Samahani naomba unisaidie niiendesheje biashara zangu :- nina internet cafe, nina stationery, duka la nguo na zabuni ya kuwalisha chakula watu fulani hivi..... napenda kujua nifanyeje ili niendelee zaidi kibiashara
Thanks BantuGirl,
Nilikuwa off line kwa siku mbili tatu, lakini nimerudi na hari mpya kasi mpya. Kwanza kabisa nakupa hongera kwa kujitahidi kibiashara kwani kuwa na biashara zaidi ya moja sio jambo dogo.
Kwanza kabisa tuangalie combination ya biashara yako.
Ni imani yangu kabisa stationary and Internet cafe zina shabiana ki msingi.. Hizi biashara mbili zipo kwenye maturity stage katika business cycle, sababu in the future number of the people with internet at home will increase, however inategemea sana location ya biashara yako.
Sasa tuziangalia kwanza hizi biashara mbili, internet and stationary. Biashara hizi ni services business, hakuna product yoyote mteja anayopata kwa kufanya biashara na wewe, ila anapata huduma. Kwa hiyo rule namba one ni kuboresha hudama. Unaweza kujifunza njia bora za kuboresha huduma, kisha ukawa watrain wafanya kazi wako. Kuna njia nyingi sana za kuongeza customer service satisfaction. Moja wapo ni kuongeza quality ya huduma, kuset fair price, kutilia maanani malalamiko ya wateja ( very important).
Baada ya kuweka hili swala kwenye big picture kabla huja execute anything, nakushauri kwanza ufanye what we call 360 survey of your rivals (washindani). Angalia washindani walio kuzunguka, jee ushindani ni wa aina gani? kichwa kwa kichwa, yaani internet cafe kila hatua chache, au kuna distance between. Baada ya kuangalia washindani wako wapo wapi, pili fanya survey ya kuangalia jee washindani wako wanatoa huduma gani? Then baada ya hapo angalia jee unaweza kuboresha huduma yako kwa kiasi gani ili uwashinde (outcompete) washindani. Avoid kutafuta njia ya haraka, make sure unatengeza njia strong, na itakayo maintain wateja wako.
Moja ya njia ni kutengeza database ya wateja wako, kila mteja anapokuja muombe asign membership for free. Mwambie hiyo member ship kila anapokuja internet cafe au stationary yako atakuwa ana pata point kadhaa na kila akifikisha point kadhaa then atapata huduma fulani free. Example, mteja akija internet cafe for 1 hr atapata 2points. Akiongeza 1 more hours anapata 2 more points, akifikisha ten points anapata labda half an hour bure. au akifikisha 10points with in 3 days then anapata 1 hour. Make sure unabadilisha badilisha promotion kama hizi ili kuwafanya wateja wako wawe more exited. Mfano fanya study na angalia ni muda gani kunakuwa hakuna watu wengi, yani kupo slow... let say mida ya saa saba na saa tisa ni slow wateja wapo wachache, then unaweza kuintroduce kitu utakacho kiita HAPPY HOUR. Yaani Pay one hour and get one more hour free. Au make 10 copies and get 5 copy free. Au Free SCANNER kwa mtu yoyote aliyelipia one hour.
Kumbuka inabidi uwe na different strategies ili washindani wako washindwe kuigizia kila mara wanapo jaribu.
Duka la Nguo.
Duka la nguo ni biashara ina husu product. Hapa inaweza kuwa challange sana. Kwanza kabisa sheria namba one, RULE OF LAW usiweke nguo kwenye duka kwa more than 60 days. Yaani ni mwiko nguo kuwepo kwenye hanger kwa zaidi ya miezi miwili. Hivyo basi, always zile nguo unazoziona zimekaa muda mrefu akikisha zinakwenda kwenye promotion. Kumbuka always promotion lazima urudishe pesa yako uliyonunulia, yaani unaweza kuongeza mark up kwenye brand new inventory na kushusha price kwenye ile ya dhamani. Mfano, Nunua moja na pata nyingine kutoka kwenye shelf X (old inventory) kwa nusu price. Hii itamvutia mteja, kumbuka umeongeza markup kwenye brand new inventory, na umekata price kwa nusu kwenye old inventory.
