kwa kuanzia ni lazima ianze na kanda ya Maziwa makuu, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla, hii ni kwakuwa Tanzania tumeingia kuwa taifa lenye utajiri zaidi barani afrika kwa sasa baada ya ugunduzi wa GESI ya kutosha inayokadiriwa kuweza kulihudumia bara la ulaya kwa miaka 100 bila kukoma. Kwa mfano tuna washindani wetu kiuchumi na mpinzani wetu hapa Afrika Mashariki ni Kenya.
Hatujaweza vya kutosha kwenye ujasusi wa kiuchumi (Economic intelligence) kule Kenya ingawa wao wamewekeza hapa kwetu. Leo hii Kenya inasafirisha madini ya TANZANITE, wanasafirisha dhahabu na kadhalika. Uwiano wa kibiashara (Balance of trade) kati ya Tanzania na Kenya ni somo la ujasusi wa kiuchumi kwa nchi ya Tanzania (Economic intelligence). Tunapotunga sera zetu za kiuchumi tunatakiwa tutumie taarifa za kiintelijensia kwa kutumia wataalamu waliobobea na pia tuangalie masuala tata yanayoweza kuibuka na mwenendo wa washindani wetu.Katika maofisa ubalozi wetu walioko Kenya tujiulize ni wangapi wenye uwezo kusimamia maslahi yetu ya kiuchumi wa Tanzania hapa Afrika mashariki kupitia Kenya?

Kuna mgogoro kati ya dola na sarafu ya Tanzania, Je hakuna uwezekano kwamba dola zimekuwa zikinunuliwa kwa wingi na kwenda Kenya ili kuhujumu uchumi na kuvuruga sera za uchumi Tanzania? Usalama wetu bado unahitaji mageuzi kutegemeana na matakwa ya kisheria na kuboresha malengo ya TISS ili iwe ya kisasa zaidi. Malengo ya TISS kulingana na hali ya dunia kwa sasa na mahitaji ya taifa tunakopitia kisiasa,kiuchumi na kiutamaduni yaegemee katika kutabiri (si utabiri wa majini/tunguri) bali ule wa kisayansi, kupenya, na kuwahi matukio ya hatari kwa maslahi na usalama wa taifa letu, na kuwasaidia wale wanaotekeleza sera yetu ya ulinzi na usalama,kulinda taifa na watu wake,utekelezaji wa sheria na kulinda maslahi na sera zetu kitaifa bila kuathiriwa na ushawishi au hatari yoyote kutoka ndani na nje ya taiafa letu na kulinda malengo yetu kama jamii kwenye nyanja za kimataifa(jamii nyingine).

Ili kujenga nguvu ya propaganda ya kijasusi, mageuzi muhimu yawe kwenye uhamilishaji wa habari. Lazima ziwepo habari za kijasusi ambazo zitakuwa hadharani, hasa zile ambazo TISS itaamua umma ujue ikilenga kanda ama Afrika zifahamu kwa manufaa ya Tanzania. Ni zile habari tu ambazo zinatolewa na kudhibitiwa na vitengo vya "disinformation and misinformation". Kwa hiyo hapo ni kwamba TISS hawajafanikiwa kwenye hivyo vitengo kama ambavyo wanashindwa kufanya kwenye ujasusi wa kiuchumi na upandikizi kiuchumi.

Malengo makuu ya Ujasusi Tanzania yanatakiwa kujikita katika Uchumi, hakuna njia ya mkato ya kufikia mafanikio ya Taifa kiuchumi bila kuruhusu uchumi wetu uongozwe na Usalama wa Taifa na Jeshi la Wananchi Tanzani (TISS na MI). Tanzania iwe na shirika la Ujasusi linaloangalia siasa kama njia tu, na sio msingi imara wa kulinda TAIFA, wanausalama watakao kuwa makini kuona kofia ya siasa haizidi kofia ya nguvu ya umma au TAIFA. Ni wakati mwafaka wa kutambua NCHI ndio nguzo ya UTAIFA na sio siasa kuwa ndio UTAIFA wenyewe. Kusimamia Demokrasi kwa jicho la ndani na sio jicho la upendeleo wa kiitikadi bali kuongozwa na kusimamia maadilli ya NCHI dhidi ya siasa. Inatakiwa Shirika ambalo halitatumika kwa faida ya chama, Mtu au kikundi cha watu bali ukweli uwe Taifa lianitaji nini kutoka kwenye siasa. Nchi inaishi katika lindi la unafi hasa vijana.

