Una swali kuhusu uchawi na uganga? Uliza ujibiwe

Status
Not open for further replies.
Zipo ajali za kawaida zinazosababishwa na sababu ya uzembe, ulevi, miundombinu, ubovu wa magari nk.

Ila ajali nyingi husababishwa na wachawi kwa malengo maalum, vikao vingi hufanyika kuzimu na vichache huzungumzwa katika vikao vyao vya kichawi na hapo hutoka maagizo maalum kutoka kwa mkuu wao juu ya nini cha kufanya.

Sababu ya kusababisha ajali ni kupata damu kwa ajili ya kunywa na pia kuchanganya katika vyachira (zana zao za uchawi), na kuna msimu wa kuagizwa damu za walio hai (majeruhi) na pia msimu wa damu za waliokufa (maiti waliokufa ajalini) na wakati mwengine huhitajika vyote kwa pamoja.
0447429d530ff726c71a0f4a2c876746.jpg
Wachawi wanapotaka kufanya jambo hilo hutega vitu vyao barabarani na muda mwengine huonekana hata kwa macho na hivyo ndio huleta maafa
084856e7c114235540df940a9d1d83f5.jpg
Ni kama mipango mengine, wanaweza itoa gari hii Morogoro na hii Dar es salaam kwa kasi kubwa na kuwapumbaza madereva huku sehemu waliyoiandaa kwa kafara ni Chalinze.

Mara nyingi kabla au baada ya ajali huonekana vituko vingi ila kunakuwa na wenye mambo yao wakipata wanachotaka mda huo
16f7eb297530e31bdb0df448388f5de3.jpg
Pia kuna sehemu korofi kwa ajali na hapana sababu yeyote ya kawaida kutokea ajali ila kunakuwa na majini ya tangu enzi ambao hujipatia damu kwa kusababisha ajali.
3102e896b2db575338c5005be17c9dbc.jpg


Pia kuna ajali nyingine ni makafara ya wamiliki wa magari kutokana na maagano waliyofanya mpaka akapata hizo mali, na baada ya kutokea hivyo ndio pesa kwake inazidi kunawiri maana katimiza ahadi.

Majaribu ni mengi ila sio mara zote hufanikiwa maana wengine ni wazito na huepuka mitego hiyo.

Umeshawahi kuona mara nyingi magari mapya hufanyiwa visomo na makafara? Umeshawahi kuona magari yanafungwa matarasimu na hirizi? Dunia ina mengi.
9835f77eb1197229fcc02d47b06313dd.jpg
Mh! Si mchezo.
 
Paka ni mnyama ambae umbo lake hutumiwa sana na wachawi pamoja na majini
c9ed01321bbad6dd35f0e630d062f58f.jpg
na unaweza kutana na paka ila kumbe sio paka bali ni kiumbe tofauti tu kimefanya kujigeuza
672150aa55c76b1ef32c4a47b6bfa691.jpg
Pia wakati mwengine wachawi hufika katika nyumba na kuadhimia kufanya usumbufu kwa walio ndani, hivyo huanza kelele nyingi kama paka wanaopigana japo sauti zao mda mwengine kama watu
db46974518ef714a67e3f3f19f86890c.jpg
Inapotokea hivi mara nyingi hufanyika maombi au kuweka zindiko ili kukabiliana na hali hiyo na utashangaa inatoweka
157c764bdcd396fe6009eb42adf116f2.jpg
Paka wa kawaida hawana usumbufu wa aina hiyo
e9bb024f09777bbb39c5caf1847bf951.jpg
Darasa zuri sana na halichoshi kufuatilia.
 
Misekule kuiona hivi hivi tu katika harakati zao ni vigumu sana maana wamewekewa nguvu za miujiza na pia aina ya ulinzi ndani ya miili yao, hivyo unaweza hisi vituko tu au kuhisi kama kiumbe kimepita
c8f73526aa04f5224cfac50889477fe7.jpg
ila wakati mwengine hufanikiwa kuonekana na hapa ni pale ambapo nguvu ya dawa hizo zimekwisha na mpatilizaji kajisahau au kaamua kumtelekeza baada ya kutimiza lengo lake
fd30d73add588c89e90dbd36b70a2ca8.jpg
Ila pia misekule wanaweza kurudishwa hata kama wapo katika ulinzi mkubwa na hapa itategemea na nguvu ya ki Mungu inayotumika au hata ndumba.

Miaka ya nyuma mimi binafsi nilishamrudisha mtu wa aina hiyo kwa ridhaa ya wazazi na ndugu zake lakini hata hivyo alipokuja walimwogopa kumchukua na kuniacha nae nikaishi nae kwa mda mrefu na changamoto nyingi, ila alipopata fahamu walikuja kumchukua.
 
