Unachokiona wewe; Wao hawakioni, usiwalaumu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
UNACHOKIONA WEWE; WAO HAWAKIONI, USIWALAUMU.

Na, Robert Heriel.

Andiko hili lamfaa yeyote, Kwa umri wowote aweza kulisoma. Imetumika lugha laini wala sio Ile lugha ngumu mliyonizoea nayo.

Niite Taikon wa Fasihi, Kuhani katika Hekalu jeusi.

Kila mtu Yu anamacho yake, yu anaukomo wake wa kuona na kutafakari, ukishalijua hili basi nakuambia upo katika nafasi nzuri.

Watu wengi wameshindwa, wameangamia na kuanguka katika mashimo yenye kiza cha umasikini, wamevutwa na kamba za ujinga, wamepotea katika mapori ya taabu, sio Kwa sababu wao walikuwa wajinga, sio Kwa sababu wao walikuwa masikini, Hasha! Isipokuwa wakiona Kwa macho ya watu wengine, walisikia Kwa masikio ya watu wengine, hawakuzitumia akili zao kwani hawakuziamini, walitumia akili za wengine.

Msemo aupendao Rais Mstaafu Jakaya Mrisho kikwete, usemao; Zakuambiwa changanya na zako" unamaana kubwa mno. Hasa katika ulimwengu huu wenye ushindani, hila, husda, vijicho, fitna na chuki.

Maneno ya wazazi, ndugu, au rafiki Kama sio jamii ni yakuayaendea Kwa tahadhari Sana. Mzazi anapokuambia utashindwa haimaanishi utashindwa, au anapokuambia utaweza haimaanishi utaweza kweli. Isipokuwa anajaribu Kueleza vile Macho na akili yake ilipofikia kukuona na kukutafakari.

Nyuma kidogo nilipokuwa nasoma, katika shule ya kata huko Kwetu Makanya, watu wengi hawakuamini katika uwezo wangu wa darasani.
Siku moja nikiwa na Bibi nyumbani, nikamuuliza "Hivi Bibi nikifaulu Nani atanisomesha?" Bibi akaacha kuchambua Ngwasha(pia hujulikana Kwa jina la ''Fiwi'') akanijibu; " wewe faulu alafu uone, ninauhakika utasoma" Bibi alinijibu tukitazamana.
Kisha baadaye akaongezea, Ila sina uhakika kama utafaulu maana" akaishia hapo.

Nilipomdodosa Mama naye, nikaona haniamini licha ya matokeo yangu ya mtihani wa Mock kuwa na matumaini lakini Hakuwa na Imani na Mimi yamoja Kwa moja.

Ningeweza kukata tamaa, lakini Jambo moja la hakika ni kuwa nilijua kuwa HAWAONI NINACHOKIONA, hivyo walinipa kazi kuwaonyesha kile nikionacho ambacho hawakuwa wanakiona.

Sababu zao zilikuwa, waalimu wachache, vitabu hakuna, hawakuwa na pesa za kunipeleka Tuition, na hata hivyo shule haikuwa na rekodi nzuri, kuna wakati ilikuwa haifaulishi hata mtu mmoja kwenda Kidato cha tano, na wakati mwingine ikifaulisha Sana basi ni wanafunzi 12 tuu Kati ya wanafunzi 100 na ushee. Zingatia pia sikuwahi kushika nafasi za juu darasani kuanzia nafasi ya 1-8 Unaweza kuona ni kipi kilifanya wazazi wangu
Wasione kile ninachokiona au kukiamini.

NILIFAULU! nikiwa nimeshika nafasi ya Kwanza katika shule yetu hiyo Kwa mwaka ule, nikiwa na wanafunzi wenzangu wanne, jumla na Mimi tukiwa watano.

Jambo hilo lilishtusha wengi, sio wazazi wangu tuu hata wanakijiji ambao hawakunitarajia kabisa. Sio kwamba sikuwa na uwezo Hasha! Bali waliniona ndio ninauwezo lakini hautosho kunipeleka Kidato cha tano.

