Una kazi?, Una nyumba?, Una gari?, Una...........???!!

Sajenti

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
3,651
412
Juzi jumamosi nilibahatika kumsindikiza rafiki yangu mmoja kwenda kujitambulisha kwa wazazi wa fiancee wake. Pamoja nami na bwana harusi mtarajiwa, tulikuwa pia na mjomba wa huyo rafiki yangu na kaka yake.

Tulipofika ukweni baada ya kukaribishwa na utambulisho mrefu, kwa kweli ilikuwa ni mjomba wa rafiki yangu kueleza kile kilichotupeleka pale. Na hilo lilipofganyika mbele ya wenyeji wetu ambao walikuwa wakitusubiri wake kwa waume...ndipo aliposimama mzee mmoja ninayemkadiria kuwa na miaka 50 -60 ambaye nilikuja kuambiwa baadaye kuwa ni baba mkubwa wa binti ambaye jamaa anamchumbia kwani baba yake mzazi alishatangulia mbele ya haki.....Kama utani mzee akaanza kumuuliza jamaa maswali ambayo baadhi yetu yalituacha hoi....Mambo yalikuwa kama ifuatavyo;

Mzee: Kijana una kazi?
Jamaa: Ndio mzee mimi ni mhandisi wa kampuni fulani
Mzee: Una nyumba?
Jamaa: Hapana mzee, bado sijabahatika kujenga lakini nina kiwanja tayari
Mzee: Una gari?
Jamaa: Hapana
Mzee: Uliwahi kuoa kabla ya kuja kumchumbia binti yangu?
Jamaa: Hapana
Mzee: Una mtoto uliyezaa huko nyuma?
Jamaa: Kimya kidogo,....baadaye ndio ninaye..
Mzee: Mchumba wako anafahamu hilo?
Jamaa: Hapana..
Mzee: Sasa wewe unataka kumchumbia binti yangu jambo kama hilo humuelezi mwenzio huoni kuwa unatengeneza bomu?...Inaelekea hauko serious wewe na kumuoa huyo msichana nadhani unahitaji kwenda kujipanga upya na ikibidi uzungumze na mwenzio....au unasemaje?

Huwezi kuamini wote tulikuwa kimya....baadae shangazi wa binti akaitwa na binti kusikia tu jamaa ana mtoto nje......mjadala ukawa mrefu lakini hatimaye jamaa alitakiwa kumueleza mchumba wake mbele ya kadamnasi ile ukweli na baadae mambo mengine yakaendelea lakini hali ilikuwa tete sana.....
 
Hao wazee mafala kweli, wanaaacha kumuuliza kijana kama mnara unashika network work wao wanaangalia material things. Shauri zao, wasilalamike mwanao akiwa ananyimwa unyumba sababu mshikaji network is not reachable
 
Kwa wazee wetu wa zamani wanajua hata nyie vijana mpendane haitoshi maana at the end of the day hamuwezi kula mapenzi.... Sasa si bora alimuuliza yoote hayo na issue ya mtoto imewekwa wazi.....

Dah! Am proud of the man, inaonesha ni muwazi na mkweli huyo binti inatakiwa kazi moja tu.... kumng'ang'ania....lol
 
Asha D huyo jamaa siyo muwazi ila nahisi alishindwa kuficha baada ya kuona jamaa wako serious, kama angekuwa muwazi angeshamwambia mchumba wake kabla.
 
Nlidhani ni tangazo la CRDB, we need 2 b open, hata mimi nasumbuliwa na ishu kama iliyo mpata mshkaji
...Unajua Bujibuji hata mimi wakati mzee anaanza kumlima jamaa maswali taswira iliyonijia kichwani ni ile ya tangazo la CRDB radioni lakini alipoingia katika vipengele vya umewahi kuoa? umewahi kuwa na mtoto nikaona kumbe mzee alikuwa anatuburudisha kwanza then akagonga jiwe kichwani....:biggrin1:
 
hakuna swali hata moja
linalo muhusu binti
wazee wengine bwana dahh

hayo ya nyumba sijui gari maswali gani hayo ..
 
Mpe pole jamaa...kweli huyo mzee ni very materialist, bora hata angemuuliza kijana anasali kanisa gani?
 
Hao wazee mafala kweli, wanaaacha kumuuliza kijana kama mnara unashika network work wao wanaangalia material things. Shauri zao, wasilalamike mwanao akiwa ananyimwa unyumba sababu mshikaji network is not reachable

Hivi hili nalo linatakiwa liulizwe, ina maana hawajakaguana.
 
hakuna swali hata moja
linalo muhusu binti
wazee wengine bwana dahh

hayo ya nyumba sijui gari maswali gani hayo ..
...Binti hawezi kuulizwa maana jamaa yeye ndio alijipeleka kwa wakwe watarajiwa kwa ajili ua kujitambulisha...So swali kwa binti likuja baadaye sana maana ya vumbi kutulia ndipo alipoulizwa kama anamfahamu jamaa na anakubali ombi la mshikaji kumtaka uchumba...maswali ni ya msingi kwa maisha ya sasa ya .com
 
Hivi hili nalo linatakiwa liulizwe, ina maana hawajakaguana.
...Mh! Hivi kuna uwezekano kijana wa siku hizi akaoa binti bila kumchakachua kidogo? Kwa sababu jamaa ni mshikaji wangu sana na yule dada amekuwa naye kwa takribani mwaka na nusu wanajuana vizuri sana mambo ya net work mambo zose si unajua tena!!
 
Unapoanzisha mahusiano na mwenzako ambaye unatarajia aje kuwa mkewe ni bora umweleze yale unayojua yanaweza leta utata baadae kama unajua una mtoto mweleze mwenzako ajue. kuliko kusikia kwa watu wengine
swala la mtoto si kitu cha kuficha ipo siku kitajulikana
 
Hakuulizwa ana Tembo card master card lol matangazo mengine yanawaharibu hadi wazee wetu
 
kwa hayo maswali mengine mzee aliyomuuliza huyo kijana sio ya kuuliza kwani kwa sisi vijana wa sasa mkijafika wakati wakutambulishana mnakuwa mnajuana so mengine asingeuliza la msingi angemuuliza mwana kama anampenda yule kijana na kama yupo tayari kuishi nae mke la msingi ni upendo mengine majaaliwa.
Ila na wanaume mnatakiwa muwewakweli kwa wenza wenu kama unatarajia kufika nae mbali au kama mnataka muanzishe familia pamoja sio sawa kumficha mwenzako hasa kwenye swala la mtoto kwani hilo ni pembe halifichiki so huyo jamaa alikosea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom