Umuhimu wa mafuta mwilini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umuhimu wa mafuta mwilini

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Oct 20, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 20, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  KATIKA mtazamo wa kawaida wa watu wengi, hupenda kujiepusha na ulaji wa mafuta kwa kila hali. Pamoja na tahadhari wanayochukua hujikuta wamelazimika kula mafuta bila ya kupenda. Kutoyataka mafuta kabisa kunatokana na elimu duni ya lishe, na matangazo ya kuogofya kuhusu madhara ya mafuta. Lakini je unafahamu umuhimu wa mafuta mwilini? Miongoni mwa vyakula vilivyosahauliwa na watu, basi mafuta ni kimojawapo. Ndugu msomaji utakubaliana na mimi kuwa iwapo utaambiwa uorodheshe vyakula unavyovifahamu, bila shaka mafuta usingeyataja.

  PAMOJA na kutoorodheshwa, si kwamba havitumiwi. Takribani watu wote hula mafuta aidha moja kwa moja na kwa njia nyingine.

  Mafuta yamegawanyika katika aina mbili; yenye asili ya wanyama na mfano mafuta ya ng'ombe (samli), mafuta ya samaki, kondoo n.k. Yenye asili ya mimea ni kama mafuta ya karanga, ufuta, maharagwe, alizeti, pamba n.k.

  Vilevile mgawanyiko mwingine ni umajimaji na ugumu (mgando) mafuta ya maji kama mpishi korie, mgando kama kimbo na blue bendi.

  Kwa kawaida mwili una uwezo wa kutengeneza mafuta wenyewe kwa kutumia vyakula mbalimbali mfano vyakula vya wanga na sukari. Pamoja na kuwa na uwezo huo wa kujitengenezea mafuta wenyewe, mwili unahitaji aina fulani ya mafuta isiyoweza kuyatengeneza (essential fat-acids). Na mafuta haya yanahitajika sana mwilini kwa kazi mbalimbali. Na mafuta haya yanapatikana katika vyakula mbalimbali tunavyokula. Moja kati

  ya kazi za mafuta haya yasiyotengenezwa na mwili ni utengenezaji ya chembechembe za mwili. Hasa chembechembe za mishipa ya fahamu na ubongo (nerves). Mfano watoto wadogo ambao bado wanakua ubongo na sehemu zingine za mwili, hujitaji sana mafuta haya. Vilevile husaidia kazi za ulinzi wa mwili kufanywa ipasavyo. Kwa upande mwingine mama wajawazito huhitaji sana mafuta haya kwa ajili ya makuzi ya mtoto aliye tumboni.

  Pamoja na hayo mafuta yote kwa ujumla yana kazi mbalimbali mwilini. Kazi zake ni kama ifuatavyo. Ni chanzo kizuri cha nguvu mwilini. (9.4 K cal/g). Pamoja na kuwa vyakula vingi vina uwezo wa kutoa nishati ya nguvu, lakini mafuta hutoa zaidi.

  Mafuta husaidia ufyonzaji wa vitamini mwilini. Kula vitamini ambazo haziyeyuki mpaka kuwe na mafuta (A,D,E,K). Hivyo basi kuwepo kwa mafuta kwenye vyakula vilivyo na vitamini hizi, huweza kuyeyuka na hivyo mwili kuzifyonza na kuzitumia kama inavyohitajia.

  Na iwapo mafuta hayatakuwepo, kuna uwezekano wa vitamini hizi kutolewa kama makapi. (Vitu visivyohitajika mwilini!). Hivyo ndugu msomaji ni jambo la kuzingatia sana, katika kukamilisha kama inavyoshauriwa na wataalam.

  Mafuta huongeza uimara wa mwili kwa kuunganisha sehemu mbalimbali za mwili. Mwili ni mkusanyiko wa viungo mbalimbali. Mfano, moyo, ini, figo, mapafu, ngozi, matumbo, koromeo n.k. Vyote hivi hufanya tofauti kwa kuushirikiana na hatimaye kufanikisha shughuli za mwili mzima. Bila ya hivyo viungo hivi vingekuwa vikining'inia bila msaidizi katika kishiko.