Mfano wa pili,
Mwaka 2018 nikiwa na mwaka mmoja tangu nimalize Chuo kikuu Pale Udsm, nilikuwa nikifundisha Shule ya Dar es salaam Prime High School iliyopo Bunju B.
Siku moja Madam Fatma(tuliyekuwa tunafundisha wote) alipigiwa simu na Kampuni ya Vodacom aende akafanye usaili kwani aliwahi tuma maombi. Fatma akaniomba nimsindikize siku iliyofuata, Kwa vile nami nilikuwa na Ratiba ya kwenda kuchukua Cheti pale chuoni. Hivyo Udsm na mlimani city Kwa vile ni pia na mdomo tukaenda, tukiwa njiani nikamuambia Fatma, nikienda Chuoni nikarudi nikakukuta bado hujafanya usaili basi nami nitafanya usaili hata Kama sijaomba kazi wala kuitwa kwenye usaili. Akabisha. Nikamuacha akaingia Mlimani City Mimi nikaendelea na Safari kwenda Chuo.
Baada ya masaa matatu nikawa nimeshachukua cheti Chuoni, nikawa narudi, kumpigia Fatma ananiambia bado hajafanyiwa usaili kwani watu walikuwa wengi, Ila yeye zamu yake ndio inafika.
Nikafika nikakuta keshaingia kwenye usaili, nikakuta bado watu kama ishirini hivi. Baada ya dakika kumi hivi akatokea mtu aliyevalia Suti maridadi, akaita majina watu kumi hivi, watu Wale wakaingia ndani,
Hapo nikamuita Yule mtu, nikamwambia nilikuja mida ya saa tano mpaka sasa hivi sijasikia jina langu, akaniuliza ninaitwa Nani, nikamjibu, akajaribu kufuatilia makaratasi aliyokuwa ameyashika huku Mimi nikijua nimefanya udanganyifu kwani jina langu halikuwepo na wala sikuomba kazi wala kuitwa, akaniuliza nilipigiwa simu nikajibu ndio, basi akaniambia Kwa vile limebaki kundi la mwisho ambalo ni hao watu kumi basi nivumilie. Akaandika jina langu Kama mzaha vile.

Baada ya nusu saa Fatma anatoka anakutana na Mimi, akafurahi akaniambia tuondoke, nikamwambia anisubiri kwani nami naingia kwenye usaili, akaduwaa na kabla hajaongea chochote Moja ya Ma-HR akatoka na kusababisha Fatma aingiwe na hofu ya kuonekana ananichoresha maswali ya humo ndani. Akatoke nje kabisa akiniacha. Punde tukaitwa tukafanye usaili, tulifanya Oral interview kisha tukaja Usaili katika Computer. Tukamaliza.

Baada ya wiki mbili matokeo yanatoka, katika waliosailiwa 270 waliochaguliwa walikuwa 40 nami nikiwepo. Fatma hakuamini kwani hakuna nilichokuwa nakiona.

Sitaki kuwachosha wala sio dhamiri yangu kujisifu hapa.

Nachotaka kusema ni hiki,
Unaweza ukawa na ndoto Fulani katika Maisha, unaweza ukawa na mipango mizuri ambayo unaiona utaiweza kuifanya lakini mipango hiyo unashindwa kuitekeleza Kwa sababu unasikiliza maneno ya watu wanaokukatisha tamaa. Wanaokuambia hauwezi.

Wanakuambia hauwezi Kwa sababu ndivyo macho Yao yaonavyo, hawaoni Kule unapoona wewe. Kwenye macho kuna kitu kinaitwa upeo. Kila mtu anaupeo wake wa kuona, wapo wanaoonja mbali, wapo wanaoona karibu na wapo wanaoona umbali WA kawaida.

