GE2025 Unadhani kwanini watu wanajiandikisha zaidi ya mara moja kwenye daftari la wapiga kura?

GE2025 Unadhani kwanini watu wanajiandikisha zaidi ya mara moja kwenye daftari la wapiga kura?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Wakuu

====

Ivi kwanini wananchi wanajiandikisha zaidi ya mara moja katika daftari la kudumu la wapiga kura ni kwamba elimu ni ndogo au wametumwa kufanya hivyo kwa nia kupiga mara 2?

Mkurugenzi wa uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) nchini Tanzania Ndg. Ramadhan Kailima amekabidhi kwa jeshi la Polisi majina 8703 ya waliojiandikisha zaidi ya mara moja wakati wa zoezi la uboreshaji wa taarifa kwenye daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2024/2025.

Akizungumza julai 26,2025 katika uzinduzi wa ratiba ya uchaguzi wa mwaka 2025 wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika Jijini Dodoma Kailima amesema kwa mujibu wa kifungu namba (114) cha sheria ya uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani namba (1) mwaka 2024,ni kosa kujiandikisha zaidi ya mara moja na akisema kuwa sheria rejewa zimeeleza adhabu zake kwa watakaokutwa na hatia.


Akieleza yaliyomo katika orodha hiyo ya waliojindikisha zaidi ya mara moja amesema; "moja ina namba ya mpiga kura aliyojiandikisha kwenye kila kituo ambacho alijiandikisha zaidi ya mara moja,pili ina majina ya wapiga kura aliyotumia katika vituo hivyo tofauti baadhi ya majina yamefanana mengine hayafanani,pia ina jina la Mkoa Halmashauri,kata na jina la kituo ambalo ameniandikisha zaidi ya mara moja."Amesema Ndg. Kailima

Soma,Pia: Kailima awataka Wananchi wajitokeze kuhakiki, kuboresha taarifa zao, atembelea Vituo vya Wapiga Kura - Tabora

Akiendelea zaidi amesema orodha hiyo inatarehe na muda aliojiandikisha kwenye vituo hivyo,ina namba za simu ambazo alizitumia kujiandikisha kwenye vituo hivyo,ina alama za vidole alizoweka kwenye kituo cha kuandikisha wapiga kura na mwisho ina picha alizopiga kwenye vituo hivyo.
 
Kwasababu ninaamini hawafanyi kwa bahari mbaya
 
We unaamini kuwa wamejiandikisha zaidi ya mara moja!? Na unaamini kuwa 37m wamejiandikisha?
 
Back
Top Bottom