Umoja wa Mataifa: Watu milioni 24 huenda wakapoteza kazi kutokana na COVID-19

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,196
4,119
Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watu milioni 24 ulimwenguni wanaweza kupoteza ajira zao kutokana na athari za COVID-19.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na kazi ILO, limesema ukosefu wa ajira duniani unaweza kuongezeka kufikia watu millioni 5.3 katika kiwango cha chini na watu milioni 24.3 katika kiwango cha juu.

Janga la mlipuko wa COVID-19 tayari limeziweka biashara nyingi chini ya shinikizo, huku baadhi ya serikali zikiahidi hatua za kiuchumi kukabiliana na ukosefu wa ajira.

Mkurugenzi wa ILO, Guy Rider amesema janga hilo sio tu limekuwa mgogoro wa kiafya duniani, lakini pia ni janga kubwa katika soko la ajira na mgogoro wa kiuchumi ambao umekuwa na athari kubwa kwa watu. Kati ya watu milioni 8.8 na milioni 35 wanaweza kuwa katika umaskini wa kufanya kazi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu kutokana na athari za COVID-19.
 
Mhh huu ugonjwa ni hatari tunaanza upya kabisa kwa sasa nimepita Nchi za kusini huko siku za karibuni maduka makubwa yote yamefungwa wamebaki wale wabishi hali ni mbaya sana Nchi za Msumbiji na Malawi kabla hata ya Corona walishatangaza baa la Njaa sijui hali ikoje sasa hivi kwa kweli...
 
Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watu milioni 24 ulimwenguni wanaweza kupoteza ajira zao kutokana na athari za COVID-19.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na kazi ILO, limesema ukosefu wa ajira duniani unaweza kuongezeka kufikia watu millioni 5.3 katika kiwango cha chini na watu milioni 24.3 katika kiwango cha juu.

Janga la mlipuko wa COVID-19 tayari limeziweka biashara nyingi chini ya shinikizo, huku baadhi ya serikali zikiahidi hatua za kiuchumi kukabiliana na ukosefu wa ajira.

Mkurugenzi wa ILO, Guy Rider amesema janga hilo sio tu limekuwa mgogoro wa kiafya duniani, lakini pia ni janga kubwa katika soko la ajira na mgogoro wa kiuchumi ambao umekuwa na athari kubwa kwa watu. Kati ya watu milioni 8.8 na milioni 35 wanaweza kuwa katika umaskini wa kufanya kazi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu kutokana na athari za COVID-19.
Mchimba shimo kaingia mwenyewe
 
Back
Top Bottom