Umoja wa Ulaya waitega Tanzania

Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,353
2,846
Baada ya Tanzania kuonesha kutokuwa tayari kusaini mkataba wa EPA, sasa Umoja wa Ulaya umebuni mbinu mpya ya kumlainisha Rais na Serikali kwa ujumla, sasa Umoja huo umeamua kutoa " Msaada wa Sh. Bilioni 490" kwa kipindi cha miaka 4 ijayo.

Kumbukeni huu ni msaada na si mkopo, sasa serikali imeukubali, na umoja wa ulaya wanajipanga kwa sasa kuja tena rasmi nchini kumshawishi Rais na Serikali ili watie saini mkataba huo wa EPA, kama Tanzania itakuwa bado kichwa ngumu, basi, Umoja huo wa Ulaya utatishia kuufuta huo msaada wa Bilioni 490 kwa kipindi cha miaka 4 kuanzia mwaka huu, ndio maana UMOJA wa ULAYA wamekaa na kutafakari kwa kina na kuona kuwa huo uitwe " MSAADA" ili uweze kufutwa kirahisi ikiwa mambo yao hayatakubaliwa na Tanzania.

Jana, UMOJA wa ULAYA ulisema kuwa, wana Imani kuwa Tanzania, Burundi na Uganda zitatia saini mkataba huo.
 
Back
Top Bottom