The Dictator
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 4,323
- 11,762
PIRANHA ni aina ya samaki wa maji baridi wanaopatikana hasa katika mito ya Amerika Kusini, kama vile Mto Amazon.
Piranha wana meno yenye ncha kali sana, yaliyojipanga kama mswaki, yanayoweza kukata nyama kwa haraka sana
Piranha huwa kimakundi, hula pamoja na wana tabia ya kushambulia kwa pamoja (swarm), hasa wanapokuwa na njaa au wakisumbuliwa na kujihisi wapo hatarini.
Zaidi, wanaweza kunusa damu au harufu ya nyama kwa hata ikiwa katika umbali mrefu.
Kuna aina 2 Maarufu:
RED-BELLIED piranha (Pygocentrus nattereri) – Wana tumbo jekundu na ndio maarufu zaidi.
BLACK PIRANHA – Wana nguvu kubwa ya kung’ata.
Ukweli na Mambo ya Kufahamu:
Ingawa wana sifa ya kuwa hatari, mara nyingi piranha hawawashambulii watu tu bila sababu ila isipokuwa tu pale wanajisikia kutishwa au wawapo na njaa sana.
Faida zao: Huchangia katika mfumo wa ikolojia kwa kuondoa samaki au wanyama waliokufa au wagonjwa. Hii ni kama ilivyo kwa ndege na wanyama wa nchi kavu kama tai (vultures) na Fisi.
TAMBUA PIA; Wanaweza kufugwa katika mizinga ya samaki (aquariums), lakini ni lazima wachungwe kwa makini sana lasivyo huwa hatari kwa mfugaji na viumbe wengine walio katika mazingira hayo.