Umesema Kuwa Ulijifunza kukaa bila kufikilia, pia ukagundua kuwa unapokaa bila kufikilia ndipo mtu anaweza kupata furaha halisi na kujitambua pia kunaongezeka.. swali ni kwamba mtu asiye waza chochote anawezaje kuwa na furaha na kujitambua kama unavyodai, wakati mawazo ndio source ya kutengeneza uhalisia wa vitu anavyovitaka binadamu? au usipo waza vitu unavyo vihitaji vitakuja automatically? maana ninavyojua mimi kama nahitaji kuwa na nyumba nzuri lazima niiwaze kwanza kabla sijaanza ku_implement effort kuipata, sasa utasemaje kuwa usipowaza chochote ndipo utakua na furaha!! How does it work? explain..
Umesema Kuwa Ulijifunza kukaa bila kufikilia, pia ukagundua kuwa unapokaa bila kufikilia ndipo mtu anaweza kupata furaha halisi na kujitambua pia kunaongezeka.. swali ni kwamba mtu asiye waza chochote anawezaje kuwa na furaha na kujitambua kama unavyodai, wakati mawazo ndio source ya kutengeneza uhalisia wa vitu anavyovitaka binadamu? au usipo waza vitu unavyo vihitaji vitakuja automatically? maana ninavyojua mimi kama nahitaji kuwa na nyumba nzuri lazima niiwaze kwanza kabla sijaanza ku_implement effort kuipata, sasa utasemaje kuwa usipowaza chochote ndipo utakua na furaha!! How does it work? explain..
Habari wakuu. Naamini wote ni wazima katika safari yetu ya Maisha ya sasa hapa duniani.
Nimependa kuanzisha mada hii kutokana na kuwa ni watu wachache sana walioweza kujifunza hili. Katika maisha yangu ya utafutaji na kujaribu kujifunza vitu mbalimbali nilijikuta katika hatua ambayo ilinifungua macho kwa undani sana.
Kupitia meditation, vitabu, mafundisho ya walimu wa imani na sayansi pamoja na kujichunguza nilikuja kuona kuwa Wazo/Mawazo yoyote (au thoughts kwa kingereza) yana nguvu kubwa sana katika maisha yetu. Kupitia meditation nilijifunza kuweza kukaa bila mawazo na nikajua kuwa mawazo/akili inaweza kukaa bila kufikiria chochote na ikiweza kukaa hivyo ndipo furaha inapokuja na kujitambua kunaongezeka. Pia nilijifunza kuwa wazo sio mimi. Mimi na wazo ni vitu viwili tofauti. Mwanadamu anaweza kulikubali wazo au kulikataa pale linapokuja akilini. Na mwanadamu anaweza kukaa bila wazo akilini, kitu ambacho ni kigumu kwa wengi. Hata hapo unaposoma hii post kuna wazo kichwani linacheza na linataka wewe ulikubali au ulikatae.
Ukikaa ukajiangalia au kutazama vitu vinavyokuzunguka utaona kabla ya hivyo vitu kuwa vitu vilikuwa ni viwazo/mawazo katika akili ya mtu fulani. Mfano madirisha, kifaa unachotumia kusoma hii mada, malazi, n.k vyote vilikuwa ni mawazo hapo mwanzo na vikaanza kutokea kweli na hivi sasa unaviona katika dunia ya kifizikia.
Kuna dunia ambayo ni limitedless, haina mwanzo wala mwisho, hakuna anayejua ipoje bali tunaona matokeo yake tu, na dunia hiyo ni MIND au Visualization halafu kuna dunia ya kifizikia. Ili kitu kitokee lazima kianzie katika dunia ya Wazo. Mfano helikopta hapo mwanzo ilianza kama wazo, mtu alijisemea au alihisi kitu kama helikopta (au kitu kinachoweza kupaa), halafu akatendea kazi wazo hilo (akajaribu kuunda na kutengeneza), halafu akafanikiwa na wewe leo unaiona helikopta. Pia unaweza kuchukua mfano wa kitu chochote ambacho mwanadamu amekiumba utaona kilianza kama wazo ndipo kikatokea baada ya kutendewa action.
Unaweza ukafanya zoezi la kuchunguza kila kinachokuzunguka hapo ulipo halafu hesabu ni vingapi vinavyokuzunguka ambavyo uliwahi kuvifikiria/kuvihisi/ au kuvizungumzia. Mimi naamini kuna siri kubwa katika mind ya mwanadamu.
Ni somo ambalo sio kila mmoja atalielewa lakini tambua kwa ufupi kuwa UNAUMBA KUPITIA MAWAZO, HISIA, IMANI NA MATENDO YAKO. Unapoamini jambo fulani unalifanya litokee na kila kitu kitajipangilia kama unavyoamini. Hata kama unaamini baya utalipata na hata kama unaamini zuri utalipata.
Hata sayansi inasema THOUGHTS ARE ENERGY LIKE WAVES. Chukulia mfano wa redio. Mawazo ni mawimbi ya redio na Universe ni channel. Kama una mawazo mazuri unapelekea mawimbi mazuri kukuzunguka na kuona vitu vizuri kiuhalisia.
NDIO MAANA INASEMEKANA HUWEZI KUBADILI MAISHA YAKO KAMA HUJABADILI MITAZAMO YAKO NA AKILI YAKO. TTUANGALIE MAWAZO TUNAYOWEKA KICHWANI AU VITU TUNAVYOVIAMINI KWANI VINAWEZA KUTUTAWALA NAKUKUA KATIKA DUNIA YA KIFIZIKIA.
Asanteni.
Kwel kabisa nakubalian na ww sasa ngoja nikulize kwa mana hata magonjwa huwa tuna ya attract kupitia mawazo yetu
Ndo maana wanafalsafa wakubwa kama plato wanasema kile unachokiona na kukishika mfano kiti hicho sio kiti halisi ila kiti halisi kipo ktk akili yako
Kwanza pokea "like" halafu hoja itachangiwa baada ya tafakuri ya kina ya mada.
Karibu sana. Ningependa watu ambao wanapenda kujifunza ambao tunaweza kutumia uzi huu kubadili maisha yetu, kuzungumzia kwa undani juu ya hii mada.
Napenda maoni na mazungumzo katika mada zaidi ya "likes".
Mkuu Apollo umeongea vizuri sana nami naongeza kuwa iyo mind is the most complex mechanism ever known in the world history nazungumzia subconscious mind maana yenyewe inafanya kazi in the background kwa kila mtu inasubiri instructions ili itoe reaction
Na kwa maelezo yako sidhani kama unazungumzia conscious mind bali subconscious mind ambayo ndo very creative when employed lakini pia mawazo [thoughts] kama ulivyoelezea kwamba kuna ile dunia ambayo ni limitedless me naifananisha na umeme yaani individidual= positive then ile dunia ya kifizikia =negative na thoughts ndo ina form circuit or system.