Una maoni gani juu kukamatwa kwa shehena ya Mafuta na Sukari Tanzania

Come27

JF-Expert Member
Dec 1, 2012
7,694
7,363
UNAMAONI GANI JUU YA KUKAMATWA KWA SHEHENA YA MAFUTA PAMOJA NA SUKUARI?

TOA MAONI JINA NA MAHALI:
Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imekamata shehena ya Sukari na Mafuta yenye thamani zaidi ya shilingi milioni mia nne ambazo zinaingianchini kutoka mataifa ya India na Brazil bila kulipa ushuru.

Shehena hiyo imekamatwa mkoani Lindi katika wilaya ya Kilwa ikiwa katika stoo ambapo hubadilishwa na kuwekwa katika vifungashio vyenye nembo za makampuni ya hapa nchini na kupelekwa sokoni.

Source: Star TV Tanzania
 
Vitu vyote hivyo vinatoka Zanzibar,naomba uulize kuna tofauti gani kati ya TRA zanzibar na ya huku bara najua system ya computer ni moja,database ni moja ?kwa nini bidhaa zinaingia zanzibar bila kulipiwa ushuru?Jee hao maofisa wa TRA bara kwa nini hawaendi kutoza kodi huko zanzibar?HILI NI SUALA LA KISIASA zaidi,HIVYO TRA INAFANYA USUMBUFU TUU KWA RAIA WAKE WA BARA.Leo zanzibar dukani sukari kilo 50 ni sh 45000 yaani kilo moja ni sh 900 wakati huku bara ni sh 95000.kilo sh 1950
 
Apo gepu ni kubwa sana. Na Mafuta ya Taa, Petroleum, diesel na Gas bei zake zikoje kwa Zanzibar
 
Vitu vyote hivyo vinatoka Zanzibar,naomba uulize kuna tofauti gani kati ya TRA zanzibar na ya huku bara najua system ya computer ni moja,database ni moja ?kwa nini bidhaa zinaingia zanzibar bila kulipiwa ushuru?Jee hao maofisa wa TRA bara kwa nini hawaendi kutoza kodi huko zanzibar?HILI NI SUALA LA KISIASA zaidi,HIVYO TRA INAFANYA USUMBUFU TUU KWA RAIA WAKE WA BARA.Leo zanzibar dukani sukari kilo 50 ni sh 45000 yaani kilo moja ni sh 900 wakati huku bara ni sh 95000.kilo sh 1950
Is this real?
 
Huo ni mwanya mkubwa na kimsingi hatuna hata hakika na ubora wa hizo bidhaa.
 
Kipindi cha mkwere bandari bubu zilikuwa nje nje yaan kulikuwa amana hata siri mchana kwepe watu walikuwa wanaingiza vitu
 
Vitu vyote hivyo vinatoka Zanzibar,naomba uulize kuna tofauti gani kati ya TRA zanzibar na ya huku bara najua system ya computer ni moja,database ni moja ?kwa nini bidhaa zinaingia zanzibar bila kulipiwa ushuru?Jee hao maofisa wa TRA bara kwa nini hawaendi kutoza kodi huko zanzibar?HILI NI SUALA LA KISIASA zaidi,HIVYO TRA INAFANYA USUMBUFU TUU KWA RAIA WAKE WA BARA.Leo zanzibar dukani sukari kilo 50 ni sh 45000 yaani kilo moja ni sh 900 wakati huku bara ni sh 95000.kilo sh 1950
Tatizo unaloongelea ni halisi lakini sio tatizo kuu la kwenye mada.

Tatizo kubwa lililoko kwenye mada ni biashara ya magendo, uchakachuaji wa bidhaa na ukwepaji kodi. Hilo swala la kubadili vifungashio ndo uchakachuaji na kiashiria kuwa hii bidhaa imeingia bara bila kibali na kwa njia ya magendo.

Hili ni tatizo kubwa kwa miaka kadhaa sasa.
 
Vitu vyote hivyo vinatoka Zanzibar,naomba uulize kuna tofauti gani kati ya TRA zanzibar na ya huku bara najua system ya computer ni moja,database ni moja ?kwa nini bidhaa zinaingia zanzibar bila kulipiwa ushuru?Jee hao maofisa wa TRA bara kwa nini hawaendi kutoza kodi huko zanzibar?HILI NI SUALA LA KISIASA zaidi,HIVYO TRA INAFANYA USUMBUFU TUU KWA RAIA WAKE WA BARA.Leo zanzibar dukani sukari kilo 50 ni sh 45000 yaani kilo moja ni sh 900 wakati huku bara ni sh 95000.kilo sh 1950
mkuu umenena kweli..mi siku zote sukari,dawa za mbu, mafuta ya kula n.k naagiza Unguja ambako bei yake ni nusu ya bei ya Dar...sijui tatizo liko wapi?
 
Vitu vyote hivyo vinatoka Zanzibar,naomba uulize kuna tofauti gani kati ya TRA zanzibar na ya huku bara najua system ya computer ni moja,database ni moja ?kwa nini bidhaa zinaingia zanzibar bila kulipiwa ushuru?Jee hao maofisa wa TRA bara kwa nini hawaendi kutoza kodi huko zanzibar?HILI NI SUALA LA KISIASA zaidi,HIVYO TRA INAFANYA USUMBUFU TUU KWA RAIA WAKE WA BARA.Leo zanzibar dukani sukari kilo 50 ni sh 45000 yaani kilo moja ni sh 900 wakati huku bara ni sh 95000.kilo sh 1950
zanzibar ni kama kwenye tax imekuwa "exempted" i mean tax free/no tax.
 
TRA ndio source ya "madudu" yote na walilijua hili toka zamani, leo kuanza kutikiswa ndio wanajifanya kufanya kazi. What kind of drama do they playing.?
 
Back
Top Bottom