Siku moja Luten Kanali Likvol Shekvov mkufunzi wa tabia na hisia za kibinadamu katika chuo cha majasusi cha Russian Federal Security Service (RFSS), alibainisha kuwa hulka za kibinadamu huathiriwa na unafiki, lakini unafiki usio na bughudha "unaolipa zaidi" ni ule ufanywao na wazee. Chuo hiki ni maarufu ulimwenguni kwakufundisha majasusi, na hasa ufundishaji wa somo maarufu liitwalo ujasusi wa kisaikolojia (Forensic psychology). Ndani ya kozi hii ndimo huzaliwa ama hupatikana majasusi wabobevu wa saikolojia ya binadamu na mazingira ambao kwa lugha ya kijasusi huitwa Profiler.

Pengine kama ilivyokuwa kwa Rais Boris Yeltsin wa Urusi kuibadili KGB kwenda FSB, hata hapa Tanzania kwa sasa kuna viashiria dhahiri hatuna mfumo imara wa kijasusi na kimsingi, tunahitaji marekebisho makubwa ambayo kimsingi ni sawa na kuweka mfumo mpya. Ni dhahiri kuna udhaifu wa mfumo wetu huo. Udhaifu huu unadhihirika katika baadhi ya michakato ya kitaifa, hasa masuala ya uchumi. Mfumo wetu wa utafutaji taarifa nyeti hauna tija na kimsingi una mianya inayoruhusu nchi kudanganywa au kutapeliwa kirahisi mno hata na kampuni kubwa za kimataifa. Baadhi wanaamini mfumo wetu bado ni imara isipokuwa taarifa hizo nyeti, mara kwa mara hazitumiki ipasavyo au hupuuzwa kabisa. Hoja hii ni nyepesi mno na binafsi siamini hivyo. Mfumo wa kiusalama ambao una mianya inayotoa fursa kwa taarifa zake nyeti zilizokusanywa kwa njia hatari na gharama kubwa kutotumika hata kama zinabeba maslahi ya nchi, huo ni mfumo dhaifu.

Mfumo wa namna hiyo unapaswa kuvunjwa au kufanyiwa marekebisho makubwa. Mfumo wa kiusalama lazima si uwe na uwezo mkubwa wa kusaka taarifa nyeti kwa njia yoyote (halali au kinyume chake), lakini pia unapaswa kujijengea mazingira ya kuhakikisha matumizi bora ya taarifa hizo kwa maslahi ya nchi. Kwa mfano, mapungufu ya ujasusi wa kiuchumi pamoja nakuwa na mfumo ambao si imara kwa sasa wa kukusanya taarifa, yameibuka madudu mengi kwenye mchakato wa ubinafsishaji. Hata ukiangalia michakato mingine muhimu kwa taifa mikono ya kitapeli imeshindwa kudhibitiwa, kwa nini? Ni dhahiri mfumo wetu ni dhaifu isipokuwa swali la kujiuliza; je, udhaifu huo uko kwenye eneo gani mahsusi? Je, ni eneo la ukusanyaji taarifa au ni matumizi ya taarifa husika? Au vyote viwili? Ndani ya maswali haya, ufumbuzi muhimu unaojitokeza ni kwamba; tunahitaji mfumo imara zaidi wa kiusalama nchini na hasa kwenye eneo la uchumi na siasa kama ilivyo kwa Urusi ya Yeltsin kwa wakati ule.

