EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,357
Brigedi ya Uingiliaji Kati ya Umoja wa Mataifa inayopambana na vikundi vyenye silaha mashariki ya Congo kikiwemo kikundi cha M23 itaundwa na wanajeshi 3,069 na kuongozwa na jenerali wa Kitanzania
Kwa mujibu wa Madnodje Mounoubai, msemaji wa Misheni ya Udhibiti ya Umoja wa Mataifa Afrika ya Kusini, Tanzania na Malawi kila moja itatuma kikosi cha askari wa miguu 850. Wanajeshi 519 waliobakia watatawanywa katika kikosi cha mizinga, kikosi cha askari maalumu na kikosi cha uchunguzi.
Wakati huo huo, M23 imeionya Tanzania ijitoe katika mipango ya kuchangia wanajeshi katika brigedi hiyo.
kiongozi wa masuala ya kisiasa katika kikundi cha M23, Bertrand Bisimwa ameionya Tanzania katika barua ya tarehe 11 Aprili kwenda kwa Rais Kikwete, kuwa "kila mara wamekuwa wakijitayarisha na vikosi vikubwa zaidi na vyenye silaha bora".
Katika barua hiyo Bisimwa aliandika "Jambo kama hilo litaifika Brigedi ya Uingiliaji Kati ikiwa hekima zenu hazitajikinga na kuingilia kati na kuacha michezo hii ya hatari katika safari zake".
"Kwa sababu hii, M23 inawaalika wabunge na watu wa Tanzania kufikiria tena hali hii kwa makini na kuishawishi serikali ya Tanzania... kutopeleka watoto wa kiume na kike katika taifa hili linaloheshimika ili kujihusisha na vita vya kipuuzi dhidi ya kaka zao wa Kongo," ilisema barua hiyo.
Siku ya Ijumaa M23 ilionya kuwa italipiza kisasi ikiwa watashambuliwa na kikosi cha kuingilia kati, ambacho kilipewa kazi ya kulinda wananchi.
Umoja wa Mataifa wasisitiza kuhusika kwa Tanzania katika DRC - Sabahionline.com