Mtu anayeona karibu hawezi kukushauri Jambo unaloliona Kwa mbali Sana, huyo atakuambia haliwezekani Kwa sababu kwenye upeo wake halioni. Wala usilaumu tena usimchukie, sio kosa lake isipokuwa haoni mbali.

MAMBO YANAYOATHIRI MUONO WA MTU.

1. Elimu.
Kwa kiasi kikubwa elimu huchangia muono wa mtu katika maisha. Mtu mwenye elimu kubwa mara nyingi huwa na muono mkubwa kuliko mwenye elimu ndogo. Hata hivyo Inategemea na Aina ya elimu.

Watu wengi wenye elimu kubwa huamini na kuona kuwa wakijiajiri katika Jambo Fulani wanauwezo wa kufika mbali kwa Yale wanayoona, lakini kutokana na kuathiriwa na Mazingira ya nyumbani ambayo wazazi wengi hawajasoma na hawaoni mbali huwashauri waachane na wazo la kujiajiri.

Sijasema kuajiriwa huwezi fika mbali Hasha!

2. Historia ya Familia na Asili.
Asili pia huchangia mtu kuona mbali au karibu. Kama Baba na Mama au Bibi na Babu walikuwa wanaona mbali ni rahisi Kwa watoto au wajukuu kuona mbali.
Mzazi anaouwezo wa kuamini wazo la mtoto Kwa sababu atalipima na kuliangalia Kwa muono wa Mbali.

3. Serikali na jamii.
Ikiwa serikali inaviongozi wenye muono WA mbali hii huweza kuathiri na wananchi wankawaida kuwa nauono WA mbali. Lakini Kama Viongozi ni low Vision, jamii nayo huathiriwa na kuwa na muono WA karibu.

Jinsi ya kuwa na Muono mkubwa/muono WA mbali.

1. Jitathmini ujue mi kitu gani unakipenda.
Na sio usombwe na upepo wa mkumbo wa fasheni wa kile jamii ikipendacho.
Utajuaje kitu Fulani unakipenda?
Kitu unacholipenda ni kile ambacho unakifanya Kwa furaha pasipo na sababu nyingine yoyote Ile. Yaani unafanya kazi unaifurahia hata Kama unalipwa Mshahara Mdogo.

2. Pata elimu na Ujuzi wa kitu ukipendacho.
3. Kifanyie kazi, Kwa kuisaidia jamii yako.
4. Wafundishe wengine wanaopenda kazi hiyo

Usiwalaumu wala kuwachukia Wale wasioona kile ukionacho siku zijazo.
Wasikukatishe tamaa Kwa maana hawaoni kile ukionacho.

Ingawaje wapo wanaoona kile ukionacho lakini kutokana na wivu au chuki huweza kukukatisha tamaa Kwa makusudi ili usifike Kule upaonapo.

Zingatia; usiwe muoga wa matokeo pale unapofuata kile ukionacho. Usifikirie matokeo Bali wewe songa.

Niishie hapa, Wale wa kusema nyuzi ndefu mnisamehe nimejitahidi kufupisha.

Ni Yule Mtibeli

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mkuu Hongera kwanza kwa kufika chuo kikuu.
Nimekuelewa kwa sana,Ahsante kwa ukumbusho !
 
Thread zako ndefu sana
 
Utanisamehe tuu
Utanisamehe tuu
Somo la Insha lilikupita kushoto ? Sijawahi ona umeandika kwa ufupi na kueleweka. Jambo dogo unandika weee!! siku ukitunga kitabu kitakuwa na page 2000.
Hebu jifunze kwa mwanafasihi halisi wa Afrika Shabani Robert ,alikuwa anaandika kidogo ila hutachoka kusoma kitabu chake.
Sasa kama unajiandikia usome mwenyewe sawa ila baadhi hatusomi maelezo mengi kwa kitu kodogo.
Ila samahani kama hupendi kukosolewa.
 
Back
Top Bottom