Umoja wa Mataifa yashtumu matukio Uganda

GREGO

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
4,279
2,913
Umoja wa Mataifa umeelezea hofu kuhusu hali ya taharuki iliyotanda nchini Uganda hususan baada ya uchaguzi mkuu wa urais uliokamilika majuzi

Afisi ya haki za kibinadamu ya Umoja huo inaelezea wasiwasi kufuatia kuwepo kwa hali ya uhasama mkubwa baina ya rais wa jamhuri Yoweri Museveni na viongozi wa upinzani akiwemo kanali mstaafu Kizza Besigye.

Kuimeibuka taharuki kufuatia mauaji ya watu wawili na vilevile kamata kamata ya kiongozi wa upinzani daktari Kizza Besigye kufuatia kutangazwa kwa matokeo ya urais.

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda
Dakta Besigye amepinga matokeo ya uchaguzi akisema kuwa haukuwa wa haki na huru.
160222143118_kizza_bisigye_624x351_bbc.jpg

Katika taarifa yake Umoja wa mataifa unaelezea jinsi maafisa wa usalama wamekuwa wakitumia nguvu kupita kiasi wanapokabiliana na watu wasiokuwa na silaha ambao msimamo wao unaelekea upande wa chama cha upinzani FDC.

Kerry amlalamikia Museveni kuhusu uchaguzi
''Inatisha sana ukitizama shime ambayo polisi na jeshi la Uganda ilikuwa nayo ilipovamia afisi za chama cha FDC siku ya ijumaa '' taarifa hiyo inaelezea.
160222143324_kizza_bisigye_arrested_624x351_bbc_nocredit.jpg

Juma lililopita waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani John Kerry alizungumza na rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa simu na kumwelezea wasiwasi wake kuhusiana na matumizi ya nguvu kupita kiasi wanaposhughulika na wafuasi wa upinzani.

Aidha Kerry alizungumzia swala la uhuru wa viongozi wa upinzani mbali na kujadili hatua ya serikali kufunga mitandao ya kijamii siku ya uchaguzi.

Chanzo: BBC Swahili
 
Siasa za miafrika ndiyo zilivyo, na bado hata waking'ang'ania madaraka bado hawaboreshi maisha ya wananchi, wanakalia Wizi tu.
 
mara ngapi viongozi wa afrika wanatembeza bakuri nchi za mabara mengine?
Hahahaha hili swali gumu......siku zote ukiwa na shida lazima unyenyekee na kumsikiliza unaemuomba msaada
 
Back
Top Bottom