Mfumo ambao si tu utakusanya taarifa kwa mujibu wa mahitaji lakini pia taarifa hizo zitajengewa mazingira ya lazima ili kutumika kwa manufaa ya nchi. Hakuna sababu ya kuendelea kuwa na mfumo ambao utekelezaji wa taarifa zake unategemea upeo wa kiongozi mkuu pekee, ingawa pia Rais ni taasisi. Tujenge mfumo ambao ingawa utahitaji wanasiasa, wachumi, wahandisi, wanasheria na wanataaluma wengine lakini kamwe usiwe na maslahi ya moja kwa moja na makundi hayo wakati wote. Kwa sasa, inawezekana mfumo wetu umefungamana zaidi na utashi wa baadhi ya wanasiasa kuliko utaifa. Tunahitaji kujenga mfumo mpya imara wa kiusalama ambao utakuwa karibu na taaluma zote nyeti lakini hautafungamana na maslahi ya taaluma hizo wala wanataaluma husika.Hii itasaidia kujenga mwelekeo wa taifa katika mazingira halisi ya mwelekeo wa dunia na si mazingira ya utashi wa wanataaluma au wanasiasa husika.

Kwa bahati mbaya, mfumo wetu wa sasa umejenga hisia kwa umma umetekwa na wanasiasa na zaidi, ni mfumo uliowekezwa katika siasa kuliko eneo la uchumi. Chombo chetu hiki lazima kicheze vilivyo na kwa ustadi disko la dunia kuhusu uchumi zaidi na si siasa pekee. Hisia kwamba mfumo wetu wa kiusalama ni dhaifu zina ushahidi. Pale tulipopaswa kudhibiti au kuchukua hatua kabla, tumeshindwa kufanya hivyo na hatimaye kufikwa na madhara yasiyo ya lazima. Matapeli wasiojaa hata mkononi wanaingia popote na kufanya wizi wa mali za umma. Wengine wanafanya hivyo wakijiita wawekezaji wa kimataifa ambao baadhi ya makuwadi wao ni wanasiasa au wataalamu wetu mashuhuri nchini.Kama tunafeli kudhibiti masuala yaliyoko ndani ya uwezo wetu tutawezaje kupanga na kutekeleza mipango ya kupata taarifa nyeti kutoka kwa mataifa mengine ili tujenga taifa bora zaidi katika ushindani wa kidunia? Kwa nini hata wale wanaojifunza au kuchipukia kwenye utapeli wa kimataifa (wawekezaji), Tanzania iwe sehemu yao ya mazoezi?

Soma kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi.......

Kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi ni 80,000/= tu.

Piga simu 0715865544 au 0755865544 popote ulipo utaletewa...

Na Yericko Nyerere
 
Hao usalama wa taifa sasa hivi wanashinda huku kwenye mitandao ya kijamii kutishia wakosaoji na kuharibu mijadala inayaoikosoa serekali na hasa pale rais anapokosolewa. Ikifika jioni wanakwenda bar kutongoza mabar maid na kuishia kujisifia kwamba wanaijua sana serekali, huku wakati mwingine wakilewa kuonyesha vijibastola vyao.
 
Hivi Tz kuna sheria inayozuia serikali kudukua mawasiliano ya raia wake ? Kama
Haipo , kwanini Hawa wabunge wasitunge sheria hiyo ? Na cha msingi Kwa Ndugu Nape, Katika Mawasiliano yako kuwa “Clean “ kwani hakuna neno la Siri hasa unapoongea kupitia mitandao. Ukitaka Siri , ongea na huyo mwenzako face to face
 
Kama kweli aliyosema Mkuchika, hao wasaka taarifa na kushauri serikali walikua wapi wakati wa epa, escrow, makinikia etc

Walikua wapi mpaka watu wasiojulikana kuingia hadi maeneo ya viongozi na kudhuru viongozi pasipo kushikwa?

Walikua wapi wasiishauri serikali madudu ya bandarini kipindi chote hadi makontena zaidi ya 11000 yanapita badnarini
 
Nape anaona kila kitu kiwekwe mjadala waingize siasa. Ndo mana jpm husema ntakata hapa au kule ili niwaletee pesa na maendeleo yapatikane pasi na kupiga kelele za bunge. Ila naona watu wasiojulikana wametrendi kipindi hiki.
 
Hao usalama wa taifa sasa hivi wanashinda huku kwenye mitandao ya kijamii kutishia wakosaoji na kuharibu mijadala inayaoikosoa serekali na hasa pale rais anapokosolewa. Ikifika jioni wanakwenda bar kutongoza mabar maid na kuishia kujisifia kwamba wanaijua sana serekali, huku wakati mwingine wakilewa kuonyesha vijibastola vyao.


