UN yataka mauaji ya Watanzania DRC yachunguzwe

strong ruler

JF-Expert Member
Nov 2, 2013
4,921
3,305
ImageUploadedByJamiiForums1454956580.998587.jpg

Umoja wa Mataifa umetaka uchunguzi wa kina ufanyike kuhusiana na ripoti ya wataalamu wa umoja huo inayosema kuwa askari 2 wa kulinda amani wa kimataifa kutoka Tanzania wameuliwa na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Maman Sidikou, mkuu wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko DRC amesema ni jambo la kusikitisha kuona panajitokeza mgongano mkubwa kati ya askari wa kulinda amani na jeshi la serikali ya DRC kiasi cha pande mbili hizo kufyatuliana risasi. Sidikou amesema ripoti ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa, wanajeshi hao kutoka Tanzania waliuawa baada ya kushukiwa kuwa na uhusiano na waasi wa ADF-Nalu kutoka Uganda. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, walinda amani kutoka Tanzania walikuwa wakiwapa silaha waasi hao.

Kamati ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa ililiandikia barua ya siri Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ikilalamikia hatua ya wanajeshi wa Tanzania ya kuwasaidia waasi na kudai kwamba wanajeshi hao ambao ni sehemu ya askari wa kulinda amani wa kimataifa huko DRC walichangia kuuawa wanajeshi 31 wa serikali ya Kinshasa mwezi Mei mwaka jana.

Chanzo:idhaa ya kiswahili radio tahran.
 
hii mbona kama habari ya siku nyingi,,,maaana jeshi la tz kuhusishwa kuuza silaha kwa waasi mbona halijaanza leo
 
Back
Top Bottom