Una gari au biashara msaada wako ni muhimu tafadhali,

Una gari au biashara msaada wako ni muhimu tafadhali,

GENTLEMAN S

Member
Joined
Feb 19, 2014
Posts
47
Reaction score
8
Habari za muda huu ndugu wanajf,
mimi ni kijana mwenye familia tayari,
nimefanya kazi na kampuni moja ila ikapunguza wafanyakazi,
nina ujuzi wa kuendesha magari aina zote nina leseni daraja la 2(class C ),pia ni fundi magari,
ninahitaji msaada wenu uwe wa mawazo wa kazi au wa mkopo niweze kuanza biashara,
kwa mtu mwenye gari ninaweza kumfanyia biashara na kumpatia kiasi kizuri cha pesa,
pia ninaweza kufanya kazi aina yeyote iliyo halali..
Tafadhali nisaidieni,familia yangu inateketea.
 
Duh,mpaka leo bado watu wamekuchunia mkuu.
Maana naona ukiwahi kupost hii issue muda mrefu sana.
Kukusaidia kwa mawazo ya watui wengine hembu weka haya yafuatayo
-Umri wako
-Mbali na magri una ujuzi gani
-Mke anaujuzi gani,au amewahi kufanya biashara gani,maana inaweza kuw anjia ya msaada pia,kuna wake vichwa.
Maana unaweza kukuta mke akapewa mtaji wa elf 50 basi huwezi kuamini akapika vitumbua,au maandazi akasimia familia huku wewe ukiendelea kutega issue zako,sasa unapotaka msaada sio ujiangalie wewe peke yako,angalia na mkeo anaujuzi gani,inaweza ikawa ni njia ya yeye kukupa ahueni,mie nakupa mfano mdogo.Maeneo ya Buguruni kuna dada mmoja alikuwa nategengeza Ice cream na kuuza shulei,yaani mtaji wake haufiki hata elfu kumi,lakini alijiweza na alisaidiwa na mama mmoja wa maeneo yale bila hata kumchaji kitu,maana umeme hata kama ataweca Ice cream zake basi hauna tofauti namatumizi yao,maana friji linakuwa wazi vile vile.Fikiria sana hili.
-Udhaifu wako upo wapi,maana usije kuwa mlevi ukategema kwamba kuna salama
-Ulajiriwa kwa miaka mingapi kabla ya kuachishwa
-Katika ajira ulifanya nini la maana au la kumbukumbu kwako,maana wengine kwenye ajira hata ushauri wa mke hamtaji,ukifilisika ndio unakuja kukaa na mke eti mpange maisha
-Familia yako ni kubwa kiasi gani
-Mnakaa maeneo gani ya mji
-Mnaishi kwenye nyumba ya kupanga au yako,na kodi kiasi gani kwa mwezi na mmechukua vyumba vingapi
 
WALIOTIMULIWA NI MADEREVA WOTE? coz ninavyojua kipindi cha labour redundancy wanaoadhirika ni wenye mapungufu katika utendaji... je ulikuwa mwajibikaji kweli?
 
Back
Top Bottom