NGAYANIMO
Member
- Feb 17, 2026
- 42
- 58
MUUNGANO WA WATANZANIA " JUMA NATURE & PROFESSOR JAY "
Umoja wa Tanzania" ni wimbo maarufu wa Bongo Fleva uliotolewa mwaka 2003 na mkongwe Juma Nature akishirikiana na Professor Jay, ukiwa kwenye albamu ya Ugali,
Uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi uliofanyika 1958 na Tanu ilifanikiwa kupata ushindi mnono baada ya kupata viti 28 kati ya viti 30 vilivyokuwa vikishindaniwa. Mwaka 1960 ulifanyika uchaguzi wa wabunge na Tanu kikaendeleza ushindi wake kwa kupata viti 70 kati ya viti 71 vilivyokuwa vikishindaniwa..
Julai mwaka 1992 serikali ya Tanzania iliutangazia ulimwengu kuwa imerejesha mfumo wa siasa za vyama vingi, kisha mwaka 1995 uchaguzi mkuu wa kwanza uliovishirikisha vyama vya upinzani ulifanyika.
Matukio hayo muhimu katika maisha ya wananchi wa Tanzania yamefanyika ndani ya miaka 60 tangu ilipopata uhuru. Kwamba katika kipindi cha miaka 60 wananchi walishuhudia kufutwa siasa za vyama vingi wakati wa utawala wa rais wa kwanza wa nchi hiyo Julius Kambarage Nyerere aliyedumu madarakani miaka 24
Kisha siasa hizo zikarejeshwa katika kipindi cha utawala wa rais wa pili, Ali Hassan Mwinyi chini ya Tume ya Jaji Francics Nyalali, huku Mwalimu Nyerere akiwa kinara wa kuunga mkono siasa hizo.
Tangu ufanyike Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa vyama vingi 1995, uhusiano wa vyama vya CCM na CUF umekuwa wa vuta-nikuvute. CUF inalalamika kuibiwa kura mara zote, huku CCM ikijinasibu kupendwa na wananchi ndiyo maana imekuwa ikishinda.
Umoja wa Tanzania, wimbo uliolenga kupatanisha mgogoro wa kisiasa kati ya vyama vya CCM na CUF
CUF ilianzishwa mwaka 1992 kutokana na maungano ya shirika mbili.
Hizi zilikuwa ni:
1. KAMAHURU kikundi cha kupambania demokrasia kwenye visiwa vya Unguja na Pemba
2. Civic Movement iliyokuwa kundi la kupigania haki za binadamu la Tanzania bara.
Professor jay " UMOJA WA WATANZANIA"
"Angalau sasa Maumivu Nayasahau/
Tanzania tumejitoa kwenye kashfa na Dharau/
Umoja wa Watanzania Sasa umejijenga Tena/
Tumshukuru Mwenyezi ndicho ninachoweza kusema/
Vifo vya wezetu ni makovu yasiofutika/
Lakini Tukiwa Pamoja Na Amini tutafarijika/
Siasa isiwe chanzo cha kuleta umwagaji Damu /
Naomba Watanzania hilo muweze kulifahamu/
Tulipoanzisha Vyama vingi kuleta hoja Nyingi/
Kwa madhumuni ya kuhakikisha Tu zipo Haki za Msingi/
Sidhani kama mlianzisha kuleta mapingano/
Msije mkageuza Siasa kuwa mikingamo/
Aluta continue mapambano yanaendelea/
Ni uchumi na kijamii Hakuna tunachongojea/
Mtuongozeni Vyema kwenye Ngazi za kimataifa/
Kwani tunafarijika nchi Yetu ikipata Sifa/
Msikatane mapanga wala msikamate mtutu/
Wote ni kitu kimoja hakuna mtusi wala muhutu/
Hivyo watanzania mwenyezi Mungu tuonyeshe njia /
Bariki kizazi hiki na Umoja wa Watanzania/
Amen..
NB: Mikingamo ni sauti ya umma,.
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202