In aina ya uchawi WA kumdhuru mtu, hakuna faida yeyote kwa anaefanyiwa zaidi ya madhara kwa kuwa kivuli chake kinahamishwa na kuwekwa kwenye mti mkubwa....atakuwa yupo yupo tu hajielewi, akili zinaingia na kutoka, mwili unanyongea muda mwengine na kuwa kama zezeta.
mm nahisi nina dalili hizo..unanisaidiaje mkuu!
 
Uchawi hautambuliki katika sheria, huwezi kumshitaki mtu kuwa kakuroga wala kupeleka jambo lolote linalohusu uchawi maana hautambuliki, soma vema post niliyokujibu....karibu.
ndo maana wakikamatwa wanauawa..
 
Habari Mtu Mzito! nina maswali Nauliza je kusafisha nyota ni kuwekewa uchawi au ni nini hufanyika mtu ili nyota yake inga`e? Swali la pili inamaana kusafisha nyota ni kutoa nuks na mikosi au vizuizi vilivyo wekwa na wabaya wako (wachawi) na ukisafisha nyota vinatoka je hapo inamaana nyota haiwezi kuharibiwa tena? Na mvuto/ dawa za mvuto ndo kusafishwa nyota au? Kusafisha nyota kuna maagano yetote au kuna uhusiano wowote kati ya mambo ya giza mizimu/ majini?
 
Mkuu naomba kuuliza huu uchawi et mtu unalima shamba watu wanakuja kulichezea huwezi kuvuna hata sikumoja ukafaidika.
Na kama unashamba et kwani ni lazima na wewe uliwekee ayo madawa ya kienyeji? Na kama usipoweka ukamkabizi mungu kuna tatizo?
Uchawi wa aina hiyo upo tena unafanyika sana na ili kuukabili wengi huweka mazindiko katika mashamba yao.

Uchawi wa kufunga mafanikio hufanyika sehemu yeyote penye riziki kama vile kwenye mashamba, biashara, maofisini, kwenye migodi nk.

Yote hayo yana namna ya suluhu zake zinazofanyika katika uganga ili mhusika asichezewe tena.

Unapoamua kumkabidhi Mungu ni sahihi kabisa na uwe mtu wa imani yako sawa sawa vinginevyo utajipambanua hivyo huku wachawi wakikucheka kwa kuwa hawaoni kinachowazuia pindi wanapokuja kukudhuru.
 
Eti ili nimnase mchawi anaeniwangia Usiku nyumbani kwani,, nifanyeje maana kuna kibibi hapa kirani wanakisimulia san wajuvi wa haya mambo kuwa eti kinasumbua sana watu usiku,,

Mim nataka hiyo dawa ya kukinasa alafu nakichapa makofi matatu,, nakiruhusu kikawasimulie wenzie,,
Hakuna njia ya kufanya wewe mwenyewe kumnasa mchawi, bali yapo mazindiko ambayo ukiwekewa utamkuta mchawi wako akiwa na vitendea kazi vyake vyote.
 
Hata huko ulaya wanafanya mazindiko kwenye mabenki yao?
Uchawi upo dunia nzima na kila sehemu wana namna zao za kufanya, kwa bahati mbaya tuliaminishwa mila na desturi zetu ni potofu na tukadhani ni sisi tu ndio wenye kufuata mambo haya ya asili.
 
Je kuna madhara gani kwangu kama nashiriki sana kwenye maombi kanisani na wkt huo naenda kwa waganga kwa ajili ya tiba ya mapepo/majini na kinga(sio kuroga mtu)
Swali lako lipo katika mrengo wa kidini, na hata madhara ni katika upande wa kidini na sio upande wa ndumba.
 
Swali langu, hv zile ngoma za usiku za kichawi huwa nazisikuaga sna huku kwetu maana kwa wachawi ndo penyewe

Je nikitaka kuzifuata na kuoana wachawi wanavyofanya ntawezaje kufika huko kwenye ngoma zao! je na madhara gani naweza kupata nikikutana nao live!!!
Ni kweli kabisa wachawi hupiga ngoma mara kwa mara katika mikutano yao haswa usiku, unaweza ukazisikia hizo ngoma lakini ukazifuata usizifikie haswa kama mwili wako hauna nguvu ya kuwaona wachawi.

Umeuliza kuwa ikitokea ukawaona wachawi mubashara, je nini hutokea? Inategemea na uzito wa mwili wako lakini wengi waliowaona walipata misukosuko ya maradhi au hata kupoteza maisha.
Kwa nini? Kwa sababu utawaona watu unaowajua kabisa na pengine wa karibu yako wakiwa wamejumuika kwenye 'shughuli' hivyo watakuandama ili siri yao isivuje.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom