Umoja wa Ulaya wapongeza utumbuaji wa Rais Magufuli

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
download-1.jpg

Umoja wa Mataifa ya Ulaya umepongeza hatua zinazochukulia na rais Dkt. John Magufuli,katika kudhibiti vitendo vya rushwa nchini na kuahidi kutoa misaada zaidi ili kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi.

Pongezi hizo zimetolewa Jijini Mwanza na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguezi pamoja na Mkuu wa idara ya siasa na mawasiliano wa umoja wa ulaya walipomtembelea Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella.

Licha ya Kupongeza hatua hizo za rais John Magufuli katika kupambana na rushwa Ujumbe huo wa Umoja wa ulaya umetaka serikali iweze kuchukua hatua zaidi dhidi ya wale wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema kuwa hiyo ni fursa kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza katika kuchangamkia fursa za miradi inayofadhiliwa na Umoja huo lakini pia ni njia moja wapo ya kudumisha mahusiano ya Kimataifa.

Pamoja na mambo mengine Umoja huo wa Ulaya umetembelea mkoa huo kwa ajili ya kuangalia fursa za uwekezaji ambapo umeiomba serikali ya Tanzania kuondoa urasimu katika upatikanaji wa vibali vya uwekezaji.
 
Safiiii, mambo Ndio haya tunapenda, Kazi nzuri lazima ipewe pongezi.
Rais wabane mpaka waseme poo!!
 
Nyumbu hawakosi la kusema baada ya wafadhiri wao wa sharti la ndoa ya jinsia moja kukosa chance
 
Safi sana.

Dunia imeanza kumkubali Anko Magu mdogo mdogo
Walijaribu kumtingisha kwenye MCC lakini jamaa hakutingishika.

Kwa sasa wameamua kushusha silaha na kujiunga kwenye safari ya Rais Magufuli.

Juzi Rais Magufuli wakati akiongea na polisi na waendesha mashitaka alisema ameongea na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron na wakakubaliana kuhusu njia za kuimarisha Jeshi la Polisi.
 
View attachment 344422

umepongeza hatua .. Dkt. John Magufuli,katika kudhibiti vitendo vya rushwa nchini na kuahidi kutoa misaada zaidi ili kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi.

Umoja wa ulaya umetaka serikali iweze kuchukua hatua zaidi dhidi ya wale wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.

Asante JPM. Keep it.

Dont leave a stone unturned!

Walete Wafdhili wengine /warudi tupate Maendeleo
 
Vitu vingine vikienda kusemewa kwa mkuu wa mkoa vinakuwa kama soga tu...
 
Walijaribu kumtingisha kwenye MCC lakini jamaa hakutingishika.

Kwa sasa wameamua kushusha silaha na kujiunga kwenye safari ya Rais Magufuli.

Juzi Rais Magufuli wakati akiongea na polisi na waendesha mashitaka alisema ameongea na Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron na wakakubaliana kuhusu njia za kuimarisha Jeshi la Polisi.

Ndiyo wanaobeza jitihada za Magu waelewe kuwa PM Cameron anaweza akaongea na JPM bila ya yeye kuhitaji kusafiri kwenda Uingereza na wakaweka sawa mambo muhimu kwa taifa letu. Naona na DFID wamekubali kusaidia mradi wa upanuzi wa Bandari ya Dar.

Lakini inawezekana Cameron pia alikuwa anaomba "poo" Standard Chartered Bank wasije wakatumbuliwa..
 
Nchi inasonga mbele wenye porojo wanazidi kupiga kelele.
 
TEGETA ESCROW,IPTL,Madini,Gas,Meremeta,EPA,Deep Green,Mabehewa,UDA...Moja ya hayo yakianza kushughulikiwa nitajua kuna nia ya dhati na Tanzania hii.
 
Ugonjwa wa Giri utakuua. Fanya kazi kwa bidii. Saidia familia yako na nina uhakika utaacha kulia lia.
 
Ni kipi hapo cha ajabu.Na ni kipi hapo hakijawahi kupata mjadala mpana hapa Tanzania,Ni kipi hapo kimeshughulikiwa kwa ukamilifu wake na kuona wahusika wanafahamika na kufikishwa mahakamani.

Mbona tunapenda cheap popularity bila kuzingatia masuala yaliyoifikisha Tanzania hapa ilipo.Mambo kama hayo niliyoyaorodhesha na mengine mengi ambayo bado hayajafahamika kwa wananchi ndio yaliyoifikisha Tanzania hapa ilipo.

Kama tunataka kusifiwa bila kikosolewa basi ujue kuna shida kubwa katika uongozi.JPM anaenda sawa ila kuna double standard.
 
Inaweza kuwa umeguswa maslahi yako ndio maana unasema double standard. Kama kunajipu unalijua litaje ili lilipuliwe. Au unasemaje Mtanzania mwenzangu. Badala ya kulia lia kila wakati na kushinda kwenye mitandao ukiwajadiri watu badala ya kufanya kazi. Unalitia umasikini Taifa.
 
pipo nyingne sijuh iko vepeee? inamfananisha rais na diwan, rais si kwa maslah ya chama bali the whole country, inashndwa support juhudi za przda zinasupport silly things, haki za binadam kwa mtu ambaye hakutenda haki kwa wanadam, nyie mazuzu ama? rais kp t up!
 
View attachment 344422

Umoja wa Mataifa ya Ulaya umepongeza hatua zinazochukulia na rais Dkt. John Magufuli,katika kudhibiti vitendo vya rushwa nchini na kuahidi kutoa misaada zaidi ili kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi.

Pongezi hizo zimetolewa Jijini Mwanza na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguezi pamoja na Mkuu wa idara ya siasa na mawasiliano wa umoja wa ulaya walipomtembelea Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella.

Licha ya Kupongeza hatua hizo za rais John Magufuli katika kupambana na rushwa Ujumbe huo wa Umoja wa ulaya umetaka serikali iweze kuchukua hatua zaidi dhidi ya wale wote watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo vya rushwa.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amesema kuwa hiyo ni fursa kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza katika kuchangamkia fursa za miradi inayofadhiliwa na Umoja huo lakini pia ni njia moja wapo ya kudumisha mahusiano ya Kimataifa.

Pamoja na mambo mengine Umoja huo wa Ulaya umetembelea mkoa huo kwa ajili ya kuangalia fursa za uwekezaji ambapo umeiomba serikali ya Tanzania kuondoa urasimu katika upatikanaji wa vibali vya uwekezaji.
Kweli kabisa, waanze na
Lugumi,
Escrow,
Rada,
Meli Chakavu,
Kagoda,
Meremeta,
Richmond Dowans,
EPA,
Nyumba za Umma,
Uhamishaji fedha kienyeji kwenda Wizara ya Ujenzi (Conflict of Interest) , Over spending Wizara ya Ujenzi kinyume na Budget.
Tuanze na hayo kwanza.
 
Back
Top Bottom