  Mafuta hutumika kama kizuizi cha mwili na sehemu mbalimbali. Mara nyingi huzizunguka sehemu za mwili ili kuzipa uzio (kizuizi) mfano moyo, mishipa ya fahamu na mafigo. Mara tu baada ya ngozi kunatabaka la mafuta ambalo huzuia mwili usipoteze joto lake kirahisi au joto la nje kuathiri mwili kiurahisi. Hivyo mafuta. Hutumika kama blanketi (insulator). Mfano unaweza kuupa kwa watu au wanyama waishio nchi zenye barafu kama Amerika ya Kaskazini huwa na tabaka kubwa sana la mafuta.

  Mafuta huongeza ladha ya chakula, na hivyo kuusaidia mwili kujitayarisha kukishughulikia chakula ipasavyo. Vyakula vilivyo na mafuta hunukia vizuri na kumvutia mlaji. Pia huongeza rangi ya vyakula kuonekana vizuri na kuleta mvuto wa kuvila. Ndugu msomaji utakubali kauli yangu, kwa mfano matembele, wali au mbatata iliyopikwa bila mafuta inavutia aidha kwa harufu au rangi ya viungo vyake? Na je ladha yake unapotia mdomoni inapendeza kukufanya utake zaidi ukifananisha na vyakula kama hivyo vilivyopikwa kwa mafuta? Bila shaka utakuwa umegundua kitu. Hiyo ni kazi yako binafsi.

  Mafuta husaidia vyakula vibaki mwilini kwa muda mrefu zaidi. Vyakula vyenye mafuta hucheleweshwa katika uyeyushaji wake. Na hivyo hufanya viwepo tumboni muda mrefu kidogo. Mfano mkate wa siagi si sawa katika kushibisha kama mkate mkavu usio na siagi. Au uji wa maziwa ambayo yana mafuta si sawa na uji wa unga mtupu. Uji mtupu huchukua takribani nusu saa kisha mtu hutaka kwenda haja ndogo.

  Vilevile mafuta husaidia kulainisha ngozi zetu. Hakika iliyokakamaa hupasukapasuka na kuuma, na hata kuwa rahisi kuingiwa na wadudu mbalimbali wa magonjwa. Pamoja na kupaka mafuta yetu, bado hata usipopaka mafuta mwili hautachanika sana. Labda kwa sehemu zenye joto jingi.

  Kwa ufupi hayo ndiyo manufaa mwili uyapatayo kutoka mafuta. Hivyo ndugu msomaji kumbuka kuupatia mwili wako vyakula ambavyo vina mafuta ili aweze kunufaika navyo. Asiyeelewa mweleweshe ili siku ukisahau akukumbushe.
   
 2. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Dahh! Mafuta haya haya yalonifanya niachike kwa obesit!!!
   
 3. m

  majogajo JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2011
  Joined: Oct 9, 2011
  Messages: 321
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  mbona cjaona yanasaidije kuongeza nguvu za kiume?
   
 4. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hayo hayo mwaya kila kitu kwa kiasi.
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,233
  Trophy Points: 280
  MziziMkavu.............mafuta husaidia kulainisha kinyesi...................na wale ambao hawali kabisa mafuta husumbulia na kinyesi kigumu ambacho chaweza hata kunyofoa sehemu ya maumbile yao na kusababisha utokwaji wa damu na hata wao kudhani pengine wanasumbuliwa na magonjwa ya tumbo au kansa................lakini kila kitu ni kwa kiasi kama[MENTION] Gaijin[/MENTION] alivyonena...........
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Aasante kaka,nimejifunza kitu!
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  May 19, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  asante kwa darasa mie natumia olive oil zaidi njoo na faida na athari zake basi.....
   
Loading...