Umoja wa mashaka...

Umoja wa mashaka...

Tutor B

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2011
Posts
9,025
Reaction score
6,618
Siku moja walipita mbuzi wawili na kumkuta ng'ombe kafungwa ktk mti wenye majani wanayo yapenda sana na kila sehemu walipopita walishindwa kuyapata maana mti ulikuwa mrefu.

Walipofika ktk mtu ule wakamsalimia ng'ombe na kumwambia una faidi umefungwa ktk mti wenye lishe na shibe nzuri. Yule ng'ombe akawaambia wale mbuzi wawili nyie hamjui tu hapa napata majani yaliyo kwisha kukauka si matamu hata kidogo.

Kati ya wale mbuzi wawili mmoja akamwambia mbinu rahisi ili tuyapate yale majani ni wewe kusimama karibu na mti halafu mimi nakwea juu ya mgongo wako alafu nachuma majani kwa wingi.

Basi ng'ombe akakubali wapande ili UMOJA wao USHIRIKIANO wao ulete tija. Alaanza mbuzi wa kwanza akapanda ktk mgongo wa ng'ombe na kula majani mengi adi akashiba na kushuka chini kwenda kukaa pembezoni mwa mti.
Ng'ombe akashangaa na kumuliza yuke mbuzi aliyepanda mbona haujachuma majani na mimi nipate kula. Yule mbuzi akasema atachuma mwenzangu mimi nimechoka.
Akapanda na mbuzi wa pili naye vilevile kama alivyo fanya yule mbuzi mwenzake akala akashiba akashuka chini akakaa chini kwa shibe.
Yule ngombe akauliza mbona hayo majani mabichi sijapata na makubaliano mchume ila nyinyi mmekula mmeshiba.
Wale mbuzi wakamwambia yule ng'ombe wewe ni mkorofi sana ndomana wamekufunga kamba ktk mti huu mzuri ili utamani majani yake.
Wale mbuzi wakaondoka na kumwacha yule ng'ombe akiwa anajuta kuwa ngazi ya mafanikio yao.
Katika jambo la UMOJA ni vyema kuchunguza USHIRIKIANO wenu kama wote mmesimamia NIA zenu na kutarajia kufanikisha malengo yenu.
Mnaweza mkawa na UMOJA wa kufanya jambo ila kati yenu mmoja au watu kadhaa wakawa wanapiga REVERSE gari wakati nyinyi mnataka kusonga mbele adi kufikia kituo cha MALENGO yenu.

Jiulize kama taifa ..
Awamu ya kwanza (Ujamaa na kujitegemea) .... walituachia nini?
Awamu ya pili (Ruksa) .........................
Awamu ya tatu (Ubinafsishaji)
Awamu ya nne (Maisha bora kwa kila mtanzania)
Awamu ya tano (Hapa kazi tu) .......
Tunaachiwa nini? au tunaonekana sisi ni wakorofi ndo maana tumefungiwa kwenye nchi yenye utajiri na tukaendelea kuwa maskini?
Tafakari ...
 
😀😀😀
 
Msg yako haiendani na unachotaka kumaanisha....wenye akili watanielewa,ila sio rahis kwa huyo ng'ombe kuendelea kupandisha mbuz watatu wakat hapat anachotarajia....

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo ng'ombe ni wewe mwananchi wa kawaida utaendelea kuwapandisha mgongoni(kuwaweka madarakan kwa kuwapigia kura) hao mbuzi (viongozi wa serikali raisi, wabunge n.k) wale mpaka majani yote yaishe bila ya wewe kuonja hata kipande kidogo cha jani.

Maendeleo hayana chama
 
Umeamua kutoa ufafanuzi mkuu! Ahsante sana - kwa namna yoyote tuendelee kuwatoa tongotongo wananchi ili wajitambue. Nchi yenye utajiri mkubwa lakini wananchi wake maskini wa kutupwa. Alafu anaulizwa mtawala ni kwa nini wananchi ni maskini - anajibu eti hajui.
Kamba iliyomfunga mwananchi wa Tanzania ni ujinga unaoendekezwa na nyinyiemu. Tuukatae ili tuweze kula majani ya mti wetu kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom