una lipi la zaidi kumshika mpenzio? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

una lipi la zaidi kumshika mpenzio?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by eRRy, Apr 15, 2010.

 1. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,080
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135


  wiki hii nataka kuzungumzia namna ambavyo usipoangalia unaweza ukamshawishi mpenzi wako akusaliti bila wewe kujua. Nataka kuligusia hili kwasababu, nimegundua kuna watu wanaowapenda sana wapenzi wao lakini bila kujijua wanajisahau na kuwafanya wapenzi wao kukinai penzi lao na kuanza kutafuta mtu mwingine wa kumpatia kila anachokitamani.

  Sote tunajua kwamba mapenzi ni kuridhishana, kupeana kile ambacho kila mmoja alikitarajia kutoka kwa mwenzake. Hata hivyo, sidhani kama yupo mtu aliye tayari kuwa na uhusiano na mtu ambaye hajui mapenzi zaidi ya yale ya faragha tu.
  Ninachomaanisha hapa ni kwamba, wapo wanawake huko mtaani ambao wanajisifu kuwa wao ni watundu sana kwenye ‘mambo flani’ lakini wanashangaa kuona bado wanasalitiwa na waume zao.

  Wanawake wa sampuli hii wanaamini kwamba, ukishakuwa mtaalam katika mambo ya kwenye sita kwa sita tayari ushamshika mumeo na kamwe hawezi kukusaliti. Jamani huko ni kujidanganya!
  Tunapoyazungumzia mapenzi, tunajumuisha mambo mengi. Kama mwanaume anachokitaka kutoka kwa mwanamke ni mapenzi tu, si angekwenda kuchukua changudoa tu akapewa kila anachokitaka?
  Lakini kwakuwa mwanaume anahitaji zaidi ya mapenzi ya kwenye sita kwa sita kutoka kwa mke, ndiyo maana wanawake wanatakiwa kuwatimizia mambo mengine ya msingi yanayoweza kuwafanya wakiri kwa kusema ‘Yes! mwanamke niliyenaye ananitosha kila idara, sihitaji mwingine katika maisha yangu’.

  Ila sasa, mwanaume hawezi kusema hivyo endapo atampata mwanamke anayejua mapenzi sana lakini, hajui kupika, ni mchafu, hana ukarimu kwa ndugu jamaa na marafiki, haheshimu ndugu wa mume wala mume wenyewe! Huyu atakuwa hana sababu ya kumshawishi mwanaume kudumu naye.
  Atashangaa licha ya ‘kumtumbuiza’ ipasavyo mumewe bado anasalitiwa au kutoswa kabisa, kwanini? Kwasababu mwanaume anakosa vitu kadhaa ambavyo angevipata asingekuwa na tamaa za kijinga.

  Nini ninachotaka ujifunze kupitia somo hili la leo? Ishu ya msingi hapa ni kwamba, mapenzi ya kitandani tu hayawezi kukufanya ukamshika vilivyo mpenzi wako. Hili si kwa wanawake tu hata wanaume pia.

  Unamkuta mwanaume ni mtaalamu wa kupachika magoli wavuni lakini hamjali mpenzi wake, hamheshimu na wala hampatilizi katika shida nyingine za msingi isipokuwa penzi tu. Jamani maisha katika uhusiano hayajengwi kwa tufali moja la mapenzi tu, wanaoamini hivyo ni malimbukeni hivyo kuna kila sababu ya kubadilika.
  Ni hayo tu kwa leo.
   
Loading...