Ummy Mwalimu itazame pia Gairo

Ummy Mwalimu itazame pia Gairo

MINENE BOY

Member
Joined
Jun 3, 2017
Posts
19
Reaction score
21
Nianze tu kwa kusema miongoni mwa mawaziri ninaowakubali hapa nchini ni huyu mama (Ummy Mwalimu).

Huyu ni miongoni mwa mawaziri wafuatiliaji sana kwenye shughuli zake za kila siku, hii mnaweza kuprove kwa namna alivyoanza na wizara ya TAMISEMI

TAMISEMI ni miongoni mwa wizara ngumu kabisa hapa nchini, lakini sina shaka na mwana mama huyu kuweza kuimudu wizara hii. Nimpongeze kwa kuanza na wakurungezi ambao hawataki kubadilika na mazingira (Hongera kwa hili).

Naomba nirejee kwenye kichwa changu cha habari hapo juu, kuna kasumba imezuka nchini kwetu siku za hivi karibuni ya mgogoro baina ya wateule wa rais (Ma RC, DC na DED). Kasumba hii isipodhibitiwa mapema inadhoofisha jitihada za maendeleo hapa nchini, lakini naona Ummy pia ameliona hili na ameanza kulifanyia kazi haraka sana.

Ummy Mwalimu nakuomba pia uitazame kwa macho yote mawili wilaya na Halmashauri ya wilaya ya Gairo. Wilaya hii imepasuka vipande vipande kuna ugomvi Kati ya DED na DC, ugomvi huu unaathiri sana utendaji kazi kwenye wilaya hii (ukipata muda fuatilia hili kwa ukaribu).

Mgogoro huu unawaathiri mpaka watendaji wa ngazi za chini kwani viongozi wao hawapo pamoja na wanafanya kazi kwa kuvutana. Kutokuelewana kwao kunawafanya viongozi hawa kuathiri shughuli zao za kila siku.

Mwisho, tunajenga nchi moja hatupaswi kugombania fito. Hakuna mtanzania zaidi ya mwingine sote sisi tuko sawa ndani ya nchi yetu. Tuheshimiane na tuthaminiane vyeo hivi ni dhamana tu leo upo na kesho haupo.
 
Tulia muziki bado unaendelea, We ongeza volume tu..

Sisiem watamalizana wao kwa wao.
 
kifupi ni kwamba afukuze DED wote Tanzania maana kila kona ni vilio
 
Serikali za majimbo zingefuta kabisa huu ujinga. Waziri wa TAMISEMI atatatua migogoro mingapi??
 
Back
Top Bottom