Second, Wajue wateja wako, nini wanapenda kununua, jee ni wanatabia gani ya ununuzi? Jee wanaonekana wana kipato cha kiasi gani? Baada ya hapo unaweza kununua nguo kutokana na demand ya wateja wako. Avoid kununu inventory kwa sababu wewe umeipenda then wateja wote watapenda. Make sure wafanyakazi wako wanawatambua wateja kwa majina yao ya kwanza. Na kila wanapofika dukani, then wafanyakazi wako wanaonyesha uchangamfu ( kumbuka uchangamfu lakini keep it professional). Bishara nyingi za Tanzania zina bargaining, basi unaweza kutengeneza njia ya kubargain. Labda waambie wafanya kazi wako nguo such and such unaweza kutoa only 500, lakini mteja akinunua mbili then unaweza kutoa 1200 kwa both close. If and only if akitaka bargain.
Kingine make sure una kuwa na different sales promotion kila week. Laabda week hii jumatano only, Red Rose Sales yaani baadhi ya nguo fulani 10% off. Swala ni kuongeza customer turnover kwenye duka lako.
Always kumbuka kila baada ya kuimpliment new strategy inabidi ufanye survey kuona kama wateja wanaridhika na service wanayopewa. Jitahidi kufanya mkutano mara moja kwa week na wafanya kazi wako wakila biashara na jadili nao biashara kwa week nzima. Jee wamekutana na challange gani, na jee challange gani zinaweza kurekebishwa. KUMBUKA MFANYAKAZI ASIEFUATA MISINGI YAKO YA BIASHARA INABIDI AONYWE AU KUSIMAMISHWA KAZI MARA MOJA KWANI NI LAZIMA WAFANYAKAZI WOTE WAWE KWENYE PAGE MOJA.
Biashara ya chakula au catering.
Hii biashara ina mambo mawili muhimu. Kwanza ni chakula chenyewe na pili ni customer service. Ni imani yangu kwamba wapishi wako ni wazuri, na wanajua wanachokifanya. Na wahudumu wako umewafunza sheria zote muhimu za uhudumu katika high quality standard.
Kuna mambo machache tazama, kwanza ni chakula kupatikana on time yaani kama kusave ni 1:00pm then 1:00pm chakula kipo tayari, pili ondoa surprises, yaani sio 10 mins kabla ya kusave chakula ndio unamwambia mteja kwamba salad sikupata. Tatu, always kila baada ya kufanya biashara na mtaje omba feedback, waulize nini wanadhani kilikosewa, na nini wanadhani kinaitaji kuboreshwa. Kama biashara za juu nilivyo suggest, kutana na wafanya kazi wako kila week, jadilini mapungufu na mafanikio. Mapungufu yote lazima yashuhurikiwe.
Kama biashara za juu unaweza kutengeneza promotion ambayo ukaipa jina lolote lile. Mfano, today special. Yaani kama jumatatu ndio una catering then disert ni free. Chagua kitu ambacho hakitakuumiza kibiashara kuwa free. Always ujanja ni mmoja. THERE IS NOTHING FREE, CUSTOMER WILL PAY IT IN ONE WAY OR ANOTHER. Nadhani umenipata kwa hapo.
Basi hayo ni machache sana, kumbuka haya mambo yanaweza kufanya kazi au kukataa. Lakini always kila unapo implement new idea unaangalia inavyo work kama haiongezi mauzo then unaachana noyo. Nina uhakika ukifuata mfumo nilio suggest hakuna wa kushinda na wewe.
Biashara zako z ote hizi zinaweza kuboreshwa kwa kutumia mfumo mmoja unaitwa Total Quality Control. Yaani kwenye hudumu unayotoa there is no good enough, always kuna chance ya kuimprove.
Ni imani yangu unafahamu normal accounting kwa ajiri ya biashara. All expenses should be recorded and all sales. Wewe owner huna exception ya kuchota pesa tuu kwenye account, bali ni lazima uwe kwenye payroll kama wafanya kazi wengine. That is a law.
Goodluck, It can be done, just put your thoughts into action.