#COVID19 UN: COVID-19 haikupunguza kasi ya mabadiliko ya tabianchi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Umoja wa Mataifa umesema janga la virusi vya corona halikupunguza kasi ya mabadiliko ya tabianchi. Katika ripoti iliyotolewa na umoja huo leo Alhamisi, imearifiwa kuwa utoaji wa hewa chafu ya kaboni katika sekta ya viwanda ulibaki katika kiwango kile kile cha mwaka 2019. Kitengo cha hali ya hewa cha Umoja wa Mataifa kimesema mlipuko wa COVID-19 ulipunguza kidogo tu viwango vya hewa ya kaboni mwaka uliopita wa 2020.

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa ambayo inabainisha data za kisayansi kuhusiana na mabadiliko ya tabianchi, imesema uzalishaji wa hewa chafu kutoka viwandani, kati ya mwezi Januari na Julai mwaka huu, ama iko katika kiwango kile kile cha mwaka 2019, au imekipita.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ripoti hii mpya inaonyesha namna jumuiiya ya kimataifa ilivyopotea njia katika mapambano ya kuzuia ongezeko kubwa la joto duniani.
 
Back
Top Bottom