Unabii wa prof Kitila Mkumbo juu ya uhai wa vyama vya upinzani nchini unaelekea kutimia

gimmy's

JF-Expert Member
Sep 22, 2011
3,305
3,327
Kwa namna ambavyo hali ya kisiasa ya vyama vya upinzani inavyozidi kupoteza mvuto mbele ya jamii kipindi hiki cha utawala wa awamu ya tano,huenda unabii wa Profesa Kitila ukatimia.

Muda mfupi mara tu baada ya utendaji uliotukuka wa serikali ya CCM chini ya Dr Magufuli,Prof Kitila mkumbo aliandika kupitia account yake ya twitter na hapa namnukuu;

"Tunahitaji upinzani utakaojikita katika sera mbadala.Upinzani unaotegemea makosa ya serikali ya CCM pekee unaweza kupwaya sana kipindi hiki",mwisho wakumnukuu.

Nafikiri kwa hali ilivyo sasa juu ya taswira ya siasa za vyama vya upinzani nchini ilivyo ni dhahiri utabiri huu unajidhihirisha kwani ni kweli wapinzani hasa CDM walizoea sana siasa za matukio ili kuimarisha chama.

Lakini prof Kitila Mkumbo hakuishia hapo kutoa tahadhari kwa vyama vya upinzani,siku nyingine kupitia account yake ya twitter aliandika tena na hapa namnukuu,

"Upinzani uchwara hushamiri sana wakati wa serikali dhaifu.Upinzani makini huibuka wakati wa serikali makini na yenye chembe ya udikteta",mwisho wa kumnukuu.

Nafikiri kama wapinzani hawataacha siasa za kuishi kwa matukio kama walivyozoea CHADEMA,Kipindi hiki cha utawa wa CCM chini ya Magufuli huenda tukashuhudia anguko kubwa la vyama vya upinzani nchini.
 
Watoto Wa mjini wana msemo, ashakum si matusi, 'unajijambisha na kucheka mwenyewe'.
 
Prof Kitila ameonya sana wapinzani kujikita kwenye sera badala ya kuvizia makosa ya CCM lakini ,avile amewekewa label kubwa ya usaliti usoni anapuuzwa .....
hujitambui wewe. wewe unadhani ni usaliti kumbe ni mfumo kandamizi uliopo chadema. mfumo usiofuata demokrasia ya aina yoyote. angalia kina Zito ,Mwigamba pia. mfumo ambao baadae ulikuja kuua ajenda ya ufisadi ili kuwanufaisha wenyewe. mfumo ambao ulimfanya Dr Slaa ajitoe. mfumo ambao ulichakachua katiba ya chama ili viongozi waendelee kugombea kina Mbowe. mfumo gani huu.!mfumo ambao ukiuliza kitu unaambiwa mamluki umetumwa na msaliti. khaaa sijapata ona aina hii ya mfumo. ni mfumo zaidi ya udikteta.
 
Asee hawa jamaa ni sheeda!;wanavizia ccm ikosee ili wajitokeze ndo maana msigwa alikuwa anajipatia misifa kupitia kamati maliasili!!,sahv hana chanc!! ahahaaa!!
 
Nilipoona Jina Prof likanivutia nikaendelea kusoma mbele yake nilipoona Kitila then Mkumbo nikafunga page. Nikaenda zangu kwenye thread zingine.
 
Prof Kitila ameonya sana wapinzani kujikita kwenye sera badala ya kuvizia makosa ya CCM lakini kwavile amewekewa label kubwa ya usaliti usoni anapuuzwa .....
Mkuu upooo? Nakumbuka wakati ule ukiwa kulee tulikuwa tunajibizana mpaka basi. Hapa nakuunga mkono
 
Jamani mbona kila wakati Prof Mkumbo anaiota CDM? Yeye si ana chama chake cha ACT, kwa nini asiende kuzungumzia kwenye kamati zao ili waje na hizo sera? Wananchi tulieni tu mambo mazuri yanakuja. Tunangojea huu uigizaji uishe, na hautachukia muda mrefu, ndipo siasa zitaanza.
 
wakati mnasema hayo pia mkumbuke kwa wananchi ni Magufuli ndiye anang'aa,si chama.Magufuli kupendwa haina maana chama ndio kinapendwa,ni angalizo tu
 
Nilipoona Jina Prof likanivutia nikaendelea kusoma mbele yake nilipoona Kitila then Mkumbo nikafunga page. Nikaenda zangu kwenye thread zingine.
Chuki zako hazipunguzi elimu ya prof Kitila
 
Jamiiforums imevamiwa na watu wajinga sana, miaka mitano watu wenyewe watamchoka Magufuli, mke mpya unamtamani Mara kwa mara, watu wanatafakari jinsi kura zilivyoibiwa. Ccm wameanza kujenga Chama kupitia Olesendeka, Magu anazuia uovu wa serikali usisemwa hadharani kwa kuzuia waandishi wa habari kuingia bungeni. CCM iko turning point hata akifanya mema vipi watu hawaitaki tu. Rushwa ndiyo inawavusha ila miaka michache ijayo watatokaa tu hata siyo kwa kura. Msisahau ya kubaka demokrasia Zanzibar. Time will tell.Wekeni tume huru ya uchaguzi siyo makada wa CCM
 
Hii soda ya serikali ya Magu sio ile yakaiwaida na ndio maaana aliwaambia,
"Eti wanasema serikali nguvu ya soda,lakini hata soda ukichanganya na gongo utalewa tu",
by Magufuli.
 
Jamani mbona kila wakati Prof Mkumbo anaiota CDM? Yeye si ana chama chake cha ACT, kwa nini asiende kuzungumzia kwenye kamati zao ili waje na hizo sera? Wananchi tulieni tu mambo mazuri yanakuja. Tunangojea huu uigizaji uishe, na hautachukia muda mrefu, ndipo siasa zitaanza.
Ndio kama story za fisi kusubiria mkono wa mtu udondoke ila matokeo nafikiri unajua.
 
Back
Top Bottom