Una mpango wa kukata rufaa? - Hapana "Fransis Cheka"

Sheria ni Sheria haichagui mtu wa kumuadhibu na mtu kama yeye ambae ni maarufu, anatakiwa awe kioo cha jamii kuwaonyesha mfano kwa vijana wanaochipukia katika mchezo wa masumbwi kuwa nguvu zake ni za kutumia wakati uko ulingoni.

Hakuna sababu yeyote inampa mtu haki ya kumpiga mtu yeyote kwa kosa lolote, ndio maana tuna vyombo vya sheria kama polisi na mahakama.

Kibaya zaidi alionyesha kujiamini saana maana alipopewa nafasi ya kuleta mashahidi na kujitetea aliamua kutofanya hivyo, hali ilioonyesha hakujutia kitendo alichofanya na kukiona ni sawa.

Hili ni somo zuri kwa wanaojiona kutokana na kujulikana kwao wanaweza kuwa juu ya sheria.
 
umesema mambo ya maana sana
 

Kabla ya kulipuka, ungesoma niliyoyaandika (Kwammba 'ni kweli Cheka katenda jinai''
Sijajua unaponilaumu, au upofu unaodai ninao uko kwenye nini. Mimi sitaku kujadili mtu - ningetaka tusimjadili mtu bali twende mbele zaidi kayaangalia mazingira yanayozisibu mahakama na magereza pamoja na mifumo yetu ya sheria/hukumu.
Ungejitahidi kidogo kusoma post yangu ungeona niliyoandika!
 
Hiyo siyo kazi ya hakimu.. angekuwa na wakili ndio angewasilisha kama sehemu ya utetezi.. jamaa kwa ujumla alichukulia kirahisirahisi.. (sheria ni msumeno...)

Totally agree with you!
 
suala sio cheka ni ukosefu wa haki ya mtu

Good will basi tutanue wigo tuangalie "Haki za Watu" sio iwe jambo lake kama yeye. . . . . .ili kama ni tatizo basi tulisonte once and for all
 

Sasa unatafuta msaada au unalalamikaa, pesa alizokuwa anapata kwenye masumbwi kapeleka wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…