Umri wa kujiunga na mgambo

MEING'ATI

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
1,212
1,009
Hi wadau!

Naomba kueleweshwa kwa wadau kuhusu hii kitu inaitwa mgambo. Je umri wa kujiunga ni kuanzia miaka mingapi?

Na je mtu ambaye hapaswi kujiunga anatakiwa awe na miaka mingapi? Pia je kama mtu ana matatizo kama maginjwa ya akili na magonjwa kama kifua figo na ini anaruhusiwa?

Mwisho kuna tetesi hao wanawapigaga raia hadi kufa na hata kupata kilema ya kudumu je pa kuwashtaki ni wapi?
 
Umri wa kujiunga na mafunzo au kwa lugha nyingine "kucheza mgambo" kisheria ni kuanzia miaka 15 hadi 54.
Mafunzo hayo siyo ya lazima ni ya hiyari.

Kabla ya kuanza mafunzo, wanafunzi wanastahili kupimwa afya zao na daktari na kisha kupewa alama za "fit" au "un fit" kutegemea na afya ya mhusika.

Na waliopata alama za "fit" ndiyo huruhusiwa kuanza huo mtanange.
Umri wa kustaafu mgambo ni miaka 55.

Kama haujaelewa pahala, ama kwa ajili ya ufafanuzi, karibu.
 
Hapa nimeoenda mumbe hawa wanaotuambia huku mtaani ni lazima wanatoa wapi huo msemo
 
Hilo neno "lazima" ni la kisiasa, lakini ukweli kisheria mafunzo ya mgambo ni ya hiyari.

Ngoja nikwambie inavyofanyika:
Kinapofika kipindi cha mafunzo hayo, mshauri wa jeshi la akiba ambaye ni mjumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, hulipeleka jambo hilo kwenye meza ya mwenyekiti ambaye ni DC.

Likiishakupata baraka, basi huyo mshauri hutafuta wagambo waliomaliza mafunzo ya uongozi wa Mgambo ili kusaidia kufundisha wanafunzi wanamgambo wapya.

Hao wakufunzi wanamgambo hufundisha kwa kujitolea na malipo ya posho zao ni faini mbali mbali zinazotozwa kwa watoro wa kila siku na wanaostahili (registered)lakini wakakaidi mafunzo.

Kipindi hicho cha mafunzo, kuna kauli kama hizo za mafunzo ni "lazima" ili ukijichanganya utozwe kwa ajili ya wakufunzi.

Kifupi jambo hilo ni hiyari, na kama hautaki kushiriki, sema wazi hata bila kisingizio kuwa "sipo tayari kushiriki", uone kama watakupeleka popote.

Kama kutakuwa na ubabaishaji zaidi, waambie wakuoneshe maandishi yanayohusu sera za mgambo ni wapi ilipoandikwa "mafunzo ya ngambo ni ya lazima"? Hakuna, bali imeelezwa wazi kuwa mafunzo hayo ni ya hiyari na kama kuna faini yoyote ya kibabe, pambana na ukatae kutoa.

Wakikuona una mwamko, watakuvutia nyuma ya jengo ili "usimwage mtama kwenye kuku wengi" na kukufukuza uende zako!
 
Upo njema!
 
IUmeeleza vema ila huku tunataka tuhamie kenya maana watu wanashikwa kwa lazima hata huku mtaani halafu tunaambiwa hata kama hutaki watakuja kutushika manyumbani na wakikupeleka wanakumwagia maji mavhafu na matope vijana wametoka huko full matooe hii imewafanya wengi kutorikea kenya hii hali kabisa sio njema sijui itafikia wapi? Wanasema wanatak watu 500 tayari wako mia tu ivo watafanya msako wa nyumba kwa nyumba hapa wagumu tunasubiri holio ya nyumba kwa nyumba ama tutorike haka kamji ketu kwanza hii nchi imejaa uholela na ukanyagaji wa sheria
 
Back
Top Bottom