Umoja wa taifa kwanza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umoja wa taifa kwanza!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ruhinda, Aug 30, 2012.

 1. R

  Ruhinda Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "Kila raia ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha uhuru, mamlaka, aridhi na umoja wa taifa....hakuna mtu atakayekuwa na haki ya kuwazuia raia wa Jamhuri ya Muungano kupigana vita dhidi ya adui yeyote anayeshambulia nchi." Katiba ya JMT ibara ya 28(1),(3)


  Leo
  napenda tukumbushane wajibu wetu wa kikatiba kama wana jamii, hasa jamii ya kitanzania ambayo kwa muda mrefu imesifika kwa amani, umoja na utulivu. Dibaji ya sera ya Utamaduni inaanza hivi, "Umoja, utulivu na mshikamano ambavyo watanzania tunajivunia vimetokana na utamaduni tuliojijengea." Kumbe Umoja tulionao ni matokeo ya mikono yetu, yaani ni matokeo ya utamaduni tuliojijengea sio waliotujengea.

  Neno "tuliojijengea" laweza kutafsiriwa kwa namna nyingi, maana mojawapo nikuwa watanzania wanao uwezo wa kufanya jambo likafanyika na likawa na matokeo makubwa chanya ama asi! Kwa uwezo huo toka enzi hizo tumeweza kujenga umoja, utulivu na mshikamano mpaka kufika hatua ya KUJIVUNA!

  Umoja, utulivu na mshikamano ni matokeo ya UTAMADUNI tuliojijengea. Kwa mujibu wa sera ya utamaduni, utamaduni ni "Mwenendo wa maisha ya jamii, mtazamo wao wa mambo na taratibu zao za kuendesha maisha zinazowatofautisha wao na jamii nyingine..."

  Kumbe mtazamo wetu wa mambo (siasa, dini, ukabila nk.) na taratibu zetu za kuendesha maisha ndizo tangu enzi zimezaa na kudumisha Umoja, utulivu na mshikamano wetu kama wanajamii. Mtazamo wa mambo ulijengwa katika misingi ya kikatiba, kwamba, "Kila raia ana wajibu wa kulinda, kuhifadhi na kudumisha uhuru, mamlaka, aridhi na umoja wa taifa."ni kwa kuzingatia wajibu huo hakuna mtu alieweza kuruhusu mambo yoyote mfano ya kisiasa, kidini au kikabila kutishia umoja wa taifa.

  Maana vitu hivi vinne; UHURU, MAMLAKA, ARIDHI na UMOJA WA TAIFA ni vitu vya msingi katika ustawi wa jamiii yoyote ile. Na ili vilindwe ni lazima mtazamo wa watu wa mambo hasa ya kidini, kisiasa na kikabila uwe wenye kushabihiana, kwamba umoja wetu, utulivu wetu na mshikamano wetu hauwezi wakati wowote kuvunjwa kwa misingi ya kisiasa, kidini ama kikabila. Hapa KUVUMILIANA (tolerance) huzingatiwa kwa masilahi mapana ya taifa.

  Hivi vitu vinne, kikubwa kikiwa UMOJA WA TAIFA, ni lulu ambazo tukizpoteza kuzipata tena, malipo makubwa yatahitajika. Sijui kama ukweli huu ndugu zangu tunaujua vema. Mifano mingi tunayo ya nchi waliocheza na Lulu hizi, leo hii wanajaribu kuzirejesha wanashindwa.

  Ninasikitika kuona kuwa watanzania tunaanza kuuacha utamaduni wetu wa kwanza ambao ulizaa hivi vitu vinne tunavyojivunia. Yaani mtazamo wetu wa mambo unabadilika siku hadi siku, badala ya kuona kuwa tunawajibu wa kulinda Umoja wa taifa, Uhuru wetu tunaanza kuwa na mtazamo kuwa IMANI zetu, VYAMA vyetu, MAKABILA yetu ndio vitu vya msingi na vya kupiganiwa. Tunaacha mambo ya msingi tunaanza kushabikia mambo yatakayotugawa milele!

  Humu JF utaona watu wakijaribu kulazimisha hoja hata ambayo si ya kidini au ya kikabila iwe hivyo, na kubadilisha mtazamo wa wachangiaji na kuamsha hisia zao na mwisho kuishia kutukanana kwa misingi ya itikadi zao za kidini, kisiasa na kikabila.

  Nionavyo mimi, kama hatutajirudi, simbali sana historia ya nchi yetu itabdilika, dibaji za sera zetu zitaandikwa upya, kwamba, "Vurugu, utengano na vita ya weneyewe kwa wenyewe tunayopigana ni matokeo ya utamaduni tuliojijengea...." Watoto wetu watakuja kujiuliza kama kuliwahi kuwepo taifa lililojulikana kama kisiwa cha amani. Watabaki kusoma vitabuni na kusimuliwa tu!

  Hapa JF kunasisitizwa uhuru wa kuongea. Na watu wanatumia uhuru huo bila kujua kuwa unamipaka. Mipaka ya uhuru huo huwa kwa mtazamo wangu katika mambo hayo manne ambayo ni wajibu wa kila raia kuyalinda. Kama mtu akiandika kwa kisingizio cha uhuru wa kuongea mambo ambayo yanatishia Uhuru wetu, Umoja wetu, mshikamano wetu mtu huyo atakuwa ni adui wa nchi yetu!

  Na kwa mjibu wa katiba yetu, "...hakuna mtu atakayekuwa na haki ya kuwazuia raia wa Jamhuri ya Muungano kupigana vita dhidi ya adui yeyote anayeshambulia nchi." Watu hawa tuwapige vita mahali popote walipo, iwe humu JF ama mahli popote hakuna wa kutuzuia, mods wapigeni ban futa thread zao wasionekane milele!

  Hakuna mtu anaqualify kuitwa GREAT THINKER kama hajui umuhimu wa kulinda Umoja wa taifa. JF ipo kwa ajili ya kutekeleza wajibu huo na si kinyume chake! Ndivyo ninavyoamini!

  Who is a great thinker anyway?
  To know a great thinker you need to examine his/her arguments. Argument means mature reasoning. One meaning of Mature is "worked out fully by the mind" or "considered" (American Heritage Dictionary). Mature reasoning, are thoughtful ones, reached slowly after full consideration of all the consequences. Therefore Great thinkers are
  1. Well informed 2. Are self critical and open to Constructive Criticism 3. Argue with their audiences in mind 4. Know their arguments' contexts.

  Great Thinkers please
  "UMOJA WA TAIFA KWANZA"
   
 2. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Well said Mkuu Ruhinda, if we could only learn to priotize our priorities, alot can be done.. Ni kweli at the end of the day ni maendeleo ya mmoja mmoja lakini, maendeleo hayo hutegemea umoja huo uliousema..suprisingly leo huku kubezwa kwa umoja huo(either kwa watu wenye nguvu kuwaonea wanyonge, kutosaidiana-yaani kuwanyanyua wanyonge kielimu, ajira nk) kumepelekea hapa tulipo na kuwa na matabaka mengi.
   
Loading...