Unadili vipi na vihererere, watu wa majungu, kujipendekeza, waongo na wasingiziaji maeneo ya Kazi

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,735
Kuna watu wamepanda vyeo kwa fitna na kuwageuka na kuwasingizia wenzao
Kuna watu wako radhi hata kuchonganisha wafanyakazi wote maeneo ya Kazi
Kuna wengine wanapenda kuogopwa hata kama hakuna sababu ya msingi
Kuna wengine maisha yao yote ni upambe na umbea hata kama mnacheka na kufahamiana kwa karibu wala sio miujiza ukisikia chuki zote kwako yeye ndiye anazisambaza.

Kwa uzoefu mdogo nilionao haya nimeyaona makanisani, kazini, kwenye vyama, vyuoni wafanyabiashara nk

Unadhani ni mbinu gani za kuishi katikati ya haya mazingira maana hayakwepeki kwa kila mwanadamu Hai... Hasa miongoni mwetu waTZ.

Nawasilisha...
 
Unamaanisha watu kama DAB???? Wa namna hiyo huwa nawacheka kwa "dharau"
 
normally hawajamaa wanapenda kumjua mtu sana {mazoea ya kiajabu} ss mm huwasipendi kabisaa mtu anijue sana so huwa ni salam nafanya yangu na kuamsha, tuheshimiane tupendane lkn tusijuane sana kujuana kirahisi hepelekea kuzinguana kirahisi2 huwa nnawadauwangu ktk pumba na mazoea
 
Nilimfata nilimchana live, alibabaika sana hajui akubali au akatae. Nilinwambie ntakulamba mitama ya nguvu na kazi naacha mshenzi wewe.
Hapa tunatafuta ridhiki hatutafutani roho, mwisho aligundulika aliishi maisha magum sana.Na alihamishwa wilayani huko.
 
Nilimfata nilimchana live, alibabaika sana hajui akubali au akatae. Nilinwambie ntakulamba mitama ya nguvu na kazi naacha mshenzi wewe.
Hapa tunatafuta ridhiki hatutafutani roho, mwisho aligundulika aliishi maisha magum sana.Na alihamishwa wilayani huko.
Safi sana, Biti huwa linasaidia wakati mwingine. Hawa ni watu ambao hawajiamini na maisha yao na wapo wengi sana maeneo ya kutafuta riziki.
 
Kwanza ni kumdharau mpaka anahisi kajichafulia,mbili unakata mazoea kabisa na mwisho siku akikuletea za kuleta react mpaka kutaka kumzaba mbele za watu.
Heshima itakuwepo sn, nilifanya hivo kwa mtu weeee ananiogopa na kuniheshimu mpaka kifo
 
Hakuna ugumu zaidi ya ule ambao boss ndo mpiga majungu kazini
hii ndio mbaya kupitiliza. Kuna jamaa amewahi kusingiziwa mambo, akachukiana na mwenzake kumbe Bosi ndio mtunzi wa uongo huo. Jamaa akakasirika akamchana bosi wake ila kilichotokea baada ya bosi kuambiwa ukweli bosi kaweka kinyongo akawa anakosoa na kumsema vibaya kila kitu chake. Kwa bahati nzuri yule bosi aliondoshwa mwenzake aliyempania kumfukuza akabaki.
Bosi akiwa source ya majungu, uongo na uchonganishi hapo mahala sio salama tena.
Uko sahihi mkuu
 
Kuwa bize na kazi zangu pamoja na kumuomba sana mungu maana daah kazini kugumu sana usiombe uwe kwenye kitengo cha fedha hata kama umeanza kazi na mshahara mdogo lakini watakuwekea fitina mpaka basi.Msingi wa kudumu ni kuchapa kazi kwa bidii na kuwa mwaminifu wa hali ya juu na kujiepusha na mazoea na watu.

NB;Kuna kanuni moja ninayoitumia inayosema"Usifurahi sana kuwa karibu na mtu maana kuwa karibu sana na mtu ni kukaribisha uwezekano wa kugombana na huyo mtu"
 
Licha ya kuwepo au kutokuwepo watu wa aina hiyo ambao wapo karibia kila mahali. Jikite zaidi kwenye mambo ya kazi, usilete mambo binafsi zaidi kazini. Hautajuta japo ujiandae kuambiwa unajisikia au unakiburi lakini faida ni nyingi sana.
 
Back
Top Bottom