Umuhimu wa kila Shule kuwa na Shamba

Umuhimu wa kila Shule kuwa na Shamba

Ryan The King

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
2,789
Reaction score
2,706
Habari Great thinker!

Napanda Jukwaani kichwani nikiwa nimeibeba mada hapo juu.

Shule ina miundo mbinu mingi ya kufundishia na kujifunzia. Miongoni mwa miundo mbinu hiyo ni pamoja na Maabara, maktaba, Madarasa Viwanja vya michezo n.k.

Miundo mbinu hii husaidia ufanisi wa Shule kitaaluma.

Mbali na Miundo mbinu hiyo, pia kuna Suala la uwepo wa Shamba Katika Shule. Ni muhimu sana kwa shule kuwa na Shamba.

Watoto wa sasa wengi ni Wavivu sana. Haiwezekani Shule ipo katika Ukanda wenye ardhi yenye rutuba na tabia ya nchi nzuri kama Songea, Rukwa, Katavi, Lindi, Mtwara na Morogoro Miongoni mwa Mikoa mingine. Shule nyingi hazina Mashamba na huenda yapo lakini Hayatumiki. Alafu jamii inahitaji serikali itoe chakula. Huu ni Umasikini.

Miaka ya zamani Kidogo kila shule kuanzia Msingi mpaka shule ya juu ya upili kulikuwa na Mashamba yaliyozalisha chakula kingi kitoshacho kwa Shule. Leo kwa nini Mashamba yamepotelea wapi? Kwa nini hayalimwi?

Napendekeza Serikali ianzishe tena Mfumo huu wa Kila Shule iwe na Shamba lake. Na kama Shamba lipo basi Lifanyiwe kazi.

Manufaa ya Kuwa na Shamba shuleni;

1. Chanzo cha Chakula.
Endapo Shule itakuwa na Shamba basi uwezekano wa kupata chakula upo. Shule za Msingi na sekondari zitajipatia chakula bila kutegemea Vyakula kutoka nje.

2. Sehemu ya mafunzo.
Wanafunzi watapata Stadi za Kilimo ikiwa watahusishwa na Kilimo cha Shamba lililomo Shuleni. Hii itawasaidia hata wakimaliza wanaweza kujiajiri katika sekta ya kilimo endapo watakosa ajira.

3. Kupunguza Ongezeko la Wavivu.
Shamba litaongeza ari ya uchapakazi kwa watoto. Uvivu utapungua kwa kiasi Kikubwa. Watoto wengi wa Sasa ni wavivu kutokana na sababu ya kutokufanya kazi shuleni. Shuleni hawana kazi zaidi ya kufagia tuu.

Yapo manufaa mengi ya kuwa na Shamba shuleni. Shamba ni moja ya miradi muhimu ipaswayo kuwapo shuleni. Miradi mingine ambayo yaweza kuwepo ni pamoja na ufugaji.

Mytake: Serikali isisitize Jambo hili kwani linafaida kubwa sana kwa Shule husika, jamii na taifa kwa ujumla. Serikali itoe pembejeo na maafisa Ugani ambao watasaidia jambo hili.

Pia Na Mashamba ya Kijiji yafufuliwe ili vijiji vipate chakula.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom