Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,505
- 9,286
Ripoti mpya ya wataalam wa Umoja wa Mataifa imeeleza kwamba takriban watoto 2,000 waliosajiliwa na waasi wa Kihouthi wa Yemen kuwa wapiganaji, walifariki vitani, kati ya Januari mwaka 2020 na Mei mwaka 2021.
Ripoti imeeleza zaidi kwamba waasi hao wanaoungwa mkono na Iran, wanaendeleza kambi za kuwasajili na kuwahimiza watoto kushiriki vita.Kwenye ripoti hiyo iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana, wataalam wamesema walichunguza baadhi ya kambi shuleni na vilevile msikiti, ambao Wahouthi hutumia kueneza nadharia zao na kuwasajili watoto.
Wataalam wameeleza kwamba walinakili visa 10, ambapo watoto walipelekwa kupigana, baada ya kuambiwa watasajiliwa katika kozi za tamaduni.Jopo hilo la wataalam limesema lilipokea orodha ya watoto 1, 406 waliokufa vitani mwaka 2020 baada ya kusajiliwa na Wahouthi na vilevile orodha ya watoto 562 waliokufa kati ya Januari mwaka jana hadi Mei mwaka jana.
Vita vya Yemen vimedumu kwa miaka saba sasa.