Ummy Mwalimu afanya Dua ya siku arobaini za Kufariki kwa Baba yake mzazi

Peter Dafi

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
392
272
UJUMBE WA MH WAZIRI WA AFYA MH UMMY MWALIMU KWA WATANZANIA WOTE JUU YA SIKU YA AROBAINI YA MZAZI WAKE.

"Ndugu zangu, napenda kuwafahamisha kuhusu "Arubaini" ya Marehemu baba yangu Mzee M.A Mwalimu itakayofanyika nyumbani kwetu, kijiji cha Mchukuuni, nje kidogo ya Jiji la Tanga Siku ya Jumamosi tar 26 March. Tutaanza na Hakiki (Dua ya kumuombea Marehemu) saa 2 asubuhi ikifuatiwa na Tahateem (kuhitimisha) saa 6 hadi 8 mchana. Karibuni sana hasa kwa ambao mtakuwa Tanga." Amesema Mh Waziri wa Afya Ummy Mwalimu.

Pia Ametukumbusha Ujumbe mzito wa Mungu!

"O our Lord! cover (us) with Thy Forgiveness - me, my parents, and (all) Believers, on the Day that the Reckoning will be established! [Ibraheem: 41]

Roho za Marehemu wote Zipumzike kwa Amani. Amina.....!
 
Kweli hapa inabidi ukawa tuweke Silaha chini tumpe pole mama yetu maana ndiyo utamaduni wetu watanzania, tupo pamoja mama yetu ingawa tupo nje ya tanga pole sana
 
Huyu mama wakati ule akiwa waziri wa maendeleo ya jamii alitembelea kituo cha kulea yatima kinaitwa MALAIKA, kipo wilaya ya Mkuranga mjini. Wale watoto jamani walikuwa na shida ya mashuka, basi mh. Ummy kawaahidi kuwaletea mashuka ambayo mpaka leo hajatimiza ahadi hiyo.
Wee mama ahadi ni deni, wakumbuke yatima wale!
 
Tumshukuru Mungu kwa Dua ya Alobaini shughuli imefanyika salama. Na tuzidi kuwaombea marehemu wote walotangulia mbele za haki
 
Huyu mama wakati ule akiwa waziri wa maendeleo ya jamii alitembelea kituo cha kulea yatima kinaitwa MALAIKA, kipo wilaya ya Mkuranga mjini. Wale watoto jamani walikuwa na shida ya mashuka, basi mh. Ummy kawaahidi kuwaletea mashuka ambayo mpaka leo hajatimiza ahadi hiyo.
Wee mama ahadi ni deni, wakumbuke yatima wale!

Sophia Simba alikuwa Wizara gani enzi hizo?
 
Back
Top Bottom