HABARI,
"tindo,
Hayo unayoyasema unauhakika nayo,Nielekeze Hiyo Bar na mimi nikawaangalie,
Utakuwa umenisaidia sana ndugu.

LUMUMBA
 
Kama kweli aliyosema mkuchika, hao wasaka taarifa na kushauri serikali walikua wapi wakati wa epa, escrow, makinikia etc

Walikua wapi mpaka watu wasiojulikana kuingia hadi maeneo ya viongozi na kudhuru viongozi pasipo kushikwa?

Walikua wapi wasiishauri serikali madudu ya bandarini kipindi chote hadi makontena zaidi ya 11000 yanapita badnarini
hii amani iliyotawala na kutamalaki Nchini Hadi wewe Na mke wako mnalala salama unajua inatoka wapi? Hatulali kila siku tuko macho hili muwe salama halafu mnatujadili humu. Nchi jirani zinawaonea geree mnavyoenjoy amani. Ngoja tuwatafute Sasa mtueleze vizuri
 
Kama kweli aliyosema mkuchika, hao wasaka taarifa na kushauri serikali walikua wapi wakati wa epa, escrow, makinikia etc

Walikua wapi mpaka watu wasiojulikana kuingia hadi maeneo ya viongozi na kudhuru viongozi pasipo kushikwa?

Walikua wapi wasiishauri serikali madudu ya bandarini kipindi chote hadi makontena zaidi ya 11000 yanapita badnarini
Umesajibiwa na bado unauliza usilolielewa umeshambiwa ni hayo mambo manne je katika hayo umeona imeandikwa kukamata mtu,??
 
Nimemsikiliza waziri,, kama kazi ya usalama wa Taifa ni kutafuta habari na kuishauri seao usalama wa taifa sasa hivi wanashinda huku kwenye mitandao ya kijamii kutishia wakosaoji na kuharibu mijadala inayaoikosoa serekali na hasa pale rais anapokosolewa. Ikifika jioni wanakwenda bar kutongoza mabar maid na kuishia kujisifia kwamba wanaijua sana serekali, huku wakati mwingine wakilewa kuonyesha vijibastola vyao.
Bwana mdogo chunga ulimi wako nitawatuma Sasa hivi vijana wangu Rama Na Frenki
 
Anachokataa Mkuchika ni nini sasa?Nape anasema kweli kwamba idara hii haifanyi kazi zake sawaswa,ingekuwa inafanya hizi kashfa kubwa zilizowahi kutokea zisingekuwepo.kwa jinsi ilivyo labda awamu hii ya tano watakuwa wanafanya hizo kazi na kuishauri serikali kimyakimya
 
hii amani iliyotawala na kutamalaki Nchini Hadi wewe Na mke wako mnalala salama unajua inatoka wapi? Hatulali kila siku tuko macho hili muwe salama halafu mnatujadili humu. Nchi jirani zinawaonea geree mnavyoenjoy amani. Ngoja tuwatafute Sasa mtueleze vizuri


Du amani huwa inalindwa na kitu moja, haki, haki haki na sio kama unavyowaza kama samaki aina ya pweza.

Eti mnalinda amani .....du huoni hata aibu. Kuna wadudu fulani wanakaa kwenye kinyesi cha ngombe kilichooza naogopa sana kukufananisha na huyo mdudu
 
Kama kweli aliyosema mkuchika, hao wasaka taarifa na kushauri serikali walikua wapi wakati wa epa, escrow, makinikia etc

Walikua wapi mpaka watu wasiojulikana kuingia hadi maeneo ya viongozi na kudhuru viongozi pasipo kushikwa?

Walikua wapi wasiishauri serikali madudu ya bandarini kipindi chote hadi makontena zaidi ya 11000 yanapita badnarini
Kama siyo usalama wa taifa hayo uliyo yataja usinge yaskia kiongozi,

Usalama wa taifa huwezi kuwalaumu, hamna mwenye ushahidi kama ishu ya escro hakuwakutoa taarifa sehemu husika,

Ishu ni viongozi wakuu wa serikali na mawaziri kuwa sehemu ya wapiga deal hao ndiyo wa kuwalaumu kwa kupewa taarifa na kuziweka kapuni
 
Back